Haki na Demokrasia havitakuja Tanzania kwa Rais kuwapa vyeo Serikalini Viongozi wa Upinzani

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,901
95,401
Jana nimemsikia Rais Samia Suluhu Hassan akidai kuwa ataanza kuteua nafasi za uongozi bila ya kuangalia vyama.Hilo halina ukakasi kwa mujibu wa sheria zetu ila kwangu mimi naamini kuwa hizo ni mbinu za kijanja janja za kurudisha utulivu wa kisiasa nchini baada ya ule uchafuzi wa wazi aliofanya mtangulizi wake Magufuli katika Demokrasia yetu.

Rais anatakiwa kuelewa kuwa political certainity haiji kwa kuteuwa wapinzani hasa wenye njaa kuwa serikalini.

Hali ya utulivu kisiasa Tanzania itakuja kwa:

1.Kuwa na chaguzi huru na haki.
2.Kuacha mihimili ya nchi kufanya kazi zake independently bila kuingiliwa wala kutishiwa na mhimili wa serikali.
3.Kuondoa uonevu wa vyombo vya usalama hasa polisi pale watu wanapotaka kufanya siasa ambayo ni haki yao kikatiba.
4.Kuwa na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
5.Dola kuacha kutumika na wanasiasa katika kuwasaidia kuingia madarakani.
6.Kuondoa sheria kandamizi na za hovyo zinazolenga kukandamiza watu.
7.Kuacha civil society
ifanye kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na serikali na kupewa vitisho.
8.Kukubali kuwa nchi hii ni ya vyama vingi na siyo lazima tuwe na mawazo sawa na CCM na hata kama tuna mawazo tofauti basi siyo maadui wa CCM au nchi.
9.CCM iache ku-label watu wanaowapinga kuwa siyo wazalendo mara wanatumika na mabeberu etc.
10.CCM ifike mahali ikubali kuwa kuna siasa za ushindani na wanaposhindwa waache kutumia dola na uhuni kubaki madarakani kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020.

Rais kuteua na kuwapa vyeo wapinzani serikalini ni MBINU YA MUDA MFUPI YA KUDHOOFISHA UPINZANI NA NI UOGA KWA RAIS.Ni matumaini yangu kuwa Rais atasoma andiko hili ili ajue kuwa wenye akili tayari tumeshajua kuwa anachotaka kufanya ni danganya toto na wala siyo kusuluhisha matatizo yetu ya kidemokrasia.

Rais anataka kutumia njia za muda mfupi kutatua matatizo ya muda mrefu kitu ambacho ni kujidanganya tu na hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya wenyewe kuwa hayapo.

Kama kawaida binadam wengi hamna jema. Hata akifanya hayo bado mtakuja kulalamika kuwa raisi anafanya haya ili kujitengenezea mazingira ya ushindi 2025.

Ukitaka kujua ukweli wa haya ninayokwambia rudi nyuma kidogo utakuta kuna viongozi walikuwa wanahitaji mtu dikteta kuongoza nchi hii, alipopatikana huyo waliemwita dikteta wale wale wakaanza kulalamika kuwa nchi hii haihitaji kuongozwa na dikteta

Pia walipinga rais kusafiri safiri, lkn alipoingia aliefata ushauri wao wa kutokusafiri wale wale wakalalamika kwanini raisi hasafiri. Walitaka elimu iwe bure ilipotolewa bure wakaanza tena kulalamika kuwa kwanini serikali inatoa elimu bure.

Walitaka nchi iwe na angalau ndege moja au mbili, ziliponunuliwa ndege tatu au nne wakaanza kupinga nk. So kwa kweli hata haya yakitimizwa bado mtalalamika tu kama kawaida yenu, kwa vile kula kwenu kunatokana na kulalamika kwenu.
 
Kuteua wapinza hakuta dhoofisha upinzani kutaimarisha umoja wa kitaifa, kinacho dhoofisha upinzani ni unyumbu wa aliyetuliwa(kujitoa ufahamu) 'herding behavior' thoughtful people suspending their individual thinking because of fear(Amygdala)
 
Sukuma gang na MATAGA mmegeuka kuwa wapinzani wakuu wa Mama Samia
 
Kwani anawalazimisha!?! kama hawataki kujenga nchi yao wenyewe na wana nondo za kusaidiana na kiongozi aliyepo kisa ni upinzani basi wakatae,uchaguzi ukiisha hakuna mpinzani wote tunaungana kujenga nyumba moja hadi uchaguzi mwingine
 
ikiwa upinzani utazichanga vyema karata zao teuzi hizi zitawaimarisha sana kisiasa bt angalizo wasikubali tu kutumika kisiasa
 
Jana nimemsikia Rais Samia Suluhu Hassan akidai kuwa ataanza kuteua nafasi za uongozi bila ya kuangalia vyama.Hilo halina ukakasi kwa mujibu wa sheria zetu ila kwangu mimi naamini kuwa hizo ni mbinu za kijanja janja za kurudisha utulivu wa kisiasa nchini baada ya ule uchafuzi wa wazi aliofanya mtangulizi wake Magufuli katika
demokrasia yetu.

