Hakika ni dr slaa wa watanzania......

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Jamani naomba kushare kidogo nilichokikuta jana huko UKONGA.Nilikuta watu kama 40 ambao walikuwa wanafanya kazi ya kupiga tofali, hakika nilishangaa walivyokuwa wakijadili mambo ya siasa.Hakika kila mtu alikuwa amekata tamaa ya maisha kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu sasa hivi.Watu wote walieleza umuhimu wa kufanya marekebisho ya Katiba haraka iwezekanavyo ili Rais atakayechaguliwa atokane na wananchi.WALISEMA WAZIWAZI KAMA DR WILBROD SLAA HATAGOMBEA URAIS 2015 BASI HAWATAPIGA KURA KWANI NDIYE KIONGOZI PEKEE ANAYEFAA KUONGOZA NCHI HII...Nilivutiwa sana na mazungumzo yao lakini muda ulinitupa mkono nikaondoka.Nikajiuliza Slaa ana nini mbona kila kona anaungwa mkono??
 
Ukipita mtaani ukasikiliza watu wanavyo jadili huwezi kuamini kama kweli SISI M ilishinda kila mtu anakandia SISI M tena wengine wanaenda mbali wanatamani kama uchaguzi mwingine ungefanyika baada ya miaka 2 tu. Kuhusu katiba mpya ndo usiseme kila mtu anaitaka. Hata wengine hawakuwahi kuona ya zamani sababu ya uzembe wa watawala...lakini bado pamoja na kutoiona wanataka mpya!
 
Chema chajiuza, linganisha Karatu ya Dr Slaa akiwa mbunge na Chalinze ya Kikwete akiwa mbunge
 
slaa bado ni nyota na tegemeo la watanzania!

na ndio maana tulimchagua..tena kwa asilimia 64 %.

mimi bado nimamwamini, ninamuhitaji!

nadhani inataka tujifunze vurugu kidoogo ili tuweze kuokoa nafsi zetu...

inatia huruma tu kuwa naibu wake ni ndumila kuwili....

watoto wangu wadogo nimewafundisha kusema "raisi wetu ni slaa. kikwete kaiba kura"!!! - it is so amazing the way they clearly come out with it!
 
Mimi naona bado wwatanzania tuko nyuma sana kifikra na kimaamuzi,utakuta mtu huyo huyo anayelalamika sasa lakini wakati wa kampeni na kupiga kura alikuwa ni mstari wa mbele katika kupigania serikali iliyopo madarakani iendelee kuwepo kwa kudhani mambo yatabadilika.
Katiba inayodaiwa na watanzania sasa ni watanzania wanagapi wanaijua katiba yenyewe?Hivi wale ndugu zetu waliopo vijijini kabisa unadhani wanajua kuwa nchi hii inaendeshwa kwa katiba?Wanachojua wao ni maisha yanaendelea kuwa magumu na viongozi pekee ndio wanaotakiwa kuwaletea maendeleo yao.
Tunachotakiwa sasa ni kuwaelimisha wananchi nini maana ya katiba na nini kimo ndani yake kwa kuangalia mapungufu yake kabla ya kuidai hiyo mpya maana huwezi dai kipya wakati cha zamani hukijui.
 
Who is werema to take this country to hell? Ukisema katiba mpya kuna watu wanapata pressure yeye ni mmoja wapo, utasikia wanakwambia wananchi , wananchi gani hao tofauti na waliokwisha kuongea?? Maaskofu wanataka katiba mpya, cwt wanataka katiba mpya, waislamu wanataka katiba mpya, tucta/wafanyakazi wataka katiba mpya, wanazuoni wanataka katiba mpya, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wanataka katiba mpya, jaji samata, jaji warioba, jaji kisanga, jaji manento, jaji bomani,jaji ramadhani wanataka katiba mpya , media wanataka katiba mpya,chadema, cuf, nccr,tlp, udp wote wanataka katiba mpya, yeye ag ni nani hasa kuzuia katiba mpya na kwa malsahi ya nani hasa??? Anaogopa nini kuandikwa katiba mpya????? Je hofu hii inatoka wapi???
 
Mimi nina Rais wangu MOYONI namuheshimu na kufuata maelekezo yake, Halafu kuna Rais anyenitawala kwa sababu ya unyonge wangu, Kibaraka wa mafisadi.
 
Chema chajiuza, linganisha Karatu ya Dr Slaa akiwa mbunge na Chalinze ya Kikwete akiwa mbunge
kAKA MKWERE ZAKE SHUGHULI.......KILA SIKU KUANZIA IJUMAAA NGOMANI MARA WANAENDA KUCHEZWA,MARA POSA YANI SIJUI MAMBO YA MAENDELEO WATAFANYA SAA NGAPI.
 
Najiuliza Kikwete hana uwezo hata wa kuomba aandikiwe miradi wa kuboresha nyumba za mbavu za Mbwa katika kijiji chake ? Siku za msiba uingia ndani kwa majirina kavaa buti za mvua. Kha! Amuige Dr. Slaa (Rais wetu wa MOYONI) kwenye jimbo la Karatu au Mbunge na Waziri Nyarambo wa Singida ambaye amechukua sera za nyumba bora kwa watu wa jimbo lake.
 
Kweli mkuu Fmgiganaji,.nilikuwa Mwz vitoto vidogo kabisa vinaonesha alama ya V,mitaani kote Chadema ni gumzo.Hao Sisiem wallishindaje nafasi ya urais?Chakachua style.
 
Back
Top Bottom