Haki huinua taifa ni maneno yanayopatikana kwenye vitabu vitakatifu vya dini

kamjabari

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
1,132
1,640
Viongozi wanapo kuwa WANYENYEKEVU na WATENDA HAKI ndani ya Nchi hakika taifa hubarikiwa kwa kila "sector"

Ni mda mwafakaTaifa letu linapaswa sasa kuliunganisha kuwa taifa lenye watu wanao pendana na kutunza amani ya moyoni na machoni.

Mataifa makubwa wanajua umuhimu wa jambo hili, wapo makini sana kuhakikisha amani moyoni mwa mtu mmojammoja ina sitirika daima na kuimarisha amani ya taifa zima kwa ujumla, kwani amani ya taifa hutokana na amani ya ndani ya mioyo yao .

Mungu humimina Baraka zake kwa taifa ambalo viongozi wake wana heshimu na kujari haki za raia wao kwa vyovyote vile iwavyo.

Mfano:
Marekani polisi alipo muua raia mwenye asili ya Africa (GEORGE FLOYD) Serikali ya Marekani ili hakikisha Jambo hilo inalibeba na kujionyesha ndani ya America na Duniani kwamba imeguswa na ukatili ule na ipo pamoja na raia.

Kinyume na hapa kwetu Tanzania ,Matukio ya polisi kuua watu haliwi Jambo la kushitua serikali, Mungu hukasilishwa sana na umwagaji wa damu za watu bila sababu ni ngumu sana Nchi kubarikiwa Kama damu za watu zina mwagwa bila utaratibu wa Mungu.

Mfano:
Polisi waliwahi kuua mwandishi wa habari pale Nyororo (Mwangosi) aliye kuwa akiteleza majukumu yake ya kiuandishi,Kupotea kwa Been Saananne, Azole Gwanda, Kupigwa risasi Aqulina na kufa, Kupigwa risasi Tundu Lissu na kuponea chupuchupu nk.

Hizi damu zote zime liliwa na ndugu na jamaa zao mbele za Mungu ,Hivi wazazi au watoto wa watu hao wanajisikiaje kuona wanadhurumiwa maisha ya ndugu zao kikatili hivyo, wanapo mlilia Mungu je hatoi laana kwa nchi?

Hata hivyo pamoja na uharibifu mkubwa huo wa maisha ya watu polisi au serikali haija wai kuomba msamaha kwa wananchi wao au kwa Ndugu wa marehemu au Tundu Lissu aliye nusulika kufa kwa kuto onyesha uwajibikaji 100% kwa jeshi la polisi .

Marekani pamoja na ukubwa wa taifa lao lakini polisi na serikali iliomba msamaha tena rais alipiga magoti mbele ya mtoto wa marehemu , vivyo hivyo polisi waliomba msamaha kwa wananchi hadharani kwa kupiga magoti.

Ni kwamba wanajua umuhimu wa kutuliza hasira za ndani na kujenga amani moyoni mwa raia wao , wanajua umuhimu wa kuheshimu na kuwanyenyekea wananchi wao ,ndiko zinako toka Baraka za taifa na amani ya nchini kwao .

Mwisho
Naishauri na kuiomba serikali yetu kuwaomba msamaha wananchi na ndugu wa marehemu hadharani , kuiunganisha taifa ili Upendo wa kweli utamalaki nchini, kinyume na sasa siasa zilivyo tupalaganya.


FB_IMG_1641930022145.jpg
FB_IMG_1641929917624.jpg
 
Haya kijana subiri data zako kutoka kwa katibu mkuu wa chama chenu, na kesho utarushiwa buku 5 ya kula mihogo na juice. Ingawa tuhuma zako na ulichoandika havina ushahidi wowote, ila ndo hivyo kila kijana kaishageuza uhana harakati kuwa ajira ya kujipatia data za bure na buku tano tano za mihogo kutoka kwa katibu mkuu wa chama.
 
Mimi nilijua matendo ya Ndugai alikuwa akifanya kuwafurahisha wanaccm.

Kumbe mambo maovu hata wao wanayaona. Walivyompopoa ndio watawala wajifunze kumbe uovu unachukiwa na kila mtu. Na kwamba Ndugai alijenga chuki kwa watu wote chadema, ccm na wasio na vyama.

Anguko lake watu wote wameshangilia hasa wanaccm wenzake aliodhani kuwa anawafurahisha
 
Back
Top Bottom