Hakika Lowassa Alivunja Rekodi Kuingiza Wanafunzi Wengi Sekondari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakika Lowassa Alivunja Rekodi Kuingiza Wanafunzi Wengi Sekondari!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Nov 5, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hatimaye nimepata Takwimu mpya za Elimu kwa mwaka 2009. Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania wanafunzi kuingia Sekondari kwa wingi kama wakati wa kipindi cha Edward Lowassa. Historia itamsuta kwa mengi lakini kwa hilo jamani tumpe hongera yake. Hongera Edward Lowassa!

  Ni kweli kwa ujumla shule za Kata ni za kiwango cha chini hasa ukizingatia kuwa kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa na Walimu wa Vodafasta. Ndio, wanafunzi wa shule hizo wanakaa kwenye ndoo kama walivyopigwa picha kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la leo. Naam ni kweli kabisa kuwa wananchi waliburuzwa sana tu ili wajenga shule za Sekondari.

  Pamoja na hayo yote ni heri mwanafunzi akae chini shuleni kuliko kukaa tu nyumbani. Pia ni heri tushughulikie suala la ubora wa elimu wakati wanafunzi wako tayari mashuleni kulikuwa kulishughulikia wakati wanazagaa mitaani. Pasipo na mori wa Kilowassa na Kisokoine hatutaweza kuendeleza sekta hii ambayo ndio msingi mkuu wa kuwatokomeza wale maadui wanne wa maendeleo: Umaskini, Ujinga, Maradhi na Ufisadi (Hilo la nne sijaliongeza mimi, aliliongeza Mwalimu Nyerere mwenyewe kwenye Hotuba zake za miaka hiyo - kama mnataka rejea nitawatumia hivi punde!)
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Hongera mchapakazi Lowasa! Ni integrity tu ndo inaleta shaka kwenye fikra za watu hata uliyoyafanya inakuwa ngumu kuyatumia kukuimarisha zaidi
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu zuri 1 haliwezi kufuta mbaya 500, au zuri moja la shilingi 500 haliwezi kufuta moja baya la shilingi 500,000. by the way tunawachagua viongozi ili wafanye mazuri, tunategemea mazuri kutoka kwao kama wanatudisappoint kwa mabaya lazima tulalamike lakini si lazima kuwasifu kwa tunayotaka wafanye.

  Mkuu remember we are not a communist country, kuwa na chagua la kukaa chini shuleni na kukaa nyumbani. Inatakiwa watoto wasikae nyumbani na shuleni wakae kwenye viti. Hilo linawezekana kabisa, ukiuza mashangingi matano wanayotembelea mawaziri yanaweza kuondoka tatizo la viti kwa watoto wa mkioa hata minne.

  Baba hastahili sifa kwa kumnunulia mtoto wake maziwa, lakini anastahili lawama kama mwanae akinywa maji machafu.
  I stand to be challenged.
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hivi hakuna dawa ya hilo ili tuweze kutumia mori wake kuleta maendeleo kwa kasi ya ndege ya uchumi unaopaa? Hatuwezi kumbatiza kama walivyombatiza Saulo baada ya kutokewa na Masihi kule kwenye Barabara ya Dameski akaongoka na kuchapa kazi ya Injili kama hana akili nzuri vile? Kwa kweli hizi takwimu zinaonyesha kuwa alifanya maajabu sana katika sekta ya elimu!
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  What we do define who we are. Kweli huyu bwana atakuwa Paul badala ya Saul. Maana nayo ni process na kama amejichanganya sana na haya matatizo ya moja kwa moja na integrity how could we know he has changed? Kumbatiza sio kwa maji tena..labda in the acid bath
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu uliyoyanena hayapingiki. Ila lazima tujiulize iweje Baba wa Kambo anashindwa, hata maziwa ya mgando hatupi! Takwimu zimeanguka vibaya sana toka tumweke benchi Baba Edo aliyewahi kughani 'Tupo Tumejaa Tele'! Sasa mbona wenzake aliowaacha hawapo tena wala hawajajaa tele?
   
