Hakika Polisi pekee hawawezi kuchunguza suala la Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakika Polisi pekee hawawezi kuchunguza suala la Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Wakati Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeunda kamati ya kufanya uchunguzi wa suala la kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, makundi mbalimbali katika jamii yameibuka na kueleza kutokuridhishwa kwao na polisi pekee kufanya kazi hiyo.

  Makundi hayo yanajenga hoja mbalimbali zinazolenga uhalali wa kutaka kuweko na tume huru ya kufanya kazi hiyo kwa sababu hadi sasa hisia ambazo zimetanda juu ya mateso yaliyomkuta Dk. Ulimboka, ni kwamba inawezekana serikali ikawa na mkono wake katika hilo.

  Tunajua na tumesikia serikali kupitia kwa viongozi wakuu, kwanza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na baadaye Waziri Mkuu kwamba serikali haina mkono katika suala hilo, lakini pia tumeshuhudia maoni ya watu mbalimbali wakiwamo madaktari wenyewe ambao ndiyo chimbuko la kadhia hii, kila upande ukionyesha kuwa kuna nguvu kutoka mahali fulani ya utekelezaji wa uhalifu huu.

  Kwa kifupi, katika suala la kutekwa, kupigwa na kuumizwa mno kwa Dk. Ulimboka ambaye kwa sasa amelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), akitibiwa chini ya uangalizi maalum, ni vigumu sana watu kuaminiana hata kama wataapa kwa miungu yao kama uchunguzi huru utakaohusisha makundi mbalimbali katika jamii hautafanyika.

  Kwa bahati mbaya, anayenyooshewa kidole katika kadhia hii ya kuudhi, kukasirisha na kwa kweli kuamsha hasira ya umma, ni serikali. Serikali inanyooshewa kidole kwa sababu za wazi kabisa, ndiyo ilikuwa katika mvutano na madaktari na Dk. Ulimboka ndiye alikuwa kiongozi wa madaktari hao.

  Hili ni suala nyeti, tata na ambalo limekuwa vigumu kueleweka kwa maelezo ya kawaida ama ya vyombo vya usalama kama polisi na hata vya wasemaji wengine wa serikali; hisia za wananchi kwa ujumla wake zimekuwa kali mno. Ni kali kuliko inavyoweza kuelezwa.

  Kwa maana hiyo inahitaji kutazamwa kwa njia ya kipekee ili kwanza kujenga imani kuwa haki itapatikana katika jambo hilo.

  Tunajua taifa hili pia lina historia yake, kwamba siyo mara ya kwanza kuundwa kwa tume huru kufanya uchunguzi wa jambo ambalo limetatiza jamii na kwa kweli ambalo linaiweka serikali katika muonekano wa kuwa mtuhumiwa wa hilo lililotendeka; katika mazingira kama hayo serikali au vyombo au chombo chake kimojawapo kujiteua tu haraka haraka kufanya uchunguzi, kwa kweli haiwaletei wananchi amani na kwa hali hiyo matokeo ya uchunguzi wake yanakuwa tayari yamekwisha kupingwa hata kabla ya uchunguzi wenyewe kuanza kufanywa.

  Ni vema ikaeleweka mapema kuwa taifa hili sasa limepiga hatua kubwa sana, kwanza kutambua na kuheshimu haki za binadamu, kuna vyomvyo ambavyo serikali imeviunda vya kulinda haki hizo, kuna sheria na katiba katika kulinda haki hizo pia, lakini zaidi sana makundi mbalimbali ya kijamii yamejipa wajibu wa kuwa waangalizi wa haki za binadamu; kila kundi katika wadau wote hawa linakubalika na kutambulika katika jamii.

  Itakuwa ni makosa makubwa kwa serikali kujiaminisha kwamba inaweza tu kupuuza makundi mengine yenye dhima ya kutetea haki za binadamu na kujifanyia mambo kama itakavyo.

  Ni kwa kutambua ukweli huu na kwa kweli tukijua fika kwamba serikali yoyote ambayo imeingia madarakani kwa njia ya sanduku la kura, inawajibika kusikiliza na kuzifanyia kazi hisia za wananchi wake, kwa kuwa wao ndiyo chimbuko la madaraka ya serikali, iunde tume huru. Hata hivyo, inawezekana ikapuuza, lakini ni uhakika pia kuwa gharama yake nayo ni kubwa baada ya kitambo kidogo.

