Haki msingi wa amani, na haki ni kwa wote, kokote, bila ubaguzi - Jenerali Ulimwengu

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,072
2,000
9 Julai 2020

Haki msingi wa amani, na haki ni kwa wote, kokote, bila ubaguzi - Jenerali Ulimwengu

Source : Jenerali Online

Dhana ya Msamaria Mwema niliyoitumia kuhitimisha makala yangu ya mwisho ni muhimu sana katika falsafa ya kisasa kwa maana kwamba inaelezea wema unaotendwa na mtu ambaye ndani ya jamii husika hatarajiwi kutenda wema. Msamaria Mwema aliyetolewa mfano na Bwana Yesu alikuwa mpita njia tu, kama walivyokuwa wapita njia wengine waliomkuta msafiri kapigwa, kaporwa na yu mahututi, mlangoni mwa kifo.

Walikwisha kupita watu wenye sifa za kutenda wema, wakiwemo makuhani, lakini wote walimuona mtu huyo kama mtu asiye na thamani, na wala hawakuona sababu ya kumsaidia. Hali yake ilikuwa haiwahusu, na ilibidi yeye mwenyewe apambane na hali yake, kama msemo wa siku hizi ulivyo. Msamaria akamuonea huruma mhanga yule, akamchukua, akampeleka hadi hospitalli, akamkabidhi kwa wauguzi na akalipia matunzo yake.

Ipo tofauti kubwa baina ya binadamu na mtu. Binadamu maana yake ni mwana wa Adamu na Hawa, kama ambavyo vitabu vya hekaya za Wayahudi zinavyoeleza. Sote tunachukuliwa kama watoto wa hao wawili waliokula lile tunda na, kutokana na kula lile tunda, wakatuachia changamoto za kila aina hadi leo hii. Mtu ni tofauti, kwa sababu pamoja na kuwa binadamu kwa maana niliyoeleza hapo juu, ana sifa ya nyongeza, kwa sababu yeye ana utu ndani yake.

Nakumbuka wimbo mmoja wa marehemu Marijani Rajabu ambamo anasema. ‘kwenye watu kumi, binadamu mmoja’. Niliwahi kumwambia mwanaziki huyo kuhusu kosa lake, lakini nilikubaliana naye kwamba ilikuwa haiwezekani kurekebisha kosa hilo, hasa kwa sababu halaiki ya wapenzi wa muziki walikwisha kulikubali kosa hilo kama sahihi.

Lakini uhalisia wa maneno hayo unatuambia kwamba ingawa wote waliopita na kumuona bwana yule amepigwa na kaumia walikuwa wote ni binadamu, aliyekuwa na UTU alikuwa ni mmoja peke yake, yule Msamaria, mtu wa kabila lisilo na thamani lakini yeye mwenyewe akawa na roho ya utu. Huko ndiko inakotokea dhana ya kisasa ya UBUNTU iliyoibuliwa na ndugu zetu wa Afrika Kusini, hata kama wao wenyewe kwa kiasi kikubwa dhana hiyo inawashinda.Na tuwe watu, basi, badala ya kuwa binadamu tu, kwa sababu ni utu peke yake unaotutofautisha na hayawani. Utu unatutaka tuwatendee wenzetu, hata tusiowajua, kama vile ambavyo tungependa sisi wenye tutendewe na wenzetu, hata kama hawatujui. Kumtendea wema mtu unayemjua ni jambo jema, lakini inawezekana wema huo umetokana na jinsi unavyomjua huyo unayemtendea wema.

Inawezekana huyo unayemtendea wema ni ndugu yako au rafiki yako, la sivyo usingetenda wema uliotenda. Huo ni wema wa bei kidogo, kwa sababu kwa maana moja, huo ni wema unaojitendea wewe mwenyewe. Wema unayemtendea mtu usiyemjua unayo thamani kubwa zaidi, kwa sababu hapo unatenda wema kwa ajili ya kutenda wema, na si kwa sababu ndugu yako au rafiki yako anahusika.

