Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,702
- 71,013
Wooote wanaojihusisha katika usimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kutamka neno HAKI imekuwa ngumu mno kama kutamka tusi na nguoni au kukufuru, lakini wamejikita kwenye neno AMANI na wako radhi kulitamka hata mara elfu moja na moja kwa siku.
Lakini AMANI ni tunda la HAKI, au tuseme HAKI ndio mzazi wa AMANI hivyo huyo AMANI ili umtambulishe aeleweke lazima utumie na Surname yake ambayo ni HAKI yaani AMANI s/o Haki.
Sasa shida ni nini kuogopa kumuweka wazi Haki? Sio Rais, PM, VP, viongozi wa NEC, wa dini hata wale kindakindaki wa chama tawala wote ni kushabikia tuu AMANI, AMANI, AMANI lakini wanaogopa Haki Haki Haki!
Sisi tunataka Haki tu, huyo AMANI atazaliwa ndani ya mapenzi ya haki!