kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,712
Siku chache zilizopita mwanamziki, mwanaharakati na mwanasiasa wa nchini uganda bobi wine alikuwa nchini jamaica kwa ziara ya kimuziki aliyoalikwa na mwanamuziki nguli wa mziki wa reggae duniani Tony Rebel.
Licha ya kuzuru Jamaica kwa ziara ya kimuziki, bobi ametumia ziara hiyo kufanya jambo ambalo ni nadra sana kwa wanamuziki wetu wa Tanzania.
Ameitumia ziara hiyo kukutana na watu mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa jamii ya wajamaica.
Amekutana na waziri mkuu wa jamaica Endrew Michael Holness na kujadiliana naye masuala mbalimbali ya maendeleo, siasa na jamii ambapo waliangazia zaidi vijana na namna wanavyoweza kutumia mziki kuwatoa katika umasikini na wanavyoweza kutumia mziki huo kufikisha ujumbe wa kuikosoa serikali kwa uhuru bila kubugudhiwa na mamlaka.
Pia amekutana na mwanamziki na mwanaharakati wa masuala mbalimbali kijamii Buju Banton ambaye ametoka kifungoni hivi karibuni baada kutumikia jela tangu mwaka 2011.
Pia amekutana na kufanya mazungumzo very positive na Mwanamziki mwingine maarufu wa Jamaica Capleton ambaye nyimbo zake zimejikita zaidi katika kupinga/kukosoa mifumo mbalimbali kandamizi ya kidunia.
hili ni somo kubwa sana kwa Wanamziki wa kitanzania hususani wale wanaopata fursa ya kusafiri nchi mbalimbali katika kazi zao za mziki.
Sijawahi kuona mwanamziki yoyote mkubwa wa kitanzania akifanya mazungumzo na kiongozi yoyote mkubwa wa nchi husika aliyoitembelea.
Sijawahi kuona mwanamziki yoyote mkubwa wa kitanzania akifanya mazungumzo na mfanyabiashara yoyote mkubwa wa nchi husika aliyotembelea ili kuvutia uwekezaji nchini au kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania.
Sijawahi kuona mwanamziki yoyote mkubwa wa kitanzania akiwa katika mazungumzo chanya na Wanasiasa wakubwa wenye ushawishi kwa jamii katika nchi husika aliyotembelea.
Wanamziki wetu wengi wanapomaliza kutumbuiza huko ugenini/ughaibuni, hurudi hotelini kwenda kulala na siku ya pili yake hutembelea maeneo mbalimbali ya Malls au Majengo makubwa kupiga picha na baadaye kupost Instagram.
Yafaa waige mfano wa bobi wine.
sio kwamba alikuwa hana uwezo wa kutembelea maeneo mbalimbali ya kula bata nchini jamaica na ku upload picha instagram, la hasha,uwezo huo anao.
lakini aliamua kufanya jambo lenye faida zaidi kwa jamii.
NB:
Kwa wale ambao hawamfamu mwanamziki Bobi Wine, warejee matukio mbalimbali makubwa ya kisiasa yaliyotokea mwaka jana(2018) nchini Uganda.