Rais anatakiwa kuelewa kuwa political certainity haiji kwa kuteuwa wapinzani hasa wenye njaa kuwa serikalini.

Hali ya utulivu kisiasa Tanzania itakuja kwa:

1.Kuwa na chaguzi huru na haki.
2.Kuacha mihimili ya nchi kufanya kazi zake independently bila kuingiliwa wala kutishiwa na mhimili wa serikali.
3.Kuondoa uonevu wa vyombo vya usalama hasa polisi pale watu wanapotaka kufanya siasa ambayo ni haki yao kikatiba.
4.Kuwa na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
5.Dola kuacha kutumika na wanasiasa katika kuwasaidia kuingia madarakani.
6.Kuondoa sheria kandamizi na za hovyo zinazolenga kukandamiza watu.
7.Kuacha civil society
ifanye kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na serikali na kupewa vitisho.
8.Kukubali kuwa nchi hii ni ya vyama vingi na siyo lazima tuwe na mawazo sawa na CCM na hata kama tuna mawazo tofauti basi siyo maadui wa CCM au nchi.
9.CCM iache ku-label watu wanaowapinga kuwa siyo wazalendo mara wanatumika na mabeberu etc.
10.CCM ifike mahali ikubali kuwa kuna siasa za ushindani na wanaposhindwa waache kutumia dola na uhuni kubaki madarakani kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020.

Rais kuteua na kuwapa vyeo wapinzani serikalini ni MBINU YA MUDA MFUPI YA KUDHOOFISHA UPINZANI NA NI UOGA KWA RAIS.Ni matumaini yangu kuwa Rais atasoma andiko hili ili ajue kuwa wenye akili tayari tumeshajua kuwa anachotaka kufanya ni danganya toto na wala siyo kusuluhisha matatizo yetu ya kidemokrasia.

Rais anataka kutumia njia za muda mfupi kutatua matatizo ya muda mrefu kitu ambacho ni kujidanganya tu na hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya wenyewe kuwa hayapo.

*Mods naombeni hapo kwenye Tittle kuwe 'vyeo serikalini' badala ya 'vyeo serikali'

Mkuu suala la msingi hapa ni KATIBA MPYA. Hili jambo lisiwe hisani ya Rais katika kuteua wapinzani bali liwe kwa mujibu wa KATIBA, kama ilivyo Zanzibar kwamba Chama kikipata nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu ndio kiunde Serikali ya MSETO.
 
Cha muhimu kuliko vyote ni kufuata katiba na sheria.
Serikali itekeleze majukumu yake kwa haki na kwa mujibu wa katiba na sheria.
Wapinzani waachwe wafanye siasa zao bila kuvunjwa kwa sheria.
Kuna faida kubwa sana kwa taifa kuwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu.
 
Kama kawaida binadam wengi hamna jema. Hata akifanya hayo bado mtakuja kulalamika kuwa raisi anafanya haya ili kujitengenezea mazingira ya ushindi 2025. Ukitaka kujua ukweli wa haya ninayokwambia rudi nyuma kidogo utakuta kuna viongozi walikuwa wanahitaji mtu dikteta kuongoza nchi hii, alipopatikana huyo waliemwita dikteta wale wale wakaanza kulalamika kuwa nchi hii haihitaji kuongozwa na dikteta. Pia walipinga raisi kusafiri safiri, lkn alipoingia aliefata ushauri wao wa kutokusafiri wale wale wakalalamika kwanini raisi hasafiri. Walitaka elimu iwe bure ilipotolewa bure wakaanza tena kulalamika kuwa kwanini serikali inatoa elimu bure. Walitaka nchi iwe na angalau ndege moja au mbili, ziliponunuliwa ndege tatu au nne wakaanza kupinga nk. So kwa kweli hata haya yakitimizwa bado mtalalamika tu kama kawaida yenu, kwa vile kula kwenu kunatokana na kulalamika kwenu.
Je! Hoja zilizotolewa hazina ukweli/ uhalisia?
 
