Hakuna aliye salama kwa utawala huu

Huyu anaejiita Sijui Nyani Ngabu ni hovyo kama walivyowachumia tumbo kama Jerry tu hamna kingine. Kwani wanaposema hakuna aliesalama wanaongelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za nchi au wanaongelea yanaondelea katika kuteka, kutesa na hata kutoa roho kwa wapinzani? Hizi akili fupi siku zote ni shida na janga la kitaifa
Nyani Ngabu is mentally sick!
 
Ni muda sasa nimekuwa nikisikia watu wakitoa ilani kuwa hakuna aliye salama kwa utawala huu [wa Magufuli].

Kwamba, hata kwa wale ambao ni CCM au wanaohusiana na CCM nao hawako salama. Yaani wakikosea au wakifanya jambo ambalo ni kinyume huo uCCM wao hautowasaidia. Na kwa mtaji huo nao wataonja joto ya jiwe kama ilivyo kwa wengine ambao hawahusiani na CCM.

Sasa mimi nimekuwa najiuliza....hivyo si ndivyo inavyopaswa kuwa!?

Kwamba, hapendwi mtu. Hakuna cha u-chama wala nini. Wewe ukiharibu utashughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila upendeleo wowote ule.

Yaani sioni lolote lililo baya hapo kwani hata ingekuwa ni mimi ningefanya vivyo hivyo.

Sasa napoona baadhi ya hawa makamanda wakiwaonya watu wanaowadhani labda ni CCM kuwa eti hakuna aliye salama chini ya utawala huu, nabaki nakuna kichwa na kuwaza mengi.

Ina maana kwa mfano hawa makamanda wakija kushika dola watakuwa na upendeleo wa makusudi kwa makamanda wenzao wanaoharibu? Watafumbia macho madudu ya makamanda wenzao au?

Kwangu mimi, suala la kwamba hakuna aliye salama chini ya utawala huu ni jambo zuri, ili mradi tu haki itendeke. Atayeharibu na ashughulikiwe bila kuangalia yeye ni wa itikadi gani, chama kipi, kabila lake, dini, jinsia, hali ya kiuchumi, na kadhalika.

Siku zote hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa na si vinginevyo.
Hivi wakati unaandika huu utumbo ulipata taarifa kuhusu RC na DC kujihusisha na Rushwa? na kama uliipata au kuisikia je unafahamu kuwa leo ni siku ya 4 na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yao? Tukisema kuna mungu watu hawawezi kuchukuliwa hatua yoyote tutakuwa tunakosea? (Rejea uvamizi wa clouds, vyeti feki vya bashite). Nyani ngabu hebu acha kujitoa ufahamu kwa kuandika mambo ya kipuuzi; kama haya niliyoyataja hayajafanywa na wahusika kanusha ili nikupe orodha nyingine
 
Mkuu, Kama kawaida mambo mengi yanapelekwa kwa mkumbo. Kuna tabia ya waathilika kutaka kuungwa mkono na wengi, hata wasiojua nini kinatokea. Hapa tulipo, Shujaa anapatikana kwa kampeni badala ya matendo yao.

Nyuma ilikuwa enzi ya watu maarufu. watu hawa ni Malaya, wezi, wahuni. Ni aibu kwamba kazi ilimaanisha uhuni au usanii kwa lugha ya sasa. Kila mtu akawa msanii. Bajeti ya chai ikawa ni sehemu kubwa na matumizi ya serikali. Watu wakaanzisha biashara ili kuiba pesa ya serikali. Hawa ndo wanaongoza maneno ya laana na kushawishi wengine kwamba woote tutaumia. Wapi?
Umeongea point sana.Asante
 
Chadema sasa hivi akili zao wote wamekabidhi kwa Mange Kimambi
 
Hakuna aliye salama si kwa mantiki hiyo kwamba kunatakiwa kuwe na upendeleo kwa wana CCM. Bali hakuna aliye salama kwa kanuni zinazotumika hivi sasa kushughulikia matatizo tuliyo nayo.

Hakuna aliye salama hata ndani ya CCM kwani hicho chama hivi sana hata wao hawana kinga ya kufukuzwa bila ya kufuata taratibu wala katiba ya chama hicho. Huku nje hakuna aliye salama kwani kila anayempinga Magufuli anaoonekana msaliti na anatakiwa ashughulikiwe.

