Haki Nyimifu Katika Katiba-Kigoma Kusini waungana Kufungua kesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki Nyimifu Katika Katiba-Kigoma Kusini waungana Kufungua kesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amavubi, Jan 7, 2012.

 1. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,471
  Likes Received: 4,744
  Trophy Points: 280
  Wapiga kura wa jimbo la Kigoma Kusini, ambalo mbunge wake ni David Kafulila wamefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu, Dar es Salaam wakipinga kifungu kwenye Katiba kinachotamka mbunge anapovuliwa uanachama anakoma kuwa mbunge.

  Watu hao watatu walifungua kesi hiyo leo na kupewa namba 1/2012 wanakilalamikia matumi ya Ibara ya 71 (1) (f) kinachosema Mbunge atakoma kuwa mbunge iwapo ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge .

  Aidha wanaiomba mahakama hiyo iamuru Bunge litunge sheria inayoruhusu mbunge aliyefukuzwa uanachama katika chama chake awe huru aruhusiwe kuhamia chama chochote atakacho bila kuvuliwa ubunge.

  Kesi hiyo imefunguliwa zikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kuvuliwa uanachama katika chama NCCR-Mageuzi na hivyo kupoteza ubunge wake.

  Kafulia alivuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 20, mwaka jana, lakini amefungua kesi mahakamani hapo kupinga hatua hiyo ya kuvuliwa uanachama.

  Kesi hiyo ya kikatiba imefunguliwa leo na wapiga kura watatu wa jimbo ambao ni wanachama wa tofauti kwa niaba ya wananchi wengine wa jimbo hilo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Walalamikaji wanaowakilishwa na Kampuni ya uwakili ya Mpoki & Associates, ni Juma Shaban Nzengula (CCM), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kigoma kata ya Nguruka, Patrick Haruna Rubilo (NCCR-Mageuzi), mjumbe wa Kata ya Itebula na Mwenyekiti wa Kijiji cha Bweru na Fanueli Misigalo Bihole ambaye ni mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) ni Katibu wa wazazi wa Kata ya Mtegowanoti.

  Wanalalamikia kifungu hicho kinakiuka haki za msingi katika Ibara ya 21 ya Katiba inayotoa uhuru wa kushiriki katika shughuli za umma kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa mujibu wa sheria.

  Aidha Ibara hiyo inakiuka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu ambao Tanzania imeuridhia na kuusaini.

  Mbali na hayo inakiuka Ibara ya 201 (1) ya Katiba ya Nchi inayotoa uhuru kwa wananchi kushiriki na kutoa maoni yao kwa uwazi. Nje ya mahakama walidai kuwa kesi hiyo wamefungua kwa niaba ya wapiga kura wa jimbo la Kigoma Kusini baada ya kuona wimbi la kufukuzwa uanachama wabunge lililoingia sasahivi baada ya mbunge wao, Kafulila kufukuzwa NCCR na sasa mbunge wa Wawi Zanzibar (CUF), Hamad Rashid kufukuzwa.

  Wakizungumza baada ya kufungua kesi hiyo, walalamikaji hao walisema kwamba wameamua kufungua kesi hiyo liocha ya kwamba wanatoka vyama tofauti kwa kuwa mbunge huo hakuchaguliwa na wanachama wa NCCR-Mageuzi tu bali na wa vyama vingine pia.

  Walisema mbunge anakuwa ametoa ahadi nyingi baada ya kuchaguliwa, na sasa ni kipindi cha kutekeleza ikiwa ni pamoja na shunguli mbalimbali za maendeleo na hivyo ni kurudisha maendeleo nyuma.

  Kwa upande wake Rubilo alisema kuwa mbunge anafunga mkataba na wananchi na kwamba huwa wanatoa ahadi nyingi katika kutekeleza mkataba huo kama vile kusomesha watoto na shughuli nyingine za maendeleo.
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ​mbona wanongelea mbunge tu waseme ata rais akifukuzwa chamani kwake awe huru kuendelea na urais wake bila kuupoteza
   
 3. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,471
  Likes Received: 4,744
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi na hawa wa sisiem.....ni kweli inatoka rohoni au wametumwa?
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sheria hiyo haimuhusu Rais!!
   
 5. L

  Lilwayne Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa nao ni nyoko zao za kutaka wajulikane
   
 6. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,471
  Likes Received: 4,744
  Trophy Points: 280
  siyo sheria ni IBARA mkuu
   
 7. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,149
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Tatizo hapa ni siasa za mikakati na mbinu za kila namna kuhakikisha mwisho wa siku mtu wa mikakati toka ndani ya system anabaki kuwa mbunge ili PLAN 'A' iendelee kama ilivyokwisha semwa hapo awali.

  Kama suala ni mgogoro wa vifungu tajwa kikatiba,je kwa nini tatizo hili halikuonekana hapo awali japo si mara ya kwanza jambo hili kutokea.
  Mchungaji mtikila alikwisha liona hili na akachukuwa hatua husika kama mzalendo a nchi hii lakini alipuuzwa sasa leo linarudi tena.
  Nafikiri ni mtihani mwingine kwa mhimili wa kisheria nchini.
   
Loading...