Hii inatufundisha tuwe na roho ya kuwapenda watu wote na kuwasaidia. Bila shaka kama falsafa hii ingetamalaki katika jamii iliyo pana tungekuwa na watenda wema kila kona ya jamii, na wala tusingekuwa na haja ya mahubiri ya kila wikiendi ya kuhamasishana kutenda wema.Unapita mtaani, na unashuhudia uovu ukitendeka lakini anayetendewa uovu huo ni mtu usiyemjua, na kwa sababu humjui, unajipitia na kuendelea na hamsini zako. Umeshindwa kutenda wema. Unamkuta mtu anatenda kosa kwa makusudi, lakini kwa sababu kosa hili hakikuumizi wewe mwenyewe kwa namna yo yote ile, unaona ni jambo lisilokuhusu na unaendelea na safari yako kana kwamba hukuona jambo lo lote.

Kosa la kuwa na mitazamo kama hii ni kwamba si wewe pekee utakayefanya hivyo. Wenzako pia, katika pita-pita zao watashuhudia maovu kama lile uliloshihudia na watakaa kimya kwa sababu hayawahusu, lakini kumbe linakuhusu wewe, lakini kwa sababu jamii yenu ilikwisha kujizoeza kutokuingilia mambo yasiyowahusu, utaumia na hakuna atakayekusikia.

Watanzania tumekwisha kufikia kiasi hiki cha kutokujali. Tunawaona watu wanaumizwa kila siku, lakini kwa sababu hao wanaoumia si ndugu zetu au marafiki zetu, tunaendelea na hamsini zetu kama vile hatujaona kitu. Tunasahau kwamba na sisi tutakapokuja kupatwa na hayo, wenzetu nao hawataona tunavyoteseka. Hakuna utu unaotendeka kwa kubaguana baina ya wale wanaostahili kutendewa haki na wale wasiostahili kutendewa haki. Bima ya kweli ya w ewe kutendewa haki na watu wasiokujua ni wewe kutenda haki kwa wale usiowajua.Tumewaona wakuu wa polisi wakiangalia watu wanapigwa na kuumizwa, halafu wakuu hao wanatoa visingizio vya kutia kichefuchefu, mara nyingi wakiwalaumu wahenga kwamba ndio walioanzisha fujo. Mkuu kama huyo wa polisi akija kumkuta mwanaye kapigwa na kutobolewa jicho na askari polisi asiyemjua, atakuwa na ujasiri wa kumlaumu mwanaye kwa kuwa sababu au chanzo cha kujeruhiwa kwake?

Tunashuhudia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka mbali mbali ambamo vinaingizwa vipengele vya money laundering , hata katika mazingira yasiyofanana kabisa na kosa hilo. Kisa ni kwamba waendesha mashitaka wanatafuta njia ya kuhakikisha kwamba mshitakiwa hatoki nje kwa dhamana.

Halafu, kwa muda mrefu tumekuwa na utaratibu ambao sielewi ulitoka wapi, eti ofisa huyo huyo anayekushitaki ndiye pia amwambie hakimu iwapo unafaa kupewa dhamana au la! Mambo yale yale, ya riwaya za George Orwell. Huyu ndiye anashitaki, na anataka mshitakiwa afungwe, halafu ndiye anaulizwa iwapo anadhani ni sawa kwa mshitakiwa kuachiwa kwa dhamana! Tusije kuwasingizia Wazungu kwamba ndio waliotufundisha mantiki hii. Hii ni yetu na tuliipata kule kule katika ‘collective imbecilization’ ya Seithy Chachage.Wakati naandika makala hii tumepata habari kwamba katika jimbo fulani la ubunge, mgombea wa chama cha upinzani ameshindwa kukabidhi fomu za kumfanya mgonbea, halafu anatangazwa mgombea wa chama tawala kwamba amepita bila kupingwa! Hivi huu si utaratbu wa kuwafanya watu wapate kichaa na hatimaye waseme, ‘liwalo na liwe!’?

Najiuliza ni kwa nini tunadhani kwamba vurugu zinazozuka katika nchi nyingine za bara la Afrika haziwezi kutokea kwetu. Wale waliokumbwa na vurugu tunazozifuatilia ni watu wenye akili kama sisi, na hawajamkosea Mungu kwa kiasi kinachozidi makosa yetu kwa Bwana Mkubwa huyo. Ni kwa nini tunadhani kwamba sisi tunayo kinga inayotufanya tuenende bila kujali mantiki, halafu tuepukane na hayo yaliyowapata wenzetu?

