Haki ya Utawala bora, Viongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu, madaraka ya Urais, mfumo wa uteuzi wa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi

Jan 22, 2021
12
13
Chachu na kasi kubwa ya maendeleo huendana na mfumo thabiti wa kuitawala katika serikali. Mfumo bora wa kiutawala huleta msisimko kwa watendaji, watumishi na wananchi kujitoa kwa dhati kuleta maendeleo katika taifa letu.

Kwa mtazamo wangu, watanzania tumekuwa na mtazamo kuwa miaka mitano katika awamu mbili za utawala wa urais, ubunge na udiwani tumeiona ni michache na ya kutosha kabisa. Ila tukienda kiundani zaidi, hatupaswi kumpa kiongozi muda mrefu wa kiutawala ili kuleta maendeleo au kukamilisha shughuli fulani za kimaendeleo ambazo alianzisha.

Maendeleo au shughuli za kimaendeleo ni hatua ambazo ni za kimuendelezo unaweza kusema 'progressive process' ambazo hata baada ya kuzikamilisha ni lazima urudi tena kufanya maboresho kadhaa sehemu fulani fulani au katika sekta fulani ambazo uliziendeleza.

Hivyo mtazamo wangu ni kwamba Miaka mitano kwa awamu mbili za utawala na uongozi ni mingi sana kwa uongozi hivyo kuna ulazima wa kuipunguza kati ya miaka mitatu mpaka minne ambayo ni tosha kabisa kwa kiongozi mchaguliwa kuleta au kuanzisha au kuendeleza shughuli za kimaendeleo ambazo alianzisha au amekuta zimeanzishwa na waliomtangulia.

Kusiwe na kisingizio cha kumuweka mtu madarakani kwa muda mrefu kisa tu anakasi ya kimaendeleo au aongezewe muda zaidi tukizani ataongeza kasi ya maendeleo au kutufikisha sehemu fulani. Mimi mtazamo wangu ni kwamba maendeleo au kasi ya maendeleo hutegemea utawala bora, sera bora, mikakati thabiti na 'proper utilization of our precious resources'

Na sio kiongozi kuongezewa muda wa kiutawala au kuwa na muda mrefu wa kiutawala. Ninaamini muda mrefu kiutawala ni uvunjifu wa demokrasia, haki ya kiutawala kwa wale wengine wenye sifa za kutawa.

Mfumo wa teuzi za wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri pia unapaswa kuangaliwa kwa jicho pana/kubwa. Raisi ndie mwenye mamlaka kikatiba ya kuteua wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri. Mtazamo wangu ni kwamba raisi amepewa nguvu kubwa sana kikatiba, zipo sababu za kumpunguzia nguvu hiyo kikatiba na ipelekwe kwa wananchi kufanya chaguzi za viongozi wa ngazi hizo kikatiba.

Tazama hapa, raisi ndie anaeteua katibu kiongozi, makatibu wakuu, mawaziri, waziri mkuu (yaani baraza zima la mawaziri), wakuu wa majeshi (polisi, magereza, uhamiaji, jwtz, jkt nk), wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri, wakuu na wasimamizi wa taasisi mbalimbali za kiserikali nk. Hapa ikumbukwe ninazungumzia raisi kama taasisi na pia ninazungumzia raisi kama mtu aliechaguliwa na wananchi kuongoza taasisi hiyo ya uraisi.

Sababu zangu kimsingi za kupunguza madaraka haya ya kuteua wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ni kwamba, kwa nyakati kadhaa tumeshuhudia viongozi katika nyadhifa hizi wakifanya uongozi wao kisiasa zaidi na wanaonesha dhahiri wakitetea heshima wa wateuaji wao, hivyo kuleta utofauti kati yao na wananchi na watumishi mbalimbali wa serikali. Endapo wananchi wakiwachagua watakuwa na haki ya kikatiba ya kuwaondoa madarakani endapo hawatarizishwa na utendaji kazi wao. Hivyo ipo wazi na kuna kila sababu ya baadhi ya mamalaka ya uteuzi kuondolewa kwenye urais na kupelekwa kwa wananchi wenyewe.
 
Wakati wa uhuru tulikuwa na Meli 6. Baada ya uhuru tuko na meli 14 yaani 6+8.

Tumerudi nyuma miaka 20.Kodi za nchi zinaishia kulipa MaRC, MaDC , DEDs, RAS na Ma DAS.

hivi vyeo ni vingi kuwatunza na kuwalisha hawa hatutakaa tuongeze meli nchini.
 
Back
Top Bottom