Hakika leo Ndugai umezungumza kama Spika wa Bunge

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Rais Samia Suluhu Hassan amekamilisha dhima ya uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa,kwa kuwaapisha kwa mujibu wa sheria.

Katika Mambo yaliyojiri na mvuto ni hotuba fupi ya NDUGAI akiwa Kama mheshimiwa Spika anayeongoza mhimili wa bunge,hotuba yake ni moja ya ushereheshaji Kama kumbukizi kwa mhimili wa mahakama juu ya dhana ya utendaji haki.

Dhima ya bunge na mahakama vina shabihiana katika suala la sheria,japo mhimili mmoja unatunga sheria na mwingine unatafsiri sheria.

Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utungaji sheria kandamizi hali inayo iweka mtegoni mhimili wa mahakama katika kutafsiri sheria na kuifanya double standard ionekane kwenye upande wa utafsiri wa sheria.

Katika Mambo makubwa wazee wastaafu waliwahi kumshauri mwendazake ni juu ya serikali kupeleka bungeni miswaada ya sheria kandamizi ambazo ukitazama mantiki ya malengo hayo ni kudhoofisha nguvu ya upande fulani Kama mlengwa mkuu.

Jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammatta alisema sheria yeyote. Kandamizi inayopora na kutweza utu wa mtu maanake ina nyang'anya haki kwa wananchi haipaswi kuwa sheria.

Miongoni mwa Mambo ambayo serikali yetu ilisaini ni mkataba wa amani wa Vienna unao Linda haki za binadamu. Lakini bunge hili la bwana Ndugai limekuwa sehemu ya utungwaji na upasishaji sheria kandamizi zinazo kinzana na ustawi wa wananchi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Mathalani,sheria kandamizi ambazo hata jaji mkuu wa sasa alikwisha zungumzia mara kwa mara ni juu ya kesi na sheria zilizo pitishwa na bunge la NDUGAI kunyang'anya haki ya dhamana kwa watuhumiwa na kuzifanya case fulani kuwa so special, maanake ni kuwalenga watu fulani kwa minajili ya kuwa target na kuwatumbukiza kwenye makosa ya kubambikiwa kwa kuwanyima dhamana na kuwatweza utu wao na kiwafilisi.

Haya yote yamefanyika katika nchi inayo jinasibu kuwa kisiwa cha amani na mbaya zaidi sheria hizo haziakisi matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa wosia wa NDUGAI kwa majaji wateule uwe chachu ya mabadiliko ya kiutendaji kwa bunge analo liongoza na kuacha umwambajifai usio na tija kwa Taifa zaidi ni kulionyesha bunge dhaifu lisilo na weledi na ubunifu wa utungaji sheria.

Ni vizuri maneno na wosia wa viongozi uendane na matendo yake.

Pia nimkumbushe kuwa chombo hicho anacho kisimamia ni chombo cha umma kwa maslahi ya umma, kinyume na hivyo ni kinyume na takwa la katiba juu ya ustawi wa wananchi.

Tukiwa na bunge dhaifu tutegemee serikali dhaifu na taifa dhaifu. Tulinusuru bunge letu kurudisha afya yake itakayowe ubunifu na weledi kwa bunge.

Tanzania ni nchi yetu sote,tubadili tabia kutibu matendo yetu,nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.
 
Bravo...leo hajamtaka Mbowe ama Lissu..kweli fahamu inaanza kumrudia baada ya haya mabadiliko makubwa ya ghafla kwenye ofisi yake!!
 
Akiwa mbele ya Rais huwa anaongea pointi anamuogopa mama alipigwa mkwara waache utoto wao bungeni, ila akirudi bungeni ataendelea na ule utoto wake.
 
Kesho wanawake wa CHADEMA wanazindua kampeni ya mwanamke ni jiko .. nasikia wamemwalika awe mgeni rasmi...maana kaapa kuufagia mfumo dume wote CHADEMA akisaidiana na hao wenzake.
 
Rais Samia Suluhu Hassan (SSH) amekamilisha dhima ya uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa,kwa kuwaapisha kwa mujibu wa sheria...
Umeeleza mambo na maneno meeengi lakini hayaendani na kichwa chako cha habari. Hujasema chochote hicho cha maana alichosema Ndugai.
 
Back
Top Bottom