Haki ya mtumishi wa umma katika harakati za kisiasa

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
Mimi ni afisa wa serikali. si mjuzi sana wa mambo ya sheria. natatizwa na mikwara ya maafisa wa serikali wa ngazi za juu kupenda kutoa vitisho na kufanya vitendo vya kibaguzi au uonevu kwa mtumishi wa serikali anayejishughulisha na siasa upande wa upinzani. yaani sometime hata unapofanya shughuli zako nje ya muda wa kazi tena bila kutumia rasilimali yoyote ya serikali, unapata vitisho. kinachouma zaidi, utakuta mtumishi mwenzio wa ofisi moja yupo bize kupita kiasi na mambo ya CCM tena ndani ya masaa ya kazi na kwa rasilimali za serikali lakini hafanyiwi chochote.
Shida yangu, naomba msaada kujua Je kuna sheria gani inayomlinda mtumishi anayejipambanua political views zake?
nawasilisha!
 
Back
Top Bottom