  Ndiyo maana nasi tunasisitiza kuishauri serikali kuwa isikilize vilio na hisia hizi juu ya janga lililomkuta Dk. Ulimboka; iunde tume huru ambayo itajumuisha watu wenye uadilifu usiotiwa shaka ili ripoti itakayopatikana ikubaliwe na umma juu janga lililomkuta Dk. Ulimboka.

  Ni vema serikali ikashughulika na janga lililomkuta Dk. Ulimboka kwa kutambua wazi kwamba inashughulikia kadhia nzima ya mgomo wa madaktari, kwa hiyo ni lazima ifanye bidii ili kwanza kuokoa maisha ya wananchi wake kwa kuwashawishi madaktari warejee kazini, lakini la umuhimu zaidi ionyeshe kwa vitendo halisi inafanyia kazi changamoto hizi zilizombele yake kwa uhuru na uwazi ambavyo vitaisafisha dhidi ya tuhuma hizi.


  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Tume yoyote ile itakayoundwa na liserikali la CCM mimi sina imani nayo. Hao CCM wanahusika moja kwa moja na hilo tendo la kinyama halafu wao wao ndiyo waje waunde tume halafu hiyo tume iwe tume huru? Bullshit!!

  They can take their tume and shove it where the sun don't shine.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kesi ya nyani kapelekewa Tumbili... tutgemee nini?
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  ‘Kipigo kililenga kumnyamazisha Ulimboka'

  Pamela Chilongola,Issa Lazaro (SJMC)
  CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema tukio la kutekwa nyara na baadaye kujeruhiwa kwa Dk Steven Ulimboka, linalenga katika kuwanyamazisha wanyonge wanaodai haki zao.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano.

  Katika tukio hilo watu wasiojulikana, walimteka nyara kiongozi huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, akiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni na baadaye kupelekwa katika Msitu wa Pande ambako alipigwa na kujeruhiwa vibaya.

  Tukio hilo limekuja wakati madaktari katika hospitali mbalimbali za Serikali, wakiwa katika mgomo usiokuwa na kikomo, wakishinikiza kulipwa maslahi bora.

  Akizungumzia tukio hilo, Mukoba, alisema kitendo cha kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa daktari huyo, si tu kwamba ni cha kuwanyamazisha wadai haki, lakini pia kimeidhalilisha Tanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiheshimu katika kuheshimu haki za binadamu.

  "CWT inalaani sana kitendo cha kumwagiza bure kwa damu ya Dk Ulimboka, Msitu wa Pande unatumika kutesa na kuulia watu wasiokuwa na hatia, msitu huo unapaswa kuwa kielelezo na alama ya Watanzania wanaoamka kupambana na dhuluma inayotekelezwa na idadi ndogo ya watu dhidi ya umma wa Watanzania,"alisema Mukoba

  Mukoba alisema CWT inahamasisha misingi ya kutetea haki za jamii na wafanyakazi ambazo zimekuwa zikimomonyoka.

  Wakati huo huo, baadhi ya wananchi katika Jiji la Dar es Salaam, wamesema tukio hilo lililenga katika kumyamazisha Dk Ulimboka, katika jitihada zake za kudai haki wa madaktari.
  .
  Wakizungumza kwa nyakati na mahali tofauti jana, wananchi hao walisema lengo la watu waliofanya unyama huyo ni kudhoofisha nguvu za Dk Ulimboka, ili asiendelee kudai haki.
  Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Furaha Alex, alisema kitendo hicho kimedhihirisha kuwa madaktari hapa nchini hawathaminiwi hapa wanapodai haki zao za msingi.

  "Kitendo cha kupigwa kwa Dk Ulimboka, kimewadhalilisha sana madaktari hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa anawawakilisha wenzake. Hili ni jambo la kusikitisha saba," alisema Alex.

  ?Kipigo kililenga kumnyamazisha Ulimboka?
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Pinda: Tukio la Ulimboka lina utata[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda , amesema tukio la kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Stephen Ulimboka, lina utata na kuongeza kuwa uchunguzi utakaofanywa na vyombo vya usalama ndio utakao maliza utata huo.

