Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,130
- 18,737
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu maoni ya Watanzania mbalimbali juu ya taswira ya uongozi wa nchi yetu na suala zima la Katiba ya Tanzania. Jambo ambalo nimefikia mkataa ni moja, kwamba ule usemi wa busara kuwa heri uhuru na umasikini kuliko utumwa na utajiri haukubaliki kwa kila Mtanzania.
Mtu yeyote anaefikiri kwamba Katiba ya Tanzania haina tatizo kwa sasa, ukizingatia ushauri uliotolewa na Nyerere huko nyuma, ni kwamba anaona sio tatizo ikitokea tukawa na raisi asiye na hekima na akaamua kutufanya watumwa ili tuwe Tanzania tajiri. Sasa kuna watu hatukubaliani na hilo na tuko radhi tuwe huru katika Tanzania masikini kuliko kuwa watumwa wa mtu mmoja katika Tanzania tajiri!
Hili ndilo swali la kujiuliza; je ni heri kuwa watumwa wa mtu mmoja katika Tanzania tajiri au watu huru katika Tanzania masikini? Uchaguzi ni wetu, na uchaguzi huu hujionyesha wazi katika yale tunayosema, hasa humu JF.
Tusisahau pia kuwa si vigumu kuwa Watanzania huru katika Tanzania tajiri. Tunahitaji kujitambua tu.