Wanavyogandamizwa wapinzani hivi sasa utafika muda na CCM nao watagandamizwa!
Una lilia kinga ndani ya vyama huku ukitaka rais aondolewe kinga?

Hizo kinga ndio zinampa kiburi hata Mbowe pale chadema yeye ndio mfalme hakuna wa kumgusa!
 
Wanachofanya makamanda ni KUHUBIRI chuki tu hakuna jipya.kila neno atakaloongea jpm lazima litazamishwe katika MTAZAMO hasi.yani anaweza akaongea maneno mengi na ya kueleweka lkn wakatoka na kaneno kamoja na kuanza kukanyumbulisha. Mfano ni hili wanalosema magufuli alisema watanzania wataishi kama mashetani. Ukiwaambia wathibitishe hawawez hata kidogo na hata ukifuatilia Ile clip inaeleweka vizur sana.Ni vitu vingi sana wanapotosha watu.Mtu akivunja sheria hataki aende peke yake anaanza kutafuta sympathy,anatafuta wa kumuunga mkono kwa kudivert hoja ya mcng. UTASIKIA HAKUNA ALIYESALAMA.
 
Chadema sasa hivi akili zao wote wamekabidhi kwa Mange Kimambi
kuna mada hapa imeletwa na mbulula mwenzako sasa jikite kwenye hoja tunazoleta usitoke nje ya hili maana mmelianzisha wenyewe
 
kuna mada hapa imeletwa na mbulula mwenzako sasa jikite kwenye hoja tunazoleta usitoke nje ya hili maana mmelianzisha wenyewe
Mkuu,, ona aibu sasa hivi chama kinamtegemea mange awapigie propaganda
 
Mwisho wa siku kitatokea kikosi kisichojulikana kikamiliki mageshi yote na kututawala kimafia.
 
Ingekua anahukumu kwa usawa tungesema sawa! Lakn kwa huu upendeleo wa mchana kweupe hakuna usawa. Tunachosema hakuna aliye salama hatumaanishi wanaokosea kwa mujibu wa taratibu za nchi yetu. Hawako salama tu wanaopinga JPM. Wewe ukimuunga mkono JPM hata uwe hambaz utapeta. Pr Mruma et alikua TISS. Et na bashite naye usalama. So hawa kufanya makosa ruksa!! Hatuko sirious wa TZ
 
Yawezekana mleta maada ni mmoja wa watu wasiojulikana.Watanzania wanahofu sana na watu wasiojulikana kwa vitu vifuatavyo

-Utekaji,kuteswa,kutishiwa kuuwawa hadharini na hata kupigwa risasi.
Halafu bado mtu anajitoa ufaham na kujiona eti bado yupo salama.Hiyo ni akili ya Kibashite tu na sio vinginevyo.

Watanzania hatupo salama na nchi haipo salama.
 
Mkuu, Kama kawaida mambo mengi yanapelekwa kwa mkumbo. Kuna tabia ya waathilika kutaka kuungwa mkono na wengi, hata wasiojua nini kinatokea. Hapa tulipo, Shujaa anapatikana kwa kampeni badala ya matendo yao.

Nyuma ilikuwa enzi ya watu maarufu. watu hawa ni Malaya, wezi, wahuni. Ni aibu kwamba kazi ilimaanisha uhuni au usanii kwa lugha ya sasa. Kila mtu akawa msanii. Bajeti ya chai ikawa ni sehemu kubwa na matumizi ya serikali. Watu wakaanzisha biashara ili kuiba pesa ya serikali. Hawa ndo wanaongoza maneno ya laana na kushawishi wengine kwamba woote tutaumia. Wapi?
Shida Ni pale zile pesa za chai maofisini kugeuka malipo ya biashara haramu ya binadamu..najiuliza kama ajira inatoka kwa kuangalia itikadi ya mtu basi tunatengeneza taifa la hovyo kabisa
 
Sasa naona unatokwa na povu kama unajiandaa kuingia kitengo cha propaganda wewe bado sana Nenda kasome ndipo uje uendelee maana sijaona hoja ya msingi hapo
 
Mkuu wengine tatizo letu ni CCM, CCM ndio laana kuu ya nchi hii. Huu mzimu unaoitwa CCM siku uking'oka ndio maendeleo yatapatikana Tanzania..
 
Back
Top Bottom