  Pinda aliyasema hayo jana bungeni alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

  "Mazingira ya tukio hili bado yana utata mwingi, yanahitaji uchunguzi wa kina, kila mtu anasema lake, mwingine hili na wengine wanasema Serikali ndiyo imehusika," alisema na kuongeza:

  "Mimi nasema kama ni Serikali basi tutakuwa ni watu wa ajabu sana, Serikali tufanye ili iweje."
  Pia Pinda alisema kuwa, Serikali imefanya juhudi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanaweza kuokoa maisha ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutumia hospitali za Lugalo pamoja na matawi yake, kutumia madaktari waliostaafu na wengine walio wizarani.

  "Tumezungumza na wenzetu wa Lugalo ili wananchi waweze kutibiwa katika hospitali hiyo na matawi mengine," alisema Pinda.

  Baada ya maelezo hayo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Tundu Lisu, alimuuliza Pinda kwa nini asiwajibike katika suala la mgomo wa madaktari kwani ni yeye amekuwa akilishughulikia kwa muda na halionekani kupata ufumbuzi.

  Baada ya swali hilo, Pinda alisema kuwa, yapo mazingira yanayoweza kumlazimu kuwajibika lakini siyo, haya ya mgomo wa madaktari kwani amejaribu kwa kiasi kikubwa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
  "Yapo mazingira yanayoweza kunifanya nijiuzulu, lakini hili la madaktari nimejaribu kwa uwezo wangu, lakini be what it is (kwa jinsi lilivyo), kuna changamoto nyingi katika suala hili," alisema Pinda.

  Baada ya majibu hayo, Lisu alipewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na kusema "If you have tried your very best and you failed, why don't you resign?" (kama umejaribu kufanya kila linalowezekana ukashindwa, kwa nini usijiuzulu??)

  Baada ya swali hilo, Spika Anne Makinda alimtaka Waziri Mkuu kutojibu swali hilo la nyongeza kwa maelezo kuwa, linafanana na swali la msingi.

  Hata baada ya maelezo ya Spika, Waziri Mkuu alijibu kwa kumueleza Lisu kuwa, anamuheshimu sana lakini lugha aliyotumia katika kuuliza swali lake siyo nzuri.

  Mbunge Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Martha Mlata, aliyesema kuna uvumi kuwa, kuna watu wanawapa baadhi ya madaktari fedha ili wahamasishe wenzao kugoma.

  Alisema kuwa, lengo la kikundi hicho ambacho hakukitaja, ni nchi isitawalike.
  Akijibu swali hilo, Pinda alisema na wao (Serikali) wamesikia uvumi huo na wameviagiza vyombo vya usalama vilifanyie uchunguzi.
  Pinda: Tukio la Ulimboka lina utata
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Wasomi walaani kupigwa Ulimboka
  BAADHI ya wasomi nchini wamelaani kitendo cha kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Stephen Ulimboka, wakisema kuwa kimechukua sura ya usalama wa taifa badala ya mgogoro wa madaktari.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema suala hili sasa limevuka hatua ya mgogoro wa madaktari na limechukua sura ya usalama wa nchi.

  Alisema mahali ambapo suala hili limefikia wananchi wanataka kuona hatua zinachukuliwa na siyo masuala ya kuambiwa kuwa mihimili inaingiliana.

  "Jana (juzi) Waziri Mkuu alisema atatoa tamko la Serikali leo (jana), akisema liwalo na liwe, huku watu wakisubiri tamko hilo, Bunge linasema haliwezi kufanya hivyo kwa sababu mihimili inaingiliana," anasema na kuongeza:

  "Wanasema hivyo huku watu wanakufa, watu hawajui wala kutaka kusikia mambo ya mihimili, sijui tulibeba kamati kwa ndege, wanataka kupata majibu ya hali hii kutoka kwa Serikali."

  Mhadhiri huyo alisema kuwa, watu wengi akiwamo yeye mwenyewe anaogopa hata kutoka ndani kwani, kama siyo Serikali iliyohusika, basi hata kikundi hicho hakijulikani kina orodha ya watu wangapi wanaotakiwa kufanyiwa unyama huo.
  Alisema kuwa, mgogoro huu umeanza tangu Desemba mwaka jana ambapo madaktari wa mafunzo kwa vitendo waligoma wakidai fedha za chakula na vifaa vya kufanyia kazi, lakini mpaka sasa Serikali imeshindwa kupata ufumbuzi.

