Haki mpiga kura na utetezi wa wasomi waliosomeswa kwa fedha za kifisadi


N

nina90

Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
38
Likes
0
Points
0
N

nina90

Member
Joined Oct 21, 2010
38 0 0
Mkusanyiko wa viongozi waliojiteua kwa uwezo wa pesa zilizizoibwa kwa wananchi na kuzitumia kujijengea uimara wa kiuchumi na kisiasa huwa siku zote unatumia kila aina ya mbinu kurubuni wavuja jasho ambao ama hawakupata elimu ya kutosha kuweza kukokotoa hoja kukdhi haja ya wanaojiita wasomi waliopata elimu kwa gharama za kodi za hao hao wavuja jasho ambao siku zote huomba na kutumaini kuwa siku moja atatokea kiongozi asiye mbadhirifu na mwenye uchungu na nchi atakaye kuwa radi kuwakomboa katika hii minyororo mikubwa ya kifisadi.

Fedha za wavuja jasho (kodi) zimetumika kuwapa elimu nzuri ya ndani na hasa nje ya nchi vijana wa viongozi ambao mara wapatapo elimu hiyo hawaitumii kuliendeleza taifa lao kama ambavyo kwa mtu mwenye busara angefanya bali wengi wao huitumia elimu hiyo kujenga hoja za kulinda maslahi ya kisiasa na kiuchumi kwa niaba ya baba na mama na utitiri wa wa mali walizofisadi. Hivi ni kweli tusomeshwe kwa gharama kubwa nje ya nchi kwa kodi za wavuja jasho kisha tuitumie elimu hiyo kuwaona wasioweza kuchangia hoja kama nyie (wasomi wa fedha za kifisadi) kuwa hawajui kujenga hoja??? ni haki hiyo? eti kwa sababu mnatetea maslahi ya baba au mama? tafakuri....

Pili, majambo haya na mengineyo yanayojionyesha wazi katika utajiri uliokithiri wa wanasiasa ambao kabla ya kuwa siasani walikuwa sawa na wavuja jasho wengiwalivyo lakini ghafla baada ya kuingia madarakani wameweza kuwa na ama mahekalu ya mabilioni pesa ambazo hata kama ungejumlisha mishahara na mapato halali ya uongozi usingeweza kujenga hata banda la nyuma la mahekalu hayo. Lingine ni umilikaji wa mali ambazo zilikuwa za umma kwa viongozi wa kisiasa, familia zao. Pia umilikishwaji na kuwa hisa kubwa katika mali adimu kama madini na migodi yake, wizi wa mabilioni katika benki zetu, ukopaji wa mabilioni ktk benki za nchi yetu kisha kuyakimbia madeni kwa njia za mkato.

Mambo haya na mengineyo ndo humfanya mwananchi wa kawaida kushindwa kuelewa nini kinaendelea katka nchi yake yenye kila aina ya utajiri kuanzia madini, ardhi, bahari mito na utawala wa chama kimoja kwa miaka 50 tangu kuchukua uhuru kwa mkoloni msimamizi (Great Britain)...chakula mlo mmoja, huduma duni za afya uadimu wake , elimu duni, kazi hakuna, mishahara haikidhi mahitaji muhimu n.k
Ujumla huu wa hali duni za maisha wananchi na utajiri wa asilimia zaidi ya 200000 % kwa miaka 50 ya uongozi wa chama kimoja zimewafanya wananchi kutaka mabadiliko ya uongozi na viongozi ili walau wapate kuchangia kufaidi matunda ya nchi yao.Kura wamepiga kwa moyo mmoja ila matokeo yanachujwa au kwa msamiati mzuri zinachakachuliwa ili kulinda maslahi ya wachache na kudharau au kukejeri matakwa ya wengi....
 

Forum statistics

Threads 1,236,909
Members 475,327
Posts 29,272,070