Uchaguzi 2020 Hakika Dkt. Magufuli haamini macho yake. Alifikiri A, imekuwa B!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.

Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.

Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.

Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
 
Me mwenyewe kura yangu kwa lissu....haiwezekani miaka mitano yote hii sijawahi kununua nguo dukani hata jeans moja tu.maisha magumu watoto wa wenye wanasoma tu na hakuna ajira
Kwaiyo Lissu ndio atakununulia Nguo?
Jitume tafuta pesa kwa Akili na jasho lako, Watu wananunua ndinga mpya kila siku wewe unafikiria Lissu atakupa nafuu ya Maisha.
 
Mitano mengine ndio hivi mpaka wapinzani wazuiwe kusikika kwenye magazeti, televisheni, radio na hata online.

Sasa ndio ajitafakari suala la kubadili katiba na kuongeza muhula mwingine hilo haliwezekani. Itakuwa ni kumwagia mafuta kwenye moto mdogo unaowaka.

Chama twawala kiko kwenye 'decline'
 
Kuna vijana wa UVCCM hapa Lumumba wakati fulani huko nyuma walijiapiza mbele ya Magufuli "Kwa makubwa uliyowafanyia Watanzania, kwenye uchaguzi wa 2020 wala huhitaji kupanda jukwaani wala kuzunguka nchi nzima kukampeni..... hiyo kazi tuachie sisi baba!"

Sasa hivi nawaona hapa kiungani Lumumba kila mtu anapambana na hali yake..... maana sumu anazomwaga Lissu kwa wapiga kura zimewaacha kama wahanga wa shoti ya umeme!
 
Ndo binadamu tulivyo, unaweza ukafanya mema 100 ukakosea mambo 2 ukaonekana hufai hata kidogo.

Ki ukweli Dr. Kafanya mambo mengi mazuri ambayo wengi hatukutarajia yatokee katika nchi yetu, lkn kwa sababu hajatoa ajira nyingi na nyongeza ya mishahara basi ndo hafai.

Bila kusahau kaweka mfumo mzuri wa fanya KAZI pata PESA, huu mfumo unawatesa watu wengi waliozoea kula bata, zugazug andikia andiko la uongo na ukweli pata pesa!!

Tuvumilie tuendako kuzuri zaidi tujifinge mkanda baba anajenga nyumba ili tuhame kwenye nyumba ya kupanga uswahilini.
Teh! Teh!
Viva Dr. Viva Dr.!!!

I Will vote him oct 28.!
 
Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.

Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.

Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.

Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
Wasalimie hapo kijiwe Cha phantom,mwambie sisi wafanyakazi tuliopunguzwa pale Buzwagi Gold Mine sababu ya makinikia yake tuna machungu nae kwelikweli.

Hatusahau!
 
Back
Top Bottom