Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Nchi ni za wananchi, na miungano pia vilevile.Iwe ni kwa faida au kwa hasara wao ndiyo wenye mamraka ya kuamua kama wawe katika muungano au la.
Leo waingereza wamekataa kuwa katika muungano wa ulaya pamoja na faida zake nyingi.Hakika hili ni funzo kuu la Uhuru wa wananchi jinsi wanavyotaka wajitawale.Tukiachana na Uhuru wao wa maamuzi; jambo hili si dogo, wala hayupo mjuzi wa mambo ya siasa anayeweza kulipuuza hata kidogo.
Kimsingi huu unaweza kuwa ni mwanzo wa mtikisiko mkubwa; utakaoitikisa miungano mingi duniani, hasa ile ambayo watu wake wamekuwa katika harakati za kujitoa.Ombi langu kwa wale viongozi wote wanaotetea miungano wahakikishe wanaiga mfano mzuri kwa viongozi wenzao wa Uingereza katika kuheshimu maamuzi ya walio wengi.