Hakika sasa naanza kuamini Rais Magufuli anaipenda Tanzania na kuuchukia umasikini

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,061
2,000
Mimi sio mtu wa kufuata mkumbo hua nafuata akili yangu zaidi. Kama mwanzoni akili yangu haijamkubali mtu basi haijamkubali ila bado haina maana kua sitamkubali huyo mtu siku zote kama kuna kitu atafanya ambacho kitasababisha nimkubali basi nitafuata akili yangu. Mimi siku zote huegemea kwenye ukweli, I am very weak for the truth, truth always attracts my attention, popote penye ukweli basi hua naelekea huko.

Ukweli umenivuta baada ya tathmini ya muda mrefu kuwa Rais Magufuli kweli anaipenda hii nchi.

Magufuli anaonekana anaipenda hii nchi kwa moyo wake wote, anatamani kuona masikini wa hii nchi wanafaidika na rasilimali za nchi yao. Juzi hapa nilikua na ziara yangu binafsi mikoa ya Geita ana Kagera kuzunguka wilaya karibu zote, ukiona maisha ya wananchi wa mikoa hiyo walivyo chini ya dimbwi la umasikini alafu unaona watu wanakula pesa zao bila huruma kama kweli uko reasonable huwezi kiruhusu hilo.

Umasikini hii nchi bado kabisa umeota mizizi, bila kua na mtu mwenye nia ya dhati kwenye kupambana na rushwa basi tatizo litazidi kua kubwa.

Mwalimu mkubwa wa dini ya Kikristo Bwana Yesu Kristo wa Nazareti aliwahi kusema siku zote utamani kuunua ukweli na ukweli siku zote utakuweka huru.
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,818
2,000
JPM anatukumbusha ukiwa kiongozi wa ngazi yoyote ujue kaziyako kuzitafuta changamoto na kuzitatua, usimtegemee aliye chiniyako akuainishie changamoto zilizopo.

wengine ni wavivu na wewe kiongozi ndie utakae wajibishwa. Sasa kama Rais wako anahangaika kutatua kero za wananchi wewe kiongozi wa chini yake unapata wapi usingizi kwa nchi iliyojaa changamoto kama hii. Tuta mlaumu JPM kwakua bado hatujui namna ya kufanyanae kazi.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,707
2,000
Mleta mada ni lini uliamini tofauti na hivyo?
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Hivi unawezaje kuuchukia umaskini wakati huo huo unawachukia matajiri?
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,061
2,000
Mleta mada ni lini uliamini tofauti na hivyo?
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Hivi unawezaje kuuchukia umaskini wakati huo huo unawachukia matajiri?
Nikajua unakuja na ushahidi kumbe unabwabwaja tu. Lakini pia nimekwambia kua akili yaku inamove kuelekea ukweli ulipo.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,376
2,000
Mkuu hao masikini huenda pia umechangiwa na gharama za maisha yake. Umewahi kuona msafara wake, ni kiasi gani hutumika? Umeona magari yanayotumiwa na serikali? Je huoni ile ni sehemu ya umasikini wa hao watu?
 

Coco

JF-Expert Member
May 13, 2019
430
1,000
Watanzania wenye uelwa mpana/uwezo wa kufikiri ni wachache sana!
Nadhani tuwe na IQ test kabla ya kupewa Access ku-post/coment chochote JF.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,120
2,000
Insue Pekee Ninayoweza Kumsifia Magufuli Ni Kwenye Insue Ya Ujenzi Hasa Mabalabala Toka Akiwa Waziri Wa Ujenzi Na Sasa Rais!

Ila Linapokuja Swala La Uchumi, Usalama Na Fredom Kwa Watu Anaowaongoza Kwakweli Kafeli Pakubwa"
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,190
2,000
Ikiwa akili zako zipo kama za Jingalao hautusumbui maana tunajua mapungufu yenu
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,061
2,000
Ikiwa akili zako zipo kama za Jingalao hautusumbui maana tunajua mapungufu yenu
Vijana humu ndani kwenye jukwaa hili hamtaki mawazo binafsi, sijakukataza kuandika unavyoona wewe, haya ni maoni yangu. Tatizo unataka maoni yangu yafanane na ya kwako jambo ambalo haliwezekani.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,190
2,000
Hapana hapa jukwaani tunaheshimu mawazo ya kila mtu.
Vijana humu ndani kwenye jukwaa hili hamtaki mawazo binafsi, sijakukataza kuandika unavyoona wewe, haya ni maoni yangu. Tatizo unataka maoni yangu yafanane na ya kwako jambo ambalo haliwezekani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom