The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Mimi sio mtu wa kufuata mkumbo hua nafuata akili yangu zaidi. Kama mwanzoni akili yangu haijamkubali mtu basi haijamkubali ila bado haina maana kua sitamkubali huyo mtu siku zote kama kuna kitu atafanya ambacho kitasababisha nimkubali basi nitafuata akili yangu. Mimi siku zote huegemea kwenye ukweli, I am very weak for the truth, truth always attracts my attention, popote penye ukweli basi hua naelekea huko.
Ukweli umenivuta baada ya tathmini ya muda mrefu kuwa Rais Magufuli kweli anaipenda hii nchi.
Magufuli anaonekana anaipenda hii nchi kwa moyo wake wote, anatamani kuona masikini wa hii nchi wanafaidika na rasilimali za nchi yao. Juzi hapa nilikua na ziara yangu binafsi mikoa ya Geita ana Kagera kuzunguka wilaya karibu zote, ukiona maisha ya wananchi wa mikoa hiyo walivyo chini ya dimbwi la umasikini alafu unaona watu wanakula pesa zao bila huruma kama kweli uko reasonable huwezi kiruhusu hilo.
Umasikini hii nchi bado kabisa umeota mizizi, bila kua na mtu mwenye nia ya dhati kwenye kupambana na rushwa basi tatizo litazidi kua kubwa.
Mwalimu mkubwa wa dini ya Kikristo Bwana Yesu Kristo wa Nazareti aliwahi kusema siku zote utamani kuunua ukweli na ukweli siku zote utakuweka huru.