Haki Uinua Taifa,Bali Dhuluma na Ukandamizaji Uangamiza Taifa

Eternal_Life

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
812
1,672
Kinachoendelea Arusha dhidi ya mbunge Lema si kitu cha kufurahisha sana kwa Watanzania wapenda haki.Haki ya mtu haiwezi kununuliwa.Se.rikali imeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye kusimamia haki,badala yake ndio inayoongoza kwa kuwatesa na kuwanyanyasa wananchi wake.

Ukweli ndoto inaweza kuwa sababu ya mtu kuhukumiwa kifungo au kunyimwa dhamana ambayo ni haki ya msingi ya kila Mtanzania?Kama siyo chuki,unafiki,roho mbaya na uzandiki uliyo wajaa(wanajijua)Ila Mungu hasinzii wala halali,iko siku ndoto ya Lema itatimia maana kila nafsi itaonja mauti.Hata uwe nani lazima mavumbini urudi.Hata uwe na jeshi la dunia nzima iko siku mauti lazima itakuhusu.

Maadam tuko hai,inatupasa kutenda haki na kusimamia haki.Kwa maana huwezi kuimba wimbo wa "Niombeeni ndugu zangu" wakati maisha yako dhidi ya watu wako ni mfano wa matendo ya shetani kwa watu wa Mungu.Tenda haki nawe utakuwa furaha machoni na kwenye mioyo ya wote.
 
Mimi nadhani viongozi wetu hawajifunzi kutoka sehemu mbali mbali za dunia namna haki zinavyotolewa, huenda wanajifunza jinsi haki zinavyofinyangwa. Na huu mfumo unaongeza umbali uliopo kati ya viongozi na wasio viongozi. Mwisho wa huu umbali kuendelea kuwa mrefu ni wasio viongozi kutaka kuondoa huu umbali kwa njia sizizo/zilizo halali. Kipindi hicho kazi zote nzuri zinazofanywa na viongozi hazitakuwa na maana na kila kitu kirudi sifuri.
 
Back
Top Bottom