Hakika Jela Haina Mwenyewe

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kuna watu wametoka Jela wakatoka na mambo makubwa duniani. Hasa kwa Historia uvumbuzi wa vitu vingi muhimu umetoka magerezani.

Waswahili wamesema si busara kukata tawi chini yake wakati wewe mwenyewe umekaa juu yake, wala kunyea kambi au kutukana wakunga na uzazi ungalipo, ni ujinga mkuu.
IPRO inatoa fundisho, kwamba Jela Haina Mwenyewe na kwa akali ya mambo, uchumi mbaya wa dunia, kukosa kazi au upunguzwaji kazi ‘redundancies’ uliopo si ajabu kufika 2010 kila mmoja atapitia gerezani.

Magereza mengi huku Afrika ni sehemu ya kutesa Binadamu au kukomoa wale kimbelembele na si sehemu ya marekebisho au Chuo cha mafunzo hata kidogo.

Umma unamtazamo mbaya wa kumwona Mfungwa kuwa ni adui mbaya sana na hata Idara ya Magereza bado haijakomaza mfumo wake wa marekebisho. Maana kufundishwa kwao kumchunga Mfungwa asitoroke wao humchukulia kuwa adui.






















Tujifunze kutokana na misemo kemkem ya waswahili wasemao;

“Ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji” “Kicheko leo kwangu lakini kesho ni kwako”

Katika tathimini ya misemo hiyo hapo juu fundisho kubwa tupatalo, hata uwe sugu ni kwamba mambo katika dunia huenda kwa mzunguko, hivyo ni vyema kuandaa tuendako kabla hatujafika huko.

Hakika Jela Haina Mwenyewe. Ninayo mengi ya kusema kubaini ukweli hapo juu. Tukio la mwaka 1997 wakati Rais Mstaafu wa kwanza wa Zambia alipowekwa ndani pasipo huruma wala simile na Mheshimiwa Rais Fredrick Chiluba wakati akiwa madarakani. Ni hakika isiyo kanika kwamba Magereza ya Zambia ni miongoni mwa Magereza mabovu katika bara la Afrika.

Rais wa Kwanza Mhe. Keneth Kaunda kwa hofu na kuwakomoa wapinzani aliyakaza sana na kuyafanya magereza hasa yawe mahala pa mateso.

Mfumo wa vyama vingi ukamweka Mhe. Fredrick Chiluba madarakani. Kwa sababu moja au ya pili Chiluba akamwona ndugu Kaunda anastahili kuwekwa ndani na ndivyo alivyofanya. Mhe. Kaunda alikaa wapi?

Palepale alipowaweka wapinzani ili wakione cha mtema kuni ndipo alipoingia yeye.

Yalikuwa ni mateso makali na nakumbuka Mhe. Kaunda akilia machozi kwa uchungu. Ipo katika rekodi kwamba wapenzi wa Kaunda wengi wao walienda kumwona

Hayati Mwalimu J. K. Nyerere akiwa mmojawapo, na ndiye aliyefanikisha kumtoa ndani kwa kumwomba Rais Chiluba. Mhe. Chiluba alikazana akisema mwache akae mahala alipotengeneza yeye mwenyewe

Utawala wa Rais Chiluba ulifika mwisho, naye ingawaje Rafikiye Mwanawasa alipewa kushika usukani, wakati Taifa lilipochachamaa kumtaka Rais Chiluba awekwe ndani ikawa sheria ni msumeno ukatao kuwili.

Rais Chiluba naye akaenda palepale alipomwona Kaunda akilia. Hatujui sasa kwa Mhe. Mwanawasa kutatokea nini?

Lakini jibu la busara ni hili tu kwamba Jela Haina Mwenyewe; Rais wa leo ni Mfungwa wa kesho

Nchini Kenya nako hatuwezi kumsahau Waziri mmoja wa wakati ule akiwa mhusika na Wafungwa na Magereza. Huyu naye alitoa amri kali ya kuondoa magodoro, vitanda ili mfungwa alale kwenye sakafu.

Haikupita muda mkondo wa sheria ukampitia yeye naye akawa mfungwa. Kwa mshangao, alipoingia Jela na kuona vitanda na magodoro ni marufuku akapiga kelele kwa wale mawada kwamba huo ni unyama.

Kwa kicheko cha kebehi wakamkumbusha amri yake akiwa Waziri. Alijisikiaje huyu?

Bado tukiwa nchini Kenya hukohuko, Kamishina mmoja wa Magereza, akatoa amri kwamba mfungwa asinywe uji kwa sukari. Kama ilivyo ada ya dunia, huyu naye akawa
ndani na kushangaa ati ni vipi mtu anywe uji pasipo sukari; ndipo walipomkumbusha amri yake. Huyu naye aliona vipi? Ninayo lukuki ya mifano na vituko vya namna hiyo.

Historia imemtunuku Mhe. Nelson Mandela kuwa mfungwa nambari moja kwa ujasiri, wake wa kukaa Jela ngumu miaka takribani 27 na kutoka humo akiwa na akili timamu na kupewa Urais wa nchi bora Afrika nzima, Afrika ya Kusini.

Mhe. Olusegun Obasanjo pia alikaa gerezani na kutengeneza Chama chake kilichoshinda na kumpa Uraisi wa nchi Tajiri Barani Afrika, Nigeria.

Hatuwezi kumsahau Rais Machachari kwa Wazungu Mhe. Robert Mugabe. Mugabe naye alikaa gerezani, kasoma humo na kupata kuwa Rais wa Zimbabwe hadi kesho. Hata hapo pia ninayo mifano mingi ya kusema kuthibitisha hayo.

Mlolongo huu wote wa maelezo sawia hapo juu lengo langu ni nini? Nataka kukupatia wewe usomaye waraka huu na dunia yote kwa jumla mafundisho makuu mawili;

Moja, ni kwamba tutengeneze magereza yawe nyumba bora za kuishi ili pindi utakapoenda wewe mwenyewe usijute.
 
Uzi huu umekuwepo miaka 10 iliyopita na bado unaakisi uhalisia. Hivi majuzi mbunge wa Arusha mjini aliwekwa rumande kwa miez kadhaa pale Kisongo alipotolewa kwa dhamana akakili kwa ulimi wake mwenyewe, sheria ya wafungwa ipitiwe upya na irekebishwe kwani aliyokutana nayo hayamstahili binadamu. Je asingewekwa humo, angelitambua hilo?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom