Hakimu kizimbani kwa madai ya kutaka kumtoa mfungwa gerezani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
18,124
2,000
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya imemfikisha mahakamani hakimu mkazi wa mahakama ya Mwanzo Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Harrison Makinda kwa tuhuma za kufanya udanganyifu ili kumtoa mfungwa gerezani.

Akizungumza leo Jumamosi Desemba 5, 2020 mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Julieth Matechi amesema hakimu huyo anakabiliwa na kesi namba 272/2020 ya kutoa taarifa za uongo za mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha sheria 122 na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.

Matechi amesema katika shtaka la kwanza Makinda anadaiwa Mei 16, 2019 aliwasilisha nyaraka yenye maelezo ya uongo kwa ofisa wa gereza la Rujewa wilayani Mbarali akimtaarifu kwamba mshitakiwa (jina limehifadhiwa) aliyetiwa hatiani na kutumikia kifungo cha miaka mitano jela anatakiwa kutolewa gerezani.

Amesema kuwa hakimu huyo alidai mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh100,000 na fidia ya Sh600,000 ili atoke gerezani wakati akijua wazi kuwa si kweli na kwamba hukumu aliyoandikiwa mshtakiwa haikuwa na adhabu ya faini hiyo.

Hakimu huyo alikana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Januari 20 ,2021.

©Mwananchi
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,533
2,000
Unathema?

1506565753.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom