Hakika Tundu Lissu amewachoma sindano ikagusa mshipa

SOKON 1

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,134
331
Wangekuwepo kina Tundu Lissu kama kumi nadhani viongozi wa serikali wasingekuwa wanakurupuka kufanya maamuzi yenye kuliletea taifa hasara wangekuwa wanaomba ushauri wa kisheria kabla ya kufanya jambo lolote kuliepusha taifa na hasara za kizembe!

Mh Tundu Lissu nikupe shukrani kwa kuwa mzalendo kuweka wazi mali za taifa letu imeshikiliwa Canada kwa sababu ya maamuzi mabaya ya kiongozi ila wao walitaka wafanye kwa siri na walipe kwa siri bila wananchi kujua hakika uko walipo waliotuletea hasara kwa maamuzi yao mabaya na ya kukurupuka pasipo kuomba ushauri watakuwa wanasikilizia maumivu ya sindano baada ya kuwaingia barabara!
 
Wakuu,
Tundu Lissu ni mpinzani, na wajibu wa wapinzani katika siasa ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani.
Alichofanya ni kufichua kilichokuwa kimefichwa na serikali kuhusu kuchelewa kwa ndege iliyonunuliwa kwa pesa za walipa kodi. Sasa msemaji wa serikali anamshutumu Tindu Lissu kwa kutokuwa mzalendo. Uzalendo gani zaidi ya kufichua madudu kama hayo?
Wajibu wa serikali kwa wananchi ni kutoa majibu yanayoeleweka na sio kulaumu watu waliotoa taarifa kwa wananchi. Kwa kweli wapinzani wametimiza wajibu wao kwa wananchi, na ninyi serikali ni vyema mtimize wajibu wenu kwa wananchi waliowapa mamlaka.
 
Kwa sasa nipo huku Singida nafatilia asili ya Mzee Lissu kuwa alitokea Arusha,Mbeya au Mara kwani watu wa kariba yake huwa hawatokei Singida
Te teh. Sasa katokea huko. Hata wayahudi waliuliza liza alipotoka Yesu na kujiuliza km kuliwahi toka Nabii. Bahati mbaya hawakujua aliyetoka ni zaidi ya nabii.Na hivyo vipimo vyao havikuwa sahihi.
 
Wangekuwepo kina Tundu Lisu kama kumi nadhani viongozi wa serikali wasingekuwa wanakurupuka kufanya maamuzi yenye kuliletea taifa hasara wangekuwa wanaomba ushauri wa kisheria kabla ya kufanya jambo lolote kuliepusha taifa na hasara za kizembe!
Mh Tundu Lisu nikupe shukarani kwa kuwa mzalendo kuweka wazi mali za taifa letu imeshikiliwa Canada kwa sababu ya maamuzi mabaya ya kiongozi ila wao walitaka wafanye kwa siri na walipe kwa siri bila wananchi kujuwa hakika uko walipo waliotuletea hasara kwa maamuzi yao mabaya na ya kukurupuka pasipo kuomba ushauri watakuwa wanasikilizia maumivu ya sindano baada ya kuwaingia barabara!

Kuna watu ni wabeba box wazuri sana Marekani, na walikuwa tayari kwa mabadiliko, lakini tangu mtu wa nyumbani aingie basi na mawazo yote yamebadirika, kutwa wako bize kumtetea mtu wa nyumbani hata kama kuna mshemsho
 
Alichofanya Lissu ni sawa na kuwafuma mke/mme ugoni readyhanded....hahahaa yaani aibu tupu, wanatapatapa

Wasimame wakae kazi ipo Lumumba ikulu hailaliki tena mpaka mwezi uishe
Wangekuwepo kina Tundu Lisu kama kumi nadhani viongozi wa serikali wasingekuwa wanakurupuka kufanya maamuzi yenye kuliletea taifa hasara wangekuwa wanaomba ushauri wa kisheria kabla ya kufanya jambo lolote kuliepusha taifa na hasara za kizembe!
Mh Tundu Lisu nikupe shukarani kwa kuwa mzalendo kuweka wazi mali za taifa letu imeshikiliwa Canada kwa sababu ya maamuzi mabaya ya kiongozi ila wao walitaka wafanye kwa siri na walipe kwa siri bila wananchi kujuwa hakika uko walipo waliotuletea hasara kwa maamuzi yao mabaya na ya kukurupuka pasipo kuomba ushauri watakuwa wanasikilizia maumivu ya sindano baada ya kuwaingia barabara!
 
Wakuu,
Tundu Lissu ni mpinzani, na wajibu wa wapinzani katika siasa ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani.
Alichofanya ni kufichua kilichokuwa kimefichwa na serikali kuhusu kuchelewa kwa ndege iliyonunuliwa kwa pesa za walipa kodi. Sasa msemaji wa serikali anamshutumu Tindu Lissu kwa kutokuwa mzalendo. Uzalendo gani zaidi ya kufichua madudu kama hayo?
Wajibu wa serikali kwa wananchi ni kutoa majibu yanayoeleweka na sio kulaumu watu waliotoa taarifa kwa wananchi. Kwa kweli wapinzani wametimiza wajibu wao kwa wananchi, na ninyi serikali ni vyema mtimize wajibu wenu kwa wananchi waliowapa mamlaka.
Tatizo wanalipwa mishahara isiyo na utoaji jasho wala upeo wa kufikiria kwani wangesema tunadaiwa kuna tatizo gani badala yake wanamshupalia Tundu lisu
 
Back
Top Bottom