Hakuna aliyemtoa Diamond, ni jitihada zake binafsi na kuukataa ukandamizaji wa media na washikadau ndo vilivyomtoa

Dong Jin

JF-Expert Member
Jun 4, 2018
754
1,442
Diamond Platnumz ni one of the best musician kwa sasa Afrika Mashariki na Kati.

Kumekuwa na mijadala kibao eti Mond alitolewa na yule, akatolewa na huyu na porojo nyingi za namna hiyo lakini mbona hatuoni wasanii wengine waliotolewa na hao watu mnaowataja waliofika hata robo ya alipo Diamond?

Kitu pekee kilichomtoa Mond ni focus na jitihada binafsi ya kazi. Kitu kingine ni kuhangaika kutafuta koneksheni muhimu za kikazi (sio koneksheni za video ya Tiwa na mama J) na kama akiona unamkwamisha anakotaka kwenda anakutema kiroho safi.

Kifupi jamaa ndo kachonga njia kwa wengine kuserereka lakini wanaangushwa na pupa zao.

Kuna kijana wa kuitwa Marioo, akiendelea hv anaweza karibia levo za Mond.

BTW nabii hakubaliki nyumbani
 
Ukweli ulionyooka,

Kijana kapambana mwenyewe,juhudi binafsi,hulka yake ya kupenda ushauri na kusikiliza,ndio imemfikisha hapo,Kuna watu wanasema aaah alipewa koneksheni na fulani,sasa huyo fulani kwanini asitumie hiyo koneksheni Kufika alipofika Mond?

Juma nature,Daz nundas,gangwe mob,haya yote ni makundi yaliyokuwa na vipaji,na kama wangefata nyayo za Mond kipindi hicho(2000s)leo hii bongo tungekuwa mbali sana.

Watu wanasahau Daz baba alikuwa anamiriki gari la kifahari sana,Jeep kipindi hicho,Mond ajatoka.

Marioo, Na wengine wanaofata wakisikiliza kwa makini watafika alipo Mond na kumzidi,ipo siku Entertainment industry itatoa ajira nyingi kuriko hata serikali.
 
Haters watasema wewe ni Juma Lokole,
Lol.
Kawaida, hata sungura baada ya kurukaruka weee ili azidake ndizi, akaona yupo hoi bin taaban na hata afanyaje hawez fikia akaamua aseme sizitaki mbichi hizi...

Ukifanya poa lazima usifiwe
 
Ukweli ulionyooka,
Kijana kapambana mwenyewe,juhudi binafsi,hulka yake ya kupenda ushauri na kusikiliza,ndio imemfikisha hapo,Kuna watu wanasema aaah alipewa koneksheni na fulani,sasa huyo fulani kwanini asitumie hiyo koneksheni Kufika alipofika Mond?
Juma nature,Daz nundas,gangwe mob,haya yote ni makundi yaliyokuwa na vipaji,na kama wangefata nyayo za Mond kipindi hicho(2000s)leo hii bongo tungekuwa mbali sana.
Watu wanasahau Daz baba alikuwa anamiriki gari la kifahari sana,Jeep kipindi hicho,Mond ajatoka.
Marioo,Na wengine wanaofata wakisikiliza kwa makini watafika alipo Mond na kumzidi,ipo siku Entertainment industry itatoa ajira nyingi kuriko hata serikali.
Kongole mkuu kwa mchango wako ambao ni productive
 
Huyu huyu Dayamondi, aliyekuwa anagongea modo za Bob junior mpaka akaanza kujiita Rais wa masharobaro
Brand ya mentor wake,akaona isiwe noma ajiite Wasafi.

Licha ya juhudi zake,hao unaosema hawajamtoa, mbona yeye mwenyewe huwa anawapa credit !?
Muanzisha uzi ni Dayamondi?

Au shabiki anamsemea?
 
Huyu huyu Dayamondi,aliyekuwa anagongea modo za Bob junior mpaka akaanza kujiita Rais wa masharobaro
Brand ya mentor wake,akaona isiwe noma ajiite Wasafi.

Licha ya juhudi zake,hao unaosema hawajamtoa,mbona yeye mwenyewe huwa anawapa credit !?
Muanzisha uzi ni Dayamondi?
Au shabiki anamsemea?
Hiyo ni kawaida kwa kila mtafutaji mwenye malengo na anayejitambua na kujua nn anachokitaka....

Watu kibao tu mtaani huku walianza kama vibarua kwa watu mpaka wakafanikiwa kuwa na biashara zao tena zaidi ya mabosi zao... Lakini pia kuna watu kibao tu ambao wanafanya vibarua kwa haohao mabosi tena zaidi ya wale waloweza kujiajiri wenyewe na bado wanamaisha ya kuunga

Ni kufocus tu kwny mipango yako na wale unaokutana nao kwenye njia zako wasikupe kikwazo bali wawe km steping stones
 
Diamond watu walio mtoa ni Papa Misifa yy alimshika mkono baada ya kuambiwa na THT hajui kuimba, akamuamini na akawekeza hela yake na mtu pili aliye mpika na kumtengeneza Diamond ni Bob Junior mpaka akawa mwimbaji japokuwa waligombana ila sasa hivi wako poa.

Wengine waliokuja baada ya hao ni walitaka kufanya nae biashara baada ya kuijua potential ya Diamond kwenye biashara ya muziki so Bob Junior na Papa Misifa ndio walio mto kimziki.
 
mpaka mama yake mzazi hajamsaidia kitu?

Jinga wewe
Unadhani kama ww binafsi huna malengo kwa kile unachokifanya wazazi wako wanaweza kukufikisha? Wangapi wanasaidiwa kila kitu na wazazi wao lakin wapowapo tu?

Elewa tu kuwa hakuna atakayeweza kukutoa ww kama we mwenyewe huna malengo ya wapi unataka kufikia

Kwa mond, mama yake na wengine wote alokutana nao kwenye safari yake ya muziki ndo hizo koneksheni nilizozisema... Na yeyote aliyempa kikwazo alitemana naye!

Hakuna sehemu utakayoenda kupiga mishe zako za kutafuta maisha afu usikutane na watu... Na kufanikiwa katikati yao itakubidi uwe na maono ya kipekee ya kile unachotaka kukifanya na akili ya kuwatumia haohao watu km ngazi.

Hakuna mtu anayeweza kumtoa mwenzake kama huyo mwenzake hajaamua kutoka
 
mond mwenyewe akikusoma hapa anakushangaa.

mjini bila mkono pagumu sana,unamjua misifa na bob junior??
unajua kwamba alikwenda kwa bob junior anarap,akaambiwa awekeze nguvu katika kuimba zaidi???

hakuna anayekataa kwamba diamond ni mfano mzuri kwa watafutaji,ila ni upuuzi kusema hakuwahi kusaidiwa kufika alipo.
 
Ungekuwa unauwezo wa kusoma huku unafikiria nnekwambia urudie kusoma nlichoandika... Kwa bahati mbaya thinking capacity yako iko chini mno
 
Ungekuwa unauwezo wa kusoma huku unafikiria nnekwambia urudie kusoma nlichoandika... Kwa bahati mbaya thinking capacity yako iko chini mno

sasa kama uwezo wa kuwasilisha hoja ni duni!!!

si kila mtu anaweza kuandika akaeleweka,yafaa wengine mkabaki kuhesabu viatu vya mond na cheni hapo wcb.
 
Back
Top Bottom