Haki za watoto: Hoja juu ya kutahiri watoto wa kiume

MAGUNJA

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
1,003
545
Haki za binadamu na haki za watoto zinaendelea kupiga hatua mbele. Mahakama ya Cologne nchini Ujerumani imehukumu kuwa kumtahiri mtoto wa kiume ni kukiuka haki za binadamu. Mahakama hiyo inasema mafundisho ya kidini na tamaduni haziwezi kuhalalisha kutahiri watoto.
Baadhi ya hoja za wanaopinga ni hizi hapa:
1. Mtoto ana haki ya kuwa na maamuzi juu ya mwili wake na si wazazi wake.
2. Kumsababishia mtoto maumivu makali bila hiyari yake ambao ni unyanyasaji wa kijinsia.
3. Ngozi inayoondolewa ina maelfu ya mishipa (nerve endings)inayoleta hisia wakati wa kujamiiana hivyo kumpunguzia mtoto hali hiyo atakapokuwa mkubwa.(limited sexual experience)
4. Hoja ya kiafya haina mantiki (Medically not nessessary)
5. Kama ni imani ya kidini mtoto kwa wakati huo haelewi hivyo unatumia imani yako kuweka kovu la maisha kwa mtu mwingine
Wale wanaounga mkono kutahiri watoto wana hoja hizi:
1. Inapunguza maambukizi ya HIV/AIDS
2. Kutekeleza maagano ya kiimani
3. Inafanya eneo husika kuwa safi (clean and hygenic)
4. Inapunguza matamanio ya kujichua n.k.
Ukweli kuhusiana na kutahiri (Facts)
1. Wayahudi wote hutahiriwa siku ya nane tangu kuzaliwa. Na YESU alitahiriwa vivyo hivyo.
2. Waislamu wana utamaduni wa kutahiri japo hakuna muda maalumu.
3. 95% ya wanaume wa Nigeria wametahiriwa.
4. Karibu 9% tu ya wanaume wa Uingereza ndio waliotahiriwa
5. 30% tu ya wanaume wote duniani ndio waliotahiriwa.
WEWE KAMA BABA AU MAMA MTARAJIA MTOTO WA KIUME UNASIMAMA UPANDE UPI?
source: The Guardian (IPP Media)
 
Back
Top Bottom