Haki za raia na wajibu wa vyombo vya dola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki za raia na wajibu wa vyombo vya dola

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Omukuru, Nov 5, 2010.

 1. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ningependa kuwauliza wanasheria, raia anapokamatwa na askari pasipo kufuata taratibu za kisheria, mfano kupigwa, kuhojiwa na kupekuliwa kabla ya kufunguliwa mashitaka, na baadaye ikagundulika kwamba raia hakuwa na hatia ya kusumbuliwa hivyo, askari aliyehusika na usumbufu huu anachukuliwa hatua gani?
   
 2. w

  wikama Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtuhumiwa akikamatwa kitaratibu lazima ahojiwe na kupekuliwa na kama ushahidi upo ashitakiwe mahakamani, kama kesi imepelelezwa na kuonekana hakuna ushahidi anaweza kuachiwa pale pale polisi, akigoma kukamatwa polisi watatumia nguvu ya kadri kuwezesha kukamatwa kwake na anapofanya hivyo anafanyakazi kwa mujibu wa sheria, pindi akipelekwa mahakamani ushahidi ukakosa akaachiwa huru askari polisi hawezi kushitakiwa kwa sababu amefanya kwa mujibu wa sheria ila akikiuka taratibu/sheria anaweza kushitakiwa !
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mean polisi wengi...wanafanya makosa makusudi mtaani hata kukujeruhi kwa kuuliza swali la msingi kama haki ya raia inavyo ruhusu...akijua wazi kabisa..hatakama huna hatia uko mbele yeye hawezi wajibiswa...this is where..mapolisi wanakosa maadili....wasi wangu...kwa kuwa sijui hawajifunzi haki za raia au wanazijua na kuupuzia...au kwa ajiri ya uelewa mdogo....yaani polisi anafanya makusudi hataki kukupa nafasi ya kumweleza..
   
Loading...