Haki haiombwi inatafutwa/kupiganiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki haiombwi inatafutwa/kupiganiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by emrema, Nov 12, 2011.

 1. e

  emrema JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeshuhudia siku ya jana ikitawaliwa na mapambano makali kati ya Polisi (Chombo cha dola) na wananchi ambao ni jamii ya watanzania waliotelekezwa kwa makusudi na Serikali walioipa dhamana ya kuwahudumia. Nikiwa mmoja wa wafanyakazi wa Chuo Kikuu nilipata usumbufu mkubwa kupita katika barabara ya kuingia kazini. Nilipata hasira sana.

  Waziri mkuu anasimama bungeni na kudai maandamano yanakwamisha maendeleo anaonyesha upeo mdogo wa kujua kwa nini watu wanaandamana mfano wasomi wa chuo kikuu. Mishahara siku hizi kwa wafanyakazi hata wa vyuo vikuu inalipwa tarehe 5 hadi 10 hapa je si kupalilia maandamano zaidi?

  Wanafunzi wamedai haki yao ya kuishi hawajapata na hata kupewa majibu ya kutia moyo.Nimeshuhudia mwanafunzi yupo ndani ya eneo la chuo anapigwa na polisi kama mwizi bila msaada wowote. Hebu fikiria yale tunayoyaona, mwanafunzi anaingia darasani nusu saa tu anaonyesha kuchoka na kusinzia sababu ya njaa hapo ni lecture ya masaa 2. Wewe mwalimu unaona zaidi ya nusu ya wanafunzi wapo kwenye hali hiyo, je unapata morali kweli ya kufundisha darasa kama hilo? Wanafunzi wengi wanachelewa kuingia darasani sababu inabidi watembee kwa miguu kwa kukosa nauli. Wengi wanaomba misaada kwetu walimu je tutawasaidia wangapi na kwa muda gani? Kibaya zaidi tunawaletea polisi wawapige mabomu na mitama. Ndio hata sisi tulipigwa sana tu miaka hiyo ya 2000 ila je hakuna mbinu nyingine ya kudeal na hili. Nashauri Wanafunzi waendelee KUPIGANIA haki yao HAKI HAIOMBWI.

  Wamachinga ni watanzania wenye haki ya kuishi, na hii inawezekana tu kwa kupata riziki, tunapowatoa kwa nguvu bila kuwaandaa wateja wao na wao pia si tunawanyima riziki. Wasingegoma kama mazingira yanaboreshwa. Mfano pale Mbeya waende wapi wakati eneo la muda walilopewa liteketa kwa moto? Nchi hii ni yetu wote si ya RC na vigogo tu. WAMACHINGA ENDELEENI KUDAI HAKI YENU.

  Wasomi wenzangu hasa mlio vyuo vikuu UNAFIKI umezidi. Tumeona na tunaendelea kuona mateso kwa wanafunzi wetu hata sisi wenyewe maslahi yetu hayako sawa, lakini tumejiziba midomo sababu ya vibaraka wachache, tunajenga Taifa gani? Ndio maana wengi wanafikiria kuingia kwenye siasa kukimbia haya. WASOMI tutazame wasommi wa Kenya juzi tu wamegoma. Kama baba (WALIMU) ni mwoga watoto watakuwaje? .TUACHE UNAFIKI TUDAI HAKI ZETU ZIPO NA ZINAWEZEKANA.

  Utabiri wangu kwa hali hii maandamano yataendelea na kuwa mabaya zaidi. Tukumbuke hata wananchi wa kawaida wameanza kutoogopa tena dola, wameanza kutojali kwenda rumande na hata gerezani HII NI HATARI. Wengi wanajua silaha japo dhaifu za kukabiliana na polisi. siku moja watavumbua silaha imara zaidi. Waziri mkuu atalalamika sana