 7. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikuwa Waziri Mkuu, na analipwa mshahara kwa kodi za wananchi, kwa hiyo ni wajibu kufanya hivyo na aliapa kwenye kiapo chake. Hii pesa haikutoka mfukoni mwake.
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ni mpenda Elimu, kwa hili alikuwa sahihi na alifanya kazi kubwa ila kwa yale mengine ni kinyume
   
 9. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  U a right mkuu. Hakufanya fadhila, ni haki yake, tena alipaswa kufanya mengi zaidi ndo mana tunahoji juu ya kuboronga kwake. Ila ni vyema tukatambua mazuri aliyoyafanya tukijua kwamba hayabatilishi mabaya yake.
   
 10. Companero

  Companero Platinum Member

  #10
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kumbuka hata Mtoza Ushuru Zakayo alirudisha mara dufu ya dufu mali alizowadhulumu wananchi wa enzi hizo na Masihi akamwezesha aanze upya mbele ya kadamnasi - Hakika ile ziara ya Lowassa kule kwenye 'Nchi Takatifu' huenda ilimbadilisha na akazaliwa upya kama Saulo wa Taso, tumpe nafasi tena tuone jinsi elimu yetu itakavyopaa na kutuwezesha kufikia malengo ya milenia kabla ya 2015!

  Mchungaji Kishoka u wapi, shusha sala ya ubatizo tuanze upya na Edo wetu!
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  i guess alikuwa na speed kuliko sitta, the problem ni kwamba alipeleka speed yake hata kwenye kuiba. . .
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo alipochakaza mazuri yake
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu tukimpka urai nadhani inawezekana kuwa kuna ukweli enrolments zinaweza kuongezeka, kama issue ni enlorement tu regardless of wanapokaa, na wanowafundisha.

  Lakini be ready for more Richmonds, and be ready for the media itakayokuwa inamtukuza rais kama ilivyokuwa mwanzoni mwa urais wa JK. Is that what you want?
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  companero naona unampigia debe bwana Lowassa teh teh
   
 15. m

  mtangi Member

  #15
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa kuwepo kwa shule ni bora kuliko kuliko watoto kuwa nyumbani. but is there anyone who knows whats goin on kwenye shule za kata?? Acheni sijui tunatengeneza generation ipi?
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwaka 2008 asilimia 56.9 ya waliofanya mtihani wa Kidato cha 4 walipata Divisheni 4!Waliofeli walikuwa asilimia 16.3%! Asilimia 16.8 walipata Divisheni 3!Sasa jiulize ni asilimia ngapi walipata Divisheni 1 na 2!

  Naomba takwimu za elimu Monduli, lazima kuna jambo la kujifunza hapo - heri the lesser evil (uovu mdogo zaidi) jamani!
   
 17. K

  Kitukuu Member

  #17
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Unampigia kampeni nini!!....lol
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,386
  Likes Received: 22,266
  Trophy Points: 280

  lazima tumsafishe na kumfanya ameremete kila kona....
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Definitely Edo kwa performance, yes he can. You agree with him the deliverables he delivers, no doubt about it. All the matters he has handled as Deputy minister, minister were very productive and no one can be blinded not to see. he also did quite a good job while a PM but the Richmond was not handled properly hence all his good work overshadowed. But by the way we should think the otherway round, lets forget about Richmond for the moment as it is a bygone for Edo. Let's see what has been done by the incumbent so far that we TZ would embrace him for? I haven't seen what tangible has he done since he came in?
  I can quickly see the way CCM think more smarter: samaki wa magufuli wametumika kama chanzo cha mapato US$8million per month is a hell of money and I am sure there smell of ufisadi ndani and the money will find away into 2010 elections?????. Kilimo Kwanza slogan 50billion to Patel, another way the money is coming in to the few rulers (2010 elections)????. EPA ya sasa (2009) hivi inayoendelea wanawapigia debe watu wao washinde ili zirudi mlango wa nyuma, wametaget kumpa yule mlipuaji wa EPA ya kwanza aliyekuwa ameachwa nje?????? There are a lot of questions to asks ourselves and the institutions need to give the TZ the answers amicably.
   
 20. Companero

  Companero Platinum Member

  #20
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bado sijaelewa huu uhusiano kati ya Kilimo Kwanza na Jeetu Patel. Nilimuuliza Bubu ataka Kusema ila hakusema. Naomba unisaidie nielewe!
   
Loading...