Hakimu amuagiza Gavana Waititu 'Baba Yao' asitie mguu wake kwenye ofisi zake za Gatuzi la Kiambu, kwa muda wote wa kesi ya ufisadi dhidi yake

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
https://www.nation.co.ke/news/Kiamb...d-from-office/1056-5215838-15s680a/index.html Gavana wa Gatuzi la Kiambu Ferdinand Waititu, almaarufu kama Baba Yao, ambaye alitoweka baada ya kusikia kwamba anasakwa kwa tuhuma za ufisadi leo hii amefikishwa mbele ya hakimu kwa 'bail hearing'. Wakili wake walipata afueni baada ya hakimu Lawrence Mugambi kukubali kumpa bail(15million) ila wakapigwa na butwaa baada ya kusikia masharti ya hakimu. Hakimu amemuagiza gavana Waititu, na afisa wengine wa serikali ya gatuzi la Kiambu, kutofika kwenye ofisi zao. Akisema hatua hiyo itahakikisha kwamba kesi yenyewe itabaki kuwa ya uwazi na ya heshima inayostahili. Hukumu hii ilikuwa kiendelezo cha hukumu ya hakimu mwingine, kwenye kesi nyingine tofauti. Hakimu Mumbi Ngugi ambaye alizua gumzo hivi majuzi baada ya kutoa hukumu ambayo itawasimamisha kazi kwa muda viongozi kama magavana ambao ni watuhumiwa kwenye kesi za ufisadi.
 
Uibe pesa nyingi kiasi hicho halafu uishie kuhangaika na mkeo mnatupwa jela.
 
Gatuzi la kiambu ni jamii gani ya kobe hiyo
Tafsiri yake kwa kiingereza ni Kiambu County. County=Gatuzi, Kiambu ni gatuzi ambalo lipo maeneo ya Ml. Kenya na linapakana na jiji la Nairobi. Kobe ni wewe.
 
Uibe pesa nyingi kiasi hicho halafu uishie kuhangaika na mkeo mnatupwa jela.
Kama alitafuna hizo hela ni stress za kujitakia. Kumbuka pasipoti za watuhumiwa wote zimechukuliwa na vitengo vya usalama. Wameonywa pia kuhusu kuingilia au kujaribu kuvuruga kesi ambayo ipo mbele ya mahakama na kwamba mashahidi wapo chini ya ulizi wa mahakama. Naibu gavana wa Kiambu nyoro ameshatangaza kwamba amechukua usukani kwa maagizo ya mahakama. Stress baada ya stress zinamuandama 'Baba Yao'. Acha iwe funzo kwa wenzake.
 
Cc. MwendaOmo, mention ya kesi ni Agosti 26. Ulibisha sana kuhusu uhalisia wa kesi hii dhidi ya gavana Waititu. So far so good DPP Haji na team yake hawakuwaachia wakili wa mtuhumiwa mwanya wa kujipenyeza, na kumnasua.
 
Back
Top Bottom