Msingi wa amani ni haki, bila haki hatuwezi kuwa na amani. Aidha, haki haina tabia ya kuangalia sura ya mtu, wala kabila lake, wala dini yake. Ndiyo maana alama ya haki duniani kote ni yule mawanamama aliyefungwa kitambaa usoni; haoni. Tunapokuwa na mifumo ya kutoa haki kwa upendeleo unaotokana na kuwaangalia watu usoni hatutakuwa na haki hata chembe.Nasema kwamba msingi wa haki zote ambazo tunadai leo ni haki ya ushiriki wa kisiasa. Bila kuwa na haki katika ushiriki katika siasa hatuwezi kubuni haki nyingine zo zote na zikawa na mashiko. Ushiriki wa kisiasa kwa raia wote unapokuwa umetengenezewa mifumo inayokubalika na watu wakairidhia, ndiyo bima ya juu kabisa ya kuondoa uwezekano wa chokochoko ndani ya jamii.

Mtawala mwenye busara ataiona hii mantiki, na kila siku atapanuwa wigo wa ushiriki huo ili asiachwe ye yote nje ya wigo wa ushiriki wa kisiasa. Mtawala asiye na busara hii atazidi kila siku kubinya hata ule wigo uliopo, huku akiongeza asilimia ya wale wanaoachwa nje ya wigo wa ushiriki. Huyo anaitakia majanga jamii yake.
Source: Haki msingi wa amani, na haki ni kwa wote, kokote, bila ubaguzi
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,349
2,000
MUONGOZO WA SHURA YA MAIMAMU TANZANIA UCHAGUZI MKUU WA TAIFA OKTOBA 2020

Shura ya Maimamu wa Tanzania imetoa waraka unaohusu Uchaguzi Mkuu.

Katika waraka huu au muongozo huu kuna mengi ya kufikirisha sana kiasi mtu atajiuliza haya yanawezekana vipi kutendeka katika nchi inayojinadi kuwa inazingatia haki na usawa kwa wananchi wake wote na inapiga vita ubaguzi wa aina yoyote.

Katika mengi niliyosoma hili hapo chini nikilijua siku nyingi na limekuwa likinisikitisha sana.

Kwa kuwa waraka wamelieieza naona itakuwa vyema nikaliweka hapa kwa faida ya wasomaji:

Uadilifu I

''Januari 11, 2019, serikali ilifanya uhamisho mkubwa wa kushitukiza kwa wahadhiri na watumishi wandamizi katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Dodoma-UDOM.

Waliohamishwa walikuwa 11, lakini wote walikuwa Waislamu:

Dk. Maryam Khamis (Director of Graduate Studies), Dk. Ibun Kombo (Political Science), Dk. Mwinyikombo Amir (Mwalimu wa Udaktari wa Binadamu), Dk. Yusuf Kambuga (College of Education), Dk. Masoud Masoud (Informatics) , Bw. Subira Sawasawa (Mkurugenzi Mkuu Rasilimali Watu), Bw. Mohamed Mwandege (Bursar/Mhasibu Mkuu), Bi. Aziza Gendo (Seniour Estate Oficer), Bw. Simba Omary (Senior Supplies Oficer), Bw. Wema Mbegu (Legal Oficer), Bw. Khamis Mkanachi (Mwalimu wa Idara ya Historia).

Barua zao za uhamisho hazikuonesha makosa katika utendaji wao wa kazi au uongozi. Pamoja na kutokuwa wakosaji, uhamisho wao uliambatana na udhalilishaji mkubwa, kunyimwa haki stahiki za uhamisho, kuhamishiwa katika nafasi za chini kinyume na hadhi zao.

Baada ya uhamisho huo, Serikali ilifanya uteuzi mwingine katika chuo hicho hicho cha Serikali.

