"Haki ya Kuitafuta Furaha" ni Moja ya Siri Kubwa ya Mafanikio ya Marekani

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Moja ya vitu ambavyo Wamarekani walibarikiwa navyo ni kuwa na Waaanzilishi wa Taifa wenye maono makubwa sana.

Walitambua Katiba ni msingi wa nchi. Wakatumia busara ya kipekee sana kuhakikisha kila neno linalotumika kwenye Katiba lina maana nzito sana. Ni busara ya kiMungu iliyopelekea kuandikwa kwa Katiba yao.

Nitagusia maneno haya ambayo kwa juu juu yanaonekana ni mepesi lakini yana uzito mkubwa sana na naamini ni moja ya siri za mafaniko yao. Kuna maneno maarufu sana yanayotoa uhuru na haki kwa Wamarekani. Maneno hayo yanasema:

"We hold these truths to be self-evident, that all men are created equal, that they are endowed by their Creator with certain unalienable Rights, that among these are Life, Liberty and the pursuit of Happiness."

Pursuit of Happiness! Uhuru wa Kutafuta Furaha! Ngoja leo niliongelee hili tu. Tungekuwa wapi kama taifa kama tungekuwa na maono kama hayo? Maneno hayo machache yanagusa na kuathiri kila nyanja ya maisha ya binadamu.

Wanaziita 'unalienable rights' yaani ni haki zisizo na mjadala! Hakuna mtu anaweza kukuletea longolongo kwenye kuzilinda na kuzitetea.

Kuna nchi nyingi ambazo zimeadopt maono kama hayo na haishangazi kwamba ziko mbali sana katika kila nyanja.

Je Taifa la Marekani liko perfect? Ukiwauliza hata wenyewe watakwambia hapana ila hawajawahi kuacha 'kuperfect' Taifa lao na Katiba yao ndiyo KIOO wanachotumia kujiangalia wanapokosea.

Biashara pekee iliyotajwa KWA JINA kulindwa na Katiba ya Marekani ni Vyombo vya Habari. Waliona nini wakaona uzito kwenye hilo? Kwa nini hawakusema viwanda au kilimo au teknolojia?

Tatizo kubwa la Tanzania toka Uhuru ni kwamba tunatunga sheria kwa matakwa binafsi ya wachache. Tumetoka 'kuadhimisha' Muungano ambao umekaa kimazingaombwe. Hakuna anayeuelewa kwa sababu haukuundwa kiroho safi. Hata waliouunda wanauonea haya kwa sababu nafsi zao zinawasuta.

Wote tunajua kuwa ni rahisi sana kuanza tabia mbaya lakini kuiacha huwa ni kazi kweli kweli. Katika maisha yangu binafsi kuna dhambi niliweza kuzishinda baada ya kujifunza kuwa "kwa kuwa tu nina uwezo wa kufanya kitu fulani haimaanishi nikifanye".

"Just because you can do something it doesn't mean that you should".

Leo hii kila siku sheria mpya za HOVYO KABISA zinatungwa na Watawala. Tuko kwenye mbio za kwenda kwenye ukichaa, a race to insanity. Ni kama vile Watawala wanajaribu kutengeneza sheria mbaya zaidi kuliko waliyoitengeneza mara ya mwisho.

Dhambi za asili bado zinatuandama na hazitatuacha salama mpaka tubatizwe upya!
 
Moja ya vitu ambavyo Wamarekani walibarikiwa navyo ni kuwa na Waaanzilishi wa Taifa wenye maono makubwa sana.

Walitambua Katiba ni msingi wa nchi. Wakatumia busara ya kipekee sana kuhakikisha kila neno linalotumika kwenye Katiba lina maana nzito sana. Ni busara ya kiMungu iliyopelekea kuandikwa kwa Katiba yao.

Nitagusia maneno haya ambayo kwa juu juu yanaonekana ni mepesi lakini yana uzito mkubwa sana na naamini ni moja ya siri za mafaniko yao. Kuna maneno maarufu sana yanayotoa uhuru na haki kwa Wamarekani. Maneno hayo yanasema:

"We hold these truths to be self-evident, that all men are created equal, that they are endowed by their Creator with certain unalienable Rights, that among these are Life, Liberty and the pursuit of Happiness."

Pursuit of Happiness! Uhuru wa Kutafuta Furaha! Ngoja leo niliongelee hili tu. Tungekuwa wapi kama taifa kama tungekuwa na maono kama hayo? Maneno hayo machache yanagusa na kuathiri kila nyanja ya maisha ya binadamu.

Wanaziita 'unalienable rights' yaani ni haki zisizo na mjadala! Hakuna mtu anaweza kukuletea longolongo kwenye kuzilinda na kuzitetea.

Kuna nchi nyingi ambazo zimeadopt maono kama hayo na haishangazi kwamba ziko mbali sana katika kila nyanja.

Je Taifa la Marekani liko perfect? Ukiwauliza hata wenyewe watakwambia hapana ila hawajawahi kuacha 'kuperfect' Taifa lao na Katiba yao ndiyo KIOO wanachotumia kujiangalia wanapokosea.

Biashara pekee iliyotajwa KWA JINA kulindwa na Katiba ya Marekani ni Vyombo vya Habari. Waliona nini wakaona uzito kwenye hilo? Kwa nini hawakusema viwanda au kilimo au teknolojia?

Tatizo kubwa la Tanzania toka Uhuru ni kwamba tunatunga sheria kwa matakwa binafsi ya wachache. Tumetoka 'kuadhimisha' Muungano ambao umekaa kimazingaombwe. Hakuna anayeuelewa kwa sababu haukuundwa kiroho safi.

Katika maisha yangu binafsi kuna dhambi niliweza kuzishinda baada ya kujifunza kuwa "kwa kuwa tu nina uwezo wa kufanya kitu fulani haimaanishi nikifanye".

"Just because you can do something it doesn't mean that you should".

Leo hii kila siku sheria mpya za HOVYO KABISA zinatungwa na Watawala. Tuko kwenye mbio za kwenda kwenye ukichaa, a race to insanity. Dhambi za asili bado zinatusakama na hazitatuacha salama mpaka tubatizwe upya!
Well said
 
Back
Top Bottom