Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,493
Miezi kadhaa huko nyuma niliandika makala isemayo "viongozi wasiokosea, na Taifa la wasiokasirika". Nilipoandika nilionesha mifano kadhaa ya jinsi gani viongozi wameboronga na hakuna aliyekubali makosa. Nilitumaini basi labda pole pole tunajifunza. Nikasema kuwa wananchi wasipoonesha kukasirishwa na vitendo vya watawala wao basi watawala huweza kufanya watakalo.
Sakata la Richmond ni ushahidi mwingine wa viongozi "wasiokosea". Nasikitika karibu mwezi sasa hakuna kiongozi hata mmoja aliyekubali kuwa amefanya makosa kuhusu Richmond. HAKUNA. Wote wanalaumu mtu mwingine na kukwepa kuwajibika na hata wale waliowajibika kwa kujiuzulu hawakukubali makosa yoyote yale.
Je nani alikosea? Naona baada ya watu kuisoma ripoti hii tunaweza kuwasaidia kuwaonesha ni nani alikosea.
a. Rais Jakaya Kikwete alikosea wapi au hakukusoea?
b. Waziri Mkuu Lowassa alikosea wapi au hakukusoea?
c. Waziri Ibrahim Msabaha alikosea wapi au hakukusea?
d. Waziri Nazir Karamagi alikosea wapi au hakukusoea?
e. Mkurugenzi wa TIC alikosea wapi au hakukusoea?
f. Usalama wa Taifa walikosea au hawakukosea?
g. Mwanasheria Mkuu alikosea au hakukosea?
h. BRELA walikosea wapi au wahakukosea?
Au inawezekana kabisa kuwa mkataba wa Richmond uliingiwa na baadaye kugundulika mapungufu yake na utapeli wake na hakuna mtu aliyekosea? Inawezekana kuwa ni kweli wote hawa wamesingiziwa na Kamati ya Mwakyembe na wameonewa tu.? Ni kwanini ni vigumu kukubali makosa na kuomba radhi? Je Kikwete atakuwa kiongozi wa kwanza kuomba msamaha Watanzania kwa makosa yake yeye mwenyewe au na yeye ataomba radhi kwa makosa ya "waliochini yake".? Au Rais naye huwa hakosei?
I don't know nimechanganyikiwa!!! hivi viongozi huwa wanakosea nisije kuwa nimeanza na wrong assumptions..