Hakika, Mbowe ni 'Chilongola'

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Mwaka 2008, wakati wa mjadala wa Ripoti Richmond Bungeni, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibaha, Dr. Ibrahim Msabaha alijiuzulu pamoja na Waziri Mkuu wa wakati huo, Mzee Edward Ngoyai Lowassa.

Katika mchango wake juu ya Ripoti hiyo na kabla ya kuachia ngazi, Dr. Msabaha alisema, pamoja na mambo mengine, kuwa katika njia ya kuelekea kuwajibika yeye ni Chilongola. Kwa tafsiri yake kutoka lugha yake mama ya kizaramo, Chilongola ni muonyesha na muongoza njia. Ni kusema, Chilongola ni kiongozi.

Dr. Msabaha alikuwa Chilongola kwakuwa alikuwa Waziri wa kwanza kuwajibika kutokana na kadhia ya Richmond. Alikuwa muonyesha njia ili wengine wamfuate. Na ikawa hivyo. Msururu wa viongozi ulifuata kwa kujiuzulu au kuwajibishwa vinginevyo.

Kuhusu kujitoa kwa vyama vya upinzani kwenye Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman A. Mbowe ni Chilongola. Mara baada ya kutangaza kuwa CHADEMA haitashiriki uchaguzi huo, viongozi kadhaa wa vyama vingine vya upinzani walijitokeza na kutangaza kuwa vyama vyao vimejiondoa kwenye uchaguzi. Chilongola Mbowe akapata uungwaji mkono.

Hata enzi ya Bunge la Katiba, Mbowe alikuwa Chilongola kwa kutoka na kususia vikao vya Bunge hilo hadi kupelekea kuundwa kwa 'hayati' UKAWA. Hakika, Mbowe ni Chilongola. He deserves to be a long-term political target!
 
NAPENDEKEZA AWE MWENYEKITI WA MAISHA WA CHAMA MAANA SIONI MWINGINE ANAYEFAA KUWA MWENYEKITI.
No, namkubali Mbowe kwa initiatives alizofanya so far lakini haimpi umungu kwenye nafasi hiyo,kama ataendelea kuwa kwenye nafasi hiyo kwa kuwa wanachama wanamchagua its ok sina shida na hilo.
 
Back
Top Bottom