Kama kawaida binadam wengi hamna jema. Hata akifanya hayo bado mtakuja kulalamika kuwa raisi anafanya haya ili kujitengenezea mazingira ya ushindi 2025.

Ukitaka kujua ukweli wa haya ninayokwambia rudi nyuma kidogo utakuta kuna viongozi walikuwa wanahitaji mtu dikteta kuongoza nchi hii, alipopatikana huyo waliemwita dikteta wale wale wakaanza kulalamika kuwa nchi hii haihitaji kuongozwa na dikteta

Pia walipinga rais kusafiri safiri, lkn alipoingia aliefata ushauri wao wa kutokusafiri wale wale wakalalamika kwanini raisi hasafiri. Walitaka elimu iwe bure ilipotolewa bure wakaanza tena kulalamika kuwa kwanini serikali inatoa elimu bure.

Walitaka nchi iwe na angalau ndege moja au mbili, ziliponunuliwa ndege tatu au nne wakaanza kupinga nk. So kwa kweli hata haya yakitimizwa bado mtalalamika tu kama kawaida yenu, kwa vile kula kwenu kunatokana na kulalamika kwenu.
Mimi nimezungumzia mambo ambayo yapo kwa mujibu wa katiba yetu.Hakuna mtu ambae atalalamika kisa serikali inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa katiba.

Hayo uliyoyazungumzia wewe ni masuala ambayo hayapo kikatiba kwa hiyo watu wana haki ya kulalamika kadri hisia zao zinavyowatuma.Tofauti yangu mimi na wewe ni kwamba mimi nimezungumzia mambo ambayo tayari yapo katika katiba yetu lakini serikali haiyatekelezi ila wewe umezungumzia mambo ambayo ni matamanio ya watu.
 
Kama kawaida binadam wengi hamna jema. Hata akifanya hayo bado mtakuja kulalamika kuwa raisi anafanya haya ili kujitengenezea mazingira ya ushindi 2025.

Ukitaka kujua ukweli wa haya ninayokwambia rudi nyuma kidogo utakuta kuna viongozi walikuwa wanahitaji mtu dikteta kuongoza nchi hii, alipopatikana huyo waliemwita dikteta wale wale wakaanza kulalamika kuwa nchi hii haihitaji kuongozwa na dikteta

Pia walipinga rais kusafiri safiri, lkn alipoingia aliefata ushauri wao wa kutokusafiri wale wale wakalalamika kwanini raisi hasafiri. Walitaka elimu iwe bure ilipotolewa bure wakaanza tena kulalamika kuwa kwanini serikali inatoa elimu bure.

Walitaka nchi iwe na angalau ndege moja au mbili, ziliponunuliwa ndege tatu au nne wakaanza kupinga nk. So kwa kweli hata haya yakitimizwa bado mtalalamika tu kama kawaida yenu, kwa vile kula kwenu kunatokana na kulalamika kwenu.
Acha upotoshaji usio na tija yoyote boss. Watu walikuwa wanahitaji kiongozi dictator sio wa kuvunja utaratibu. Kama alisikia kilio cha watu kuwa kunahitaji kiongozi dictator na akaona acha awe dictator, mbona tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ni kelele ya muda mrefu na hajatii kelele hizo? Yule alikuwa dictator wa kuzaliwa na wala si kutii kelele zilizokuwepo.

Hili suala la kusafiri, kelele ilikuwa ni kusafiri sana hata safari zisizo na tija, na sio kusafiri tu. Acha upotoshaji tafadhali.

Elimu bure, ni wapi walioitaka ilipotolewa wakaikataa? Ukiishiwa na utetezi ni vyema kukaa kimya kuliko kupotosha.

Hakuna aliyepinga uwepo wa ndege, watu walipinga mchakato wa manunuzi ya ndege, hasa kwa mtindo wa cash wenye usiri mkubwa. Na pia ilipasawa kipaombele kiwe nini kabla ya ununuzi wa ndege kwa mtindo wa cash. Na ili taifa liwe na afya mijadala ya hivyo ni muhimu.

Mimi sishauri wapinzani wakubali vyeo, bali wampe mama ushirikiano, lakini mama awe na wajibu wa kuhakikisha katiba mpya tena ile rasimu ya Warioba inapatikana. Wakati huo huo ahakikishe demokrasia inaheshimiwa kwa mujibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom