Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 416
- 462
Hakika nimekuwa najiuliza maranyingi kuhusu Nani Waziri Mkuu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimekuwa nafuatilia shughuli mahususi wanazozifanya mawaziri wakuu katika pande zote mbili zilizoungana na kubaini kuwa wanawajibika zaidi katika kusimamia shughuli za serikali bungene na wanajibika kwa kiasi kidogo saaana katika Upande wa Zanzibar. Naona Kama kunamipaka ya utendaji wa Waziri Mkuu upande huo nakupelekea kunitafakarisha na kupata majibu ya kwanini Maraisi waliotangulia waliona busara ya kuiweka wizara ya TAMISEMI chini ya Waziri Mkuu kwa kuwa anawajibika zaidi Bara na kukwepa mkanganyiko wa endapo Raisi atatokea Zanzibar Nani atasimamia Tanganyika.
Busara yangu inanituma kwamba TAMISEMI ndio Tanganyika.
Naomba mchango wenu katika ili nami nipate uelewa.
Nimaoni yangu tuu wanabodi.
Busara yangu inanituma kwamba TAMISEMI ndio Tanganyika.
Naomba mchango wenu katika ili nami nipate uelewa.
Nimaoni yangu tuu wanabodi.