Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,901
- 95,401
Jana nimemsikia Rais Samia Suluhu Hassan akidai kuwa ataanza kuteua nafasi za uongozi bila ya kuangalia vyama.Hilo halina ukakasi kwa mujibu wa sheria zetu ila kwangu mimi naamini kuwa hizo ni mbinu za kijanja janja za kurudisha utulivu wa kisiasa nchini baada ya ule uchafuzi wa wazi aliofanya mtangulizi wake Magufuli katika Demokrasia yetu.
Rais anatakiwa kuelewa kuwa political certainity haiji kwa kuteuwa wapinzani hasa wenye njaa kuwa serikalini.
Hali ya utulivu kisiasa Tanzania itakuja kwa:
1.Kuwa na chaguzi huru na haki.
2.Kuacha mihimili ya nchi kufanya kazi zake independently bila kuingiliwa wala kutishiwa na mhimili wa serikali.
3.Kuondoa uonevu wa vyombo vya usalama hasa polisi pale watu wanapotaka kufanya siasa ambayo ni haki yao kikatiba.
4.Kuwa na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
5.Dola kuacha kutumika na wanasiasa katika kuwasaidia kuingia madarakani.
6.Kuondoa sheria kandamizi na za hovyo zinazolenga kukandamiza watu.
7.Kuacha civil society
ifanye kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na serikali na kupewa vitisho.
8.Kukubali kuwa nchi hii ni ya vyama vingi na siyo lazima tuwe na mawazo sawa na CCM na hata kama tuna mawazo tofauti basi siyo maadui wa CCM au nchi.
9.CCM iache ku-label watu wanaowapinga kuwa siyo wazalendo mara wanatumika na mabeberu etc.
10.CCM ifike mahali ikubali kuwa kuna siasa za ushindani na wanaposhindwa waache kutumia dola na uhuni kubaki madarakani kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020.
Rais kuteua na kuwapa vyeo wapinzani serikalini ni MBINU YA MUDA MFUPI YA KUDHOOFISHA UPINZANI NA NI UOGA KWA RAIS.Ni matumaini yangu kuwa Rais atasoma andiko hili ili ajue kuwa wenye akili tayari tumeshajua kuwa anachotaka kufanya ni danganya toto na wala siyo kusuluhisha matatizo yetu ya kidemokrasia.
Rais anataka kutumia njia za muda mfupi kutatua matatizo ya muda mrefu kitu ambacho ni kujidanganya tu na hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya wenyewe kuwa hayapo.