Hakika mungu ni mkubwa

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
[h=3]ALIYEDHANIWA AMEKUFA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JUMAMOSI MBEYA MJINI AFUNGA NDOA,[/h]

[h=3][/h]
Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya

<tbody>
</tbody>
Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100 Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo

<tbody>
</tbody>
Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo katika kanisa la agape
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea.

Chanzo :http://kapingaz.blogspot.com/2012/12/aliyedhaniwa-amekufa-kwenye-ajali.html?spref=fb

<tbody>
</tbody>

<tbody>
</tbody>

 
Duh naona gari imeharibika kiasi cha kutosha, lakini ashukuriwe Mungu wapo walionusurika mauti.
 
hakika huyo ndo mke wake mwema mana angekuwa mwingine angesepa akamwacha jamaa auguze vidonda vyake.
 
Lililofungwa mbinguni na duniani limefungwa, na kinyume chake.
Haikuwa wakati wa huyu jamaa kutangulia kunako haki.
Ndoa hii ibaki kuwa ushahidi chini ya jua, kuwa Mungu ndiye muweza.
Mungu ibariki ndoa hiyo changa.
 
Hizo picha za gari na pikipiki ni katika eneo la ajali/tukio?
 
tatizo binaadamu hujifanya wanamjua sana mungu lakini kumbe huwa kwa unafiki sasa likishatokea tukiolamuujiza wa mungundipo unawaona watu wanakurupuka kama hawajui kama mungu ni muweza.get well soon kaka maana mungu amekukomboa ukiwa kwenye safari zinazomhusu.
 
Kila mja ataondoka kwa wakati wake! Kama wakti bado utaendelea kudunda!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom