Haki ya kufanya mtihani wa kitaifa

heavyload

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
900
497
Naomba msaada wa kisheria kuhusu mtahiniwa mtarajiwa kunyimwa kufanya mtihani wa kitaifa hasa wa kidato cha sita kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi mwezie huku akiwa ameshalipia pesa ya usajili na ameshasajiliwa kuufanya mtihani huo.Je ni sahihi kunyimwa kufanya mtihani afanyeje ili apate haki yake ikiwa amelipa ada kwa miaka miwili tena private school hadi pesa ya usajili?
 
Ni ngumu sana kukushauri maana umeeleza upande wako, shule unaweza kufukuzwa hata imebaki siku moja ufanye mtihani hata kama mtihani huo umelipia.
 
Ukifukuzwa hata siku ya mtihani Kama taratibu zote zimefuatwa Basi utakuwa umepoteza haki ya kufanya mtihani kwa sababu hiyo Ni haki ya bona fide students na wewe wakati huo utakuwa umeishapoteza haki hiyo maan hautakuwa mwanafunzi
 
La msingi fanya mpango ufanye mtihani mwakani. Acheni mambo ya kupenda penda kesi uchwara.
Mtihani wenyewe umeshafafanyika tayari.
 
Back
Top Bottom