  "Wanasema udaktari ni wito, nani anaweza kufanya kazi akiwa na njaa, kwa nini wao Wabunge wasijitolee kwenda bungeni bila kulipwa posho, waache kutuambia mambo ya separation of power '(mgawanyo wa madaraka); watu wanakufa hospitali, wanataka majibu ya Serikali," alisema Bashiru.
  Alisema kuwa kuwa, lugha zinazotolewa sasa hivi juu ya mgomo wa madaktari, ni lugha za viongozi walioshindwa kutawala.

  Kwa upande wake Profesa Abdallah Safari, anasema unyama aliofanyiwa Dk Ulimboka unaonyesha kuwa, sasa Tanzania imefikia katika Siasa za Kimafia.

  "Tumezoea kusikia wanauliwa wanasiasa, lakini kwetu Tanzania tumeanzisha historia mpya ya kutaka kuuwa Professionals (wataalam) kitu ambacho kwa Afrika hakijawahi kutokea," alisema Safari.
  Alisema kuwa, suala hili lisichukuliwe kwa mzaha na kutaka Tume Huru ilichunguzwe kwa kuwa, Serikali inadaiwa kuhusika katika tukio hilo.

  "Polisi hapa wanasema wanalichunguza, lakini wao ndio wanatuhumiwa, hapa hayatapatikana majibu sahihi, ni lazima kuwe na tume huru," alisema Profesa Safari.

  Aidha Dk Benson Bana, aliwataka Watanzania waungane kulaani tukio la kupigwa kwa Dk Ulimboka, kwa kile alichosema siyo utamaduni wa Watanzania.

  "Lakini nawataka madaktari wajiangalie upya, huwezi kudai haki huku watu wakiwa wanakufa, wakae meza moja na Serikali wajadiliane," alisema Dk Bana.Wasomi walaani kupigwa Ulimboka


   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hata mtoto ukimweleza tu jinsi hali ilivyokuwa hakika atakuambia tu ya kwmb ccm wasifanye uchunguzi kuhusu hili la Dr Ulimboka!

  ccm tangu awali tumeshasema ni janga la Taifa letu!
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hata na Gratian Mukoba anapoeleza hofu yake hiyo sawa na hawa wa chuo kikuu wanajua sasa kumekucha Tanzania, maana huenda anayefuata ni Gratian Mukoba zamu yake, kisha kina safari. Maana serikali ya ccm imegundua kwamba wasomi na professionals hawana mwitikio kwa ccm kama zamani, badala ya kuweka dole juu wanainamisha dole chini. Ukiulizwa unafanya kazi gani wewe sema ni mkulima wa Ng'wagitolyo. Hapo utakuwa salama. Mwalimu, daktari,....unajitakia kuhasiwa, kungolewa meno na makucha bila ganzi na kutukosesha wajukuu bure. Hayo ndio maendeleo ya Tanzania ya JK.
   
 9. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  hela za kukodi madaktari wa nje kwa mabilioni ya pesa zipo kama ilivyoandika Tanzania daima la leo (200bilion kukodi madaktari),lakini za kuwalipa madai yao na kununua vifaa vya hospital hakuna,Hivi ni nani aliyetuloga,kwenye sehemu za madili ya matumizi ya mabilioni na kukodi hela hupatikana Tanzania bana!
   
 10. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  wananchi hawana imani na tume inayoongozwa na watuhumiwa.

  1:kiongozi wa tume ACP Msangi ametajwa kwamba anahusika kwenye tukio lenyewe.
  2:Kova alidanganya ASP Mokiri alikuwa katika upelelezi wakati Dk.Ulimboka anafikishwa Muhimbili ilihali ASP Mokiri alikuwa anachunguza kama Dk.Ulimboka alikuwa bado hai na ndo madaktari walipogundua alichokuwa akikifanya walimpa kichapo.
  4: Pinda alisema "liwalo na liwe"
  5: polisi walipata habari za kutekwa kwa Dk.Ulimboka mapema lakini hawakuchukua hatua zozote.
   
Loading...