Katika uteuzi huo walioteuliwa walikuwa 11, wote Wakristo: Prof. Leonard James Mselle, Prof. Adam B. Swebe Mwakalobo, Prof. Julius William Nyahongo, Prof. Justin Ntalikwa, Prof. Frowing Paul Nyoni, Prof. Odass Bilame, Prof. Ainory Piter Gasese, Dkt. Victor George Mareale, Dkt. Alex Shayo, Dkt. Calvin Swai, Dkt. Augustine Mwakipesile.

Kuhamisha wahadhiri 11, katika Chuo Kikuu si jambo dogo.

Vilevile kuhamisha Wahadhiri 11, wa dini moja (Waislamu) katika Chuo Kikuu ukaingiza wahadhiri 11 wa dini moja (Wakristo), na hao Waislamu 11, baadhi yao ukawatoa kabisa katika mfumo wa elimu kwa kuwapeleka sekta nyingine na zisizo lingana na hadhi zao si jambo dogo. Wala si hatua ya kitaalamu ya kuboresha mfumo wa Elimu wa Taifa.

Na wala si hatua ya kijinga bali ya werevu uliofurutu ada dhidi ya maslahi ya Taifa.

Hatuwa hiyo ni salamu nzito kwa jamii yao na Taifa kwa ujumla. (Ndio maana katika maoni yetu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tulipendekeza Katiba Mpya imtambuwe Mwenyezi Mungu na Dini liwe suala rasmi na la wazi katika uendeshaji wa nchi).''
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,072
2,000
9 Julai 2020

SHEIKH PONDA AFUNGUKA MAZITO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Source : DARMPYA TV

  1. Maboresho ya kanuni za uchaguzi
  2. Watu washiriki ktk uchaguzi wa Mpito huku tukitegemea Tume Huru huko baadaye.
  3. Mahitaji ya Kundi-maslahi
  4. Sifa za mgombea urais

More info :
Waislamu Tanzania wataka uchaguzi huru na wa haki, wataja sifa za wagombea
Jul 09, 2020 15:32 UTC
  • Waislamu Tanzania wataka uchaguzi huru na wa haki, wataja sifa za wagombea
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki mwezi Oktoba mwaka huu nchini humo.
Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa mwito huo leo Alkhamisi katika kikao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, vyombo husika vinapaswa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki.
Kuhusu sifa za wagombea wa uchaguzi mkuu, Sheikh Ponda amesema waraka uliotolewa na taasisi hiyo imeorodhesha baadhi ya sifa hizo kama ifuatavyo: mgombea awe mkweli na mwenye utu, awe mwenye kuheshimu kiapo, awe mwenye sifa ya kupiga vita ubaguzi wa aina zote na awe mwenye maarifa ya kutosha ya kuongoza watu na serikali.
Sifa zingine zilizoainishwa kwenye waraka huo wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ni mgombea awe mwenye kuheshimu uhuru na mawazo ya watu wengine, mbali na kuzijua na kuziheshimu haki za binadamu. Kadhalika taasisi hiyo ya Waislamu wa Tanzania imetaka wananchi wasiwachague watu madikteta na wadhalilishaji katika uchaguzi huo wa Oktoba.
Sheikh Issa Ponda na viongozi wengine wa Kiislamu katika kikao na wanahabari Dar es Salaam
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania amesema Waislamu wa Tanzania wanataka haki na usawa na ndipo wamekuwa wakishiriki katika chaguzi mbali mbali za nchi hiyo. Amesema Waislamu wa Tanzania hivi sasa hawaoni nafuu katika uhuru wa kuabudu, uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe, usalama wa viongozi wao, Madrasa zao, Misikiti na watu wao.
Aidha ameeleza bayana kuwa, Waislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki hawaoni usawa wowote katika madaraka na ajira za serikali, na kwamba mfumo wa elimu wa taifa hilo umeshindwa kutoa fursa sawa wala kutenda haki kwa wote.

Source : Waislamu Tanzania wataka uchaguzi huru na wa haki, wataja sifa za wagombea
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,072
2,000
ASKOFU MUNGA :HATUWEZI KUKUBALI KUFUNGWA MIDOMO KISA MAENDELEO


Source : DARMPYA TV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom