singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WIKI iliyopita, gazeti moja la kila siku lilimkariri Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akilalamikia kampeni inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya kusimamisha na kufukuza watumishi wa umma wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu, wizi, uzembe na njama za kuhujumu mapato.
Katika habari hiyo, nilisoma hadi mwisho nikagundua mambo mawili anayoelezea Mbowe kuhusu kampeni hiyo iliyopewa jina la utumbuaji majipu. Mosi, ni madai kwamba ufukuzaji wa watumishi wa umma unafanywa bila kufuata utaratibu na pili; kama alinukuliwa sawasawa, ni madai kwamba watendaji hao wa serikali ‘wanatumbuliwa’ bila makosa yao kuwekwa hadharani! Mbowe ambaye aliyasema hayo katika ibada maalumu ya uzinduzi wa ukarabati wa Kanisa la Kiinjili la Kiliutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nshara wilayani Hai, aliwataka viongozi wa dini kukemea mwenendo huo.
Katika habari hiyo, Mbowe pia alizungumzia mgogoro wa Zanzibar ambao si maudhui ya makala haya, lakini katika kipengele hicho cha kukemea utumbuaji majipu, kiliniacha nikiwa na maswali mengi. Mbali na maswali niliyojiuliza, nilianza kuthibitisha kile ambacho kimekuwa kikidaiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kwamba hii ya sasa si Chadema ya zama zile. Nitafafanua.
Swali la kwanza nililojiuliza ni kama kweli utumbuaji unafanyika kinyume cha sheria na taratibu kama alivyodai Mbowe. Kwa uelewa wangu ni kwamba wengi wa hawa wanaokumbwa na kampeni hii inayoungwa mkono na Watanzania wengi wakiwemo wanachama wa Chadema, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Rukwa, Zeno Nkoswe, wanasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
Ni kwa mantiki hiyo, baada ya uchunguzi, mwajiri ambaye ni serikali, ataamua, kuwarudisha kazini kama hawana makosa, kuwafukuza kazi au kuwafikisha kortini. Ninachoelewa pia ni kwamba wale wanaofikishwa mahakamani moja kwa moja ni ambao tuhuma zao ziko wazi na ushahidi mwingi upo. Halikadhalika, sijasikia mtendaji yeyote wa sekta ya umma ambaye amesimamishwa, kufukuzwa au kufikishwa mahakamani bila tuhuma zake kuwekwa hadharani.
Nikirudi kwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Rukwa, Nkoswe, aliwahi kukaririwa na gazeti hili akisema: “Serikali hii ya Awamu ya Tano, binafsi nimefurahishwa nayo sana kwa sababu uozo katika sekta ya umma ambao tumekuwa tukiupigia kelele, sio viongozi wa upinzani pekee, bali hata wananchi wa kawaida, sasa tunaona dhahiri ukifanyiwa kazi.”
Akaendelea kusema: “Hakika Rais John Magufuli akifanikiwa vyema, nchi yetu itakuwa ya heshima kubwa duniani na sisi wananchi tutaona manufaa makubwa.” Na huu ndio ukweli dhahiri ambao ninaamini hata Mbowe anao moyoni mwake. Chadema niliyoijua Kabla hata sijasoma habari yenyewe, nilijiuliza maswali mengi sana. Je, Mbowe anayetajwa hapa ni yuleyule Mbowe wa Chadema iliyokuwa inalalamikia sana kukithiri kwa ‘majipu’ huku nyuma hadi siku chache kabla ya nchi kuanza harakati za uchaguzi mkuu mwaka jana?
Kila nilipokuwa nabahatika kushiriki vikao vya Bunge, sehemu kubwa ya michango ya wabunge wa Chadema ilikuwa ni kulalamikia namna nchi yetu inavyoporwa na watu wanaotumia madaraka kwa maslahi binafsi. Ingawa kuna wakati wasemaji wa Chadema walikuwa wakilalamika kwa hisia tu, wakati mwingine walikuwa wakija na hoja zenye mashiko. Chadema ‘ile’ haikuwa inahimiza hatua kuchukuliwa kwa wabadhirifu na mafisadi wa fedha za umma pekee, bali pia ilihimiza uwajibikaji na watendaji katika sekta ya umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Ili kuunga mkono hoja zangu, napenda kutumia maneno ya mwana-Chadema mmoja tu, Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha). Ipo video yake moja unaweza kuisikiliza katika youtube (www.youtube. com/watch?v=8tkj) ambapo Halima ‘anatumbua’ majipu, kinyume kabisa na kauli hizi za Mbowe. Baadhi ya maneno ya Mwenyekiti huyo wa Bawacha alipokuwa anachangia katika moja ya bajeti zilizopita ni haya: “Tokea tumekuja bungeni kwa mara ya kwanza, linapokuja suala la matumizi ya fedha za umma, linapokuja sula la mikataba ni wizi mtupu.”
Katika video hiyo Mdee analalamikia pia hasara iliyosababisha Tanzania kudaiwa dola za Marekani milioni 50, sawa na Sh bilioni 90 zilizotokana na mkataba mbovu wa Shirika la Ndege ATCL baada ya kutumia ndege kwa muda wa miezi sita tu. Anasema fedha hizo ni sawa na bajeti ya maendeleo ya miaka miwili ya wizara ya kilimo, sekta inayoajiri Watanzania wengi.
Lakini kubwa analolilalamikia ni serikali kuongelea hoja hiyo kwa lugha nyepesi bila kuonesha kuwawajibisha walioipa serikali hasara kubwa kama hiyo. Hapo nimechukua mfano wa msemaji mmoja tu wa Chadema ‘ile’ niliyokuwa ninaijua, ambayo takribani wasemaji wake wengi akiwemo Mbowe mwenyewe walikuwa ni kulalamikia tu namna serikali isivyochukua hatua kali, za haraka na madhubuti kwa watumishi wa umma ambao ni wabadhirifu, wezi na wazembe.
Ndio maana napata shida kuamini kama haya ya wakati huo yalikuwa maigizo au nini? Ninavyoamini mimi, baadhi ya hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano sasa ni kufanyia kazi ushauri wa muda mrefu uliokuwa unatolewa na upinzani, hususan Chadema, kuhusu tatizo la ‘majipu’ katika sekta ya umma. Na pengine, hata takwimu walizokuwa wanazitoa au ushahidi wao sasa unafanyiwa kazi.
Kwa mantiki hiyo, wengi tulitazamia kuona chama hicho kinachoongozwa na Mbowe, kikipongeza baadhi ya mambo kama alivyosema Mwenyekiti wake wa Rukwa, Nkoswe. Chadema ilipoamua kumchukua Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za kushiriki ‘dili’ chafu la kuleta kampuni ya kitapeli ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, Edward Lowassa, wengi walitabiri kwamba mwisho wake wa kupambana na maovu katika sekta ya umma umefika kikomo.
Ufuatiliaji wa kampeni za chama hicho wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu nao ulionesha kwamba Chadema ilikuwa imekosa kabisa uwezo (moral authority) wa kuzungumzia ufisadi. Huku kukiwa na madai kwamba sasa chama hicho ndicho kimbilio la wafanyabiashara ambao wana ‘walakini nyingi’ katika biashara zao ikiwemo kukwepa kodi, haya aliyoyasema Mbowe yanazidi kutusadikisha sisi wengine ambao tulitaka tusiamini, kwamba hii ya sasa siyo Chadema ile ya akina Zitto Kabwe, Hayati Chacha Wangwe na Dk Wilbrod Slaa.
Kazi ya upinzani ni kupinga tu? Mimi ninaamini kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inakubali kukosolewa kwani inaongozwa na wanadamu, si malaika. Kama ndivyo wanaweza kufanya makosa. Kwa mantiki hiyo, watu kama Mbowe wana nafasi kubwa ya kuikosoa lakini kwa njia na lugha za kiungwana. Kosa ambalo limekuwa likifanywa na wapinzani siku zote, na hilo kuna siku nitaliandikia makala kwa urefu, ni kutojua namna nzuri ya kumkosoa kiongozi.
Mafundisho ya Dini ya Kiislamu yanasema kwamba kiongozi yeyote wa nchi, haombewi dua mbaya, bali nzuri, ili Mwenyezi Mungu ampe uwezo na moyo wa huruma kwa wananchi wake. Kadhalika, mafundisho yanasema kiongozi wa umma, hata kama ni dhalimu (fisadi), hakosolewi kwa njia ya dharau na kuvunjiwa heshima. Ukitaka kumkosoa kiongozi wa umma, unampa heshima yake kwanza kisha unatafuta mazuri yake na kuyasifia na kisha unazungumzia mambo ambayo unadhani anapaswa kuyafanyia kazi huku ukitumia lugha ya kiungwana.
Tuyaache hayo. Mpaka sasa, watumishi zaidi ya 160 wa sekta ya umma wamesimamishwa kazi au kufukuzwa huku baadhi yao wakifikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na uwajibakaji mbovu, ule uliokuwa ukilalamikiwa na Chadema. Kwa mafundisho hayo ya dini na kwa akili tu ya kawaida, nilitegemea Mbowe angeanza kusifia mazuri yaliyofanywa katika kipindi kifupi sana cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo ni mengi, kama alivyosema Nkoswe.
Kisha, kama yapo ya kukosoa, angeyasema ingawa si hayo ya utumbuaji majipu kwa sababu si kweli alichokisema labda kama ni tukio moja au mawili kati ya majipu mengi yaliyotumbuliwa na yanayoendelea kutumbuliwa. Je, ni kweli, hata hatua ya kutoa elimu bure Mbowe haoni? Kubana matumizi kunakofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kuongeza mapato ya serikali yanayokusanywa na mengine lukuki hayaingii kwenye akili ya Mbowe?