Supermind
JF-Expert Member
- Apr 22, 2018
- 259
- 243
Habarini wanajamvi.
Nimekuwa nikitafakari siku nyingi juu ya uwepo wa Mungu. Lakini majibu bado ni utata mkubwa na kujazwa imani kila kukicha.
Watu weusi ndio kizazi pekee chenye imani ya dhati juu ya huyu Mungu asieonekana ambae tusadiki ndie Mungu wa kweli. Lakini cha kushangaza sijui tunakwama wapi. Tumekuwa tukizama kwenye maombi juu ya vitu vingi lakini matokeo ni sisimizi (yaani kidogo sana au hamna kabisa).
Ila wenye imani huzidi kukutia moyo na kukwambia maombi yatajibiwa tu sio lazima wee ujue. Au watakwambia yalishajibiwa ila wee huna jicho la kiroho pengine hukujua. Kwa kweli ni mafumbo mengi na imani tuu na kudhania dhania ndiko kumetawala. Kimsingi nimechunguza binafsi imani hii, mtu maskini wala haimsaidii kiviile, sana naona ndo wanazidi kuwa maskini tu, sjui kwa nini.
Wenzetu WACHINA tumekuwa nao sawa kimaendeleo na kiuchumi mwanzoni mwa vita vya pili vya dunia. Hawa watu inasadikika hawana imani wala dini yeyote nchini mwao. Muasisi wa Taifa lao bwana Mao Tse dong inasemekana alipiga marufuku dini zote wakati wa ujenzi wa ujamaa wa china. Nchi ilipiga hatua kwa kasi ya ajabu hadi leo ni tishio duniani kiuchumi na maendeleo.
Maswali magumu ya kujiuliza, kwa hawa wachina;
1. Ni nani anawabariki wakati hawaamini katika Mungu na wala hawasali.?
2. Mbona kila siku wanafanya maendeleo makubwa wakati hata misikiti na makanisa hawana.?
3. Mbona sisi Waafrika tunamwamini Mungu wa Mbinguni na tunasali sana lakini hatupati baraka kama za wachina?
4. Waafrika tunakosea wapi hasa.? Au tunakosea namna ya kuabudu na kuendesha hizi dini.?
Wachina wameendelea kuishangaza dunia.
*Wameweza kujenga hospitali/ karantini kubwa duniani ya wagonjwa wa corona kwa wiki moja tu.
*Wameweza ku-wipe out/kuifutilia mbali corona kwa mda wa mwezi mmoja tu
*Wachina wanazidi kuwa tishio kiuchumi na kimaendeleo duniani kote kila kukicha.
Je, ni nani hasa Mentor wao? Kwanini hawa watu wanaodaiwa kukosa imani ya Mungu tumuabuduye sisi wanazidi kuchanja mbuga kwa kila kitu, ili hali sisi tuaminie tunazidi kuwa masikini?
Kwa maoni yangu kuna haja ya kufanya research juu ya huyu Mungu wa uchina awasaidiae ili kama vip nasi tu-adapt/tuige. Maana si kwa kufanikiwa huko.
Sijataka kuzama sana kwa undani kuhusu uchina kuepuka kuwachosha wasomaji na wachangiaji. Ila kimsingi wachina wanavitu ni hatari.
Karibuni wanajamvi tujadili kwa ajili ya kubadili mind set na kupanuana kifikra.
Sent using Jamii Forums mobile app