Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kama ilivyo kwa wabunge wengi ndani ya Bunge ambao wanatokana na chama kinachounda serikali, chama cha mapinduzi CCM, wabunge wanaounda kambi ya upinzani wanastahili heshima kamili kwa haki za msingi. Kwa mfano, wanastahili kuwa na haki ya kuishi, na kwa hiyo, katika shughuli zao za kisiasa, wakingwe dhidi ya vitendo vyovyote ambavyo vitawaondolea hadhi yao na kuwadhuru wao pamoja na mali zao. Kama kunaonekana upo uhitaji wa hilo, Serikali italazimika kuwapatia ulinzi wa kutosha kwa usawa na masharti sawa kama wabunge wanaotokana na chama kinachounda serikali, yaani Chama cha mapinduzi CCM.
Vilevile, Uhuru wa kujieleza, kutoa maoni na kuyasimamia, kupata na kutoa TAARIFA ni muhimu kwa wabunge wote, na zaidi hasa ni muhimu kwa wabunge wanaounda kambi ya upinzani ili kuruhusu kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa ufasaha.
Wawakilishi wa wananchi (wabunge) wa kambi ya Upinzani ni lazima waweze kukemea vikali na kwa uhuru, ndani ya Bunge na nje ya Bunge (Mbele ya Umma) ukiukwaji wa KATIBA, Sheria za nchi, kanuni na taratibu, na vitendo vyote wanavyovibaini kuwa ni kinyume na maslahi ya Umma, hata kwenye majimbo yao ya uwakilishi, na kuchukua hatua kama sehemu ya kutibu na kudhibiti.
Kambi ya upinzani pia wanastahili usawa, na kwa masharti sawa, sawa na wabunge wanaotokana na chama kilichounda serikali, chama cha mapinduzi CCM, kwenye vyombo vya habari vya taifa (Mfano TBC, Daily news, hbari leo, nk) ili wapitishe na kusambaza maoni yao, kuikosoa serikali na matendo yake inapokosea, na kupendekeza njia mbadala ya zile zinazochukuliwa na serikali kama suluhisho.
Wabunge, hasa hasa wanaounda kambi ya upinzani, wanastahili kuyatumia madaraka yao, ili kuweza kufanya kazi na kushirikiana na wabunge wengine wanaotokana na chama kilichounda serikali, yaani chama cha mapinduzi CCM, bila ubaguzi wowote, ikiwa ni pamoja na kuifuatilia serikali kwa kila hatua na kuikosoa popote inapoonekana ipo haja ya kufanya hivyo. Itaendelea...