Haki sawa baina ya Mwanaume na Mwanamke Haitokuja tokea kamwe

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Ni ngumu sana kubadilisha misingi ya dunia, hususa misingi ambayo aliiweka, akairidhia na kuiumba. Baada ya Mungu kuumba kila kitu Mungu. Dunia haikupendeza bila kiumbe chenye mfano wa Mungu. Ndio wakaumbwa watu wawili wenye wa mfano wa Mungu (Mwanaume na mwanamke). Lakini uumbaji haukuishia hapo.

Mwanamke wa kwanza kabla ya Eva (Hawa), aliumbwa nae kwa mfano wa Mungu. Adamu hakuweza kumtawala Wala kumuongoza, maana wote walikuwa wenye uwezo wa aina moja kilicho watofautisha ni maumbile yao tu. Basi ndipo mwanamke wa pili (Eva/Hawa) akatwaliwa ubavu mwa Adamu, baada kupewa usingizi mzito Sana. Naye Adamu alipo-amka, akamfurahia Eva na kukiri hakika huyu ni mfupa katika mifupa yangu, nyama katika nyama yangu nae nitamwita mwanamke.

Na ndipo Mwanaume atamwacha baba yake na mama yake ataambatana mkewe na watakuwa mwili mmoja.

Mwanamke wa kwanza nae aliumbwa kutumia mavumbi (Lilith), mwanamke wa pili (Eva/Hawa) alitwaliwa kwenye ubavu wa Mwanaume.

Lengo ni nini la kuanza maelezo yote haya?

Lengo ni kufumbuana tu, Mwanaume afumbuke na Mwanaume ajielewe.

Wanawake mpo?

Wanaharakati wa wanawake (Femist) Hakuna haki sawa baina ya Mwanaume na wanamke hilo mjue. There is no gender equality but you can atleast practice gender equity.

Mwanamke utawaliwa na Mwanaume katika siku zako zote za kuishi hapa duniani, Mwanamke tamaa yake itabaki kuwa chini ya Mwanaume.

<<...Mungu yu kichwa Cha Yesu Kristo, Yesu Kristo yu kichwa cha Mwanaume na Mwanaume yu kichwa Cha Mwanamke...>>

Tafsiri yake Mungu msaidizi wake mkuu ni Yesu Kristo <<"...Ameketi mkono wa kuume, ndio maana ya right hand man...>>, Msaidizi wa Yesu Kristo ni Mwanaume, msaidizi wa Mwanaume ni mwanamke. Ndio kilicho mshinda mwanamke wa kwanza (Lilith) kuwa Chini ya Mwanaume.

Tafsiri ya pili, Mungu ndie mtawala mkuu, mtawala wa pili Yesu Kristo, Mtawala wa tatu ni Mwanaume na wa mwisho Mwanamke.
 
Hata Wazungu, Wachina, Wahindi, Waarabu wanakuona hivyo hivyo kama wewe unavyowaona wanawake.
 
Hawawezi kukuelewa, hata kimaumbile tu hawako sawa, nilishangaa yule mama spika wa bunge la marekani alivyochana hotuba ya Trump hadharani, haya mambo wameyalea wazungu wenyewe acha wawapande kichwani.
 
Back
Top Bottom