Hakimu, Mawakili wa Serikali waibana Mahakama ili iwafutie baadhi ya mashtaka

graceirene

Member
May 26, 2011
25
4
WATU watano akiwemo hakimu mkazi na wanasheria wawili wa serikali wanaokabiliwa na mashitaka 11 ya utakatishaji fedha haramu, kujihusisha na rushwa na kuongoza mtandao wa kupanga uhalifu wameiomba mahakama iwafutie baadhi ya mashitaka hayo kwani upelelezi umeshindwa kukamilika kwa wakati kisheria.

Aidha waliiomba mahakama imuunge mkono Rais John Magufuli kwa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa kwenye gereza la Butimba mkoani Mwanza alipotaka upelelezi ufanyike haraka ili watu wapungue magerezani.

Waliwasilisha maombi hayo Agosti mosi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Niku Mwakatobe kupitia mawakili wao Elibariki Maeda , Valentine Nyalu na Fridolin Bwemelo.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 34/2019 ambapo wakili wa serikali, Janeth Sekule
alieleza mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa kwenye shauri hilo ni pamoja na Nelson Kangelo, Mwanasheria na wakili wa shirika la hifadhi za Taifa, (TANAPA), Maneno Mbunda, hakimu Mkazi Bernad Nganga, mwanasheria wa serikali, Fortunatus Muhalila na Tumaini Mdee.

Mawakili wa washitakiwa hao waliwasilisha maombi sita wakiiomba mahakama ifute makosa yote yanayowakabili wateja wao ambayo upelelezi unatakiwa kukamilika ndani ya siku 60 na libaki kosa la kughushi ambalo halina ukomo wa upelelezi.

Walidai kuwa notisi ya serikali namba296/2012 inawaelekeza waendesha mashitaka wasifungue kesi kama upelelezi haujakamilika pamoja na maelekezo ya Mkurugenzi wa mashitaka ya Novemba 3, 2008 ambayo kwenye kipengele cha nne inataka mamlaka husika kumwajibisha mwendesha mashitaka au mpelelezi ambaye kwa hila atasababisha haki kutotendeka.

"Vilevile maelekezo haya ya DPP yameelekeza ofisi zake kutokufungua kesi kama upelelezi haujakamilika isipokuwa kwa makosa makubwa kama ya mauaji, unyang'anyi wa kutumia silaha na uhaini. Kitendo cha polisi kufungua kesi hii bila upelelezi kukamilika ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu na kiashirio cha kusababisha haki kutotendeka", alisema wakili Bwemelo kwa niaba ya mawakili wenzake na kuongeza.

"Upande wa mashitaka uelekezwe kuanza kusikiliza kesi yao kama upelelezi bado upande wa mashitaka waiondoe kesi hiyo mahakamani kwani waliifungua kinyume cha notisi ya serikali hivyo mahakama iondoe kesi hiyo na washauriwe kuifungua tena upelelezi ukikamilika,"

Mawakili hao waliendelea kueleza kuwa washitakiwa watatu ni watumishi wa serikali jambo alilodai kuwa wanazidi kuitia hasara serikali kwani wanaendelea kulipwa mishahara huku hawafanyi kazi na wanatunzwa na serikali gerezani hivyo kama upelelezi haujakamilika ni vema shauri hilo likaondolewa mahakamani ili kuiepusha serikali kuendelea kupata hasara.

WATUMIA MAELEKEZO YA RAIS GEREZA LA BUTIMBA

Walidai kuwa wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza (Mei 6, mwaka huu) wakili wa serikali alisema upelelezi uko ukingoni jambo walilohoji iweje mpaka sasa zaidi ya miezi miwili upelelezi haujakamilika jambo walilosema hiyo inakwenda kinyume na maelekezo ya Rais, John Magufuli aliyoyatoa alipotembelea gereza la Butimba mkoani Mwanza.

“Rais alisema upelelezi ufanyike haraka ili watu wapungue magerezani.Hivyo tunaiomba mahakama imuunge mkono mheshimiwa Rais kwani amesema hataki kuongoza nchi ya watu wanaonung’unika na wanaolia machozi," wakili Bwemelo.

Aidha waliomba endapo wakili wa serikali aliyepo mahakamani hapo jana majibu ya hoja zao basi apewe siku saba za kuleta majibu mahakamani hapo.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka Agosti 7, mwaka huu ambapo upande wa Jamhuri watatakiwa kuleta majibu ili mahakama iweze kufanya uamuzi.

Awali Mei 6, mwaka huu mwanasheria wa serikali, Javelin Rugaihuruza aliwasomea mashitaka matatu washitakiwa wa kwanza, Kangelo na wa tano, Mdee ambapo wanadaiwa kuongoza mtandao wa kupanga uhalifu kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.
 
Maamuzi hayo yatasaidia kwa Kesi zingine.Msingi wao wa Kisheria ni Mzuri sana kama siasa hazita tawala Maamuzi ya Hakimu
 
Bado yuko sahihi unamkamataje mtuhumiwa wakati upelelezi haujakamilika halafu kila siku unadai upelelezi haujakamilika huku mtu anasota lupango...
Hakimu analia lia baada ya yeye kupewa shitaka la uhujumu uchumi,akili imemkaa sasa.
 
Mbwa kala mbwa mtuhumiwa mwanasheria mlalamikaji mwanasheria Hakimu mwanasheria.Haaaaaa
 
Bado yuko sahihi unamkamataje mtuhumiwa wakati upelelezi haujakamilika halafu kila siku unadai upelelezi haujakamilika huku mtu anasota lupango...
Ndio yuko sahihi lkn ni baada ya kujionea mahabusu hua kuna hali gani ndo ameelewa sasa.
 
Back
Top Bottom