Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,730
- 2,850
Hakuna ugumu wowote kwenye neno haki.kwa watawala kwa sababu tayari lipo, haki inayotafutwa kwa hao wanaolitajia ni kinyume na tamaduni zetu, hizo ndizo haki wana ziiimba.Wooote wanaojihusisha katika usimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kutamka neno HAKI imekuwa ngumu mno kama kutamka tusi na nguoni au kukufuru, lakini wamejikita kwenye neno AMANI na wako radhi kulitamka hata mara elfu moja na moja kwa siku.
Lakini AMANI ni tunda la HAKI, au tuseme HAKI ndio mzazi wa AMANI hivyo huyo AMANI ili umtambulishe aeleweke lazima utumie na Surname yake ambayo ni HAKI yaani AMANI s/o Haki.
Sasa shida ni nini kuogopa kumuweka wazi Haki? Sio Rais, PM, VP, viongozi wa NEC, wa dini hata wale kindakindaki wa chama tawala wote ni kushabikia tuu AMANI, AMANI, AMANI lakini wanaogopa Haki Haki Haki!
Sisi tunataka Haki tu, huyo AMANI atazaliwa ndani ya mapenzi ya haki!
Ila kila mtanzania ana haki ya kufanya au kupata chochote bila kuvunja sheria.
Nyie endeleeni kuomba hiyo haki ambayo ni kinyume na mila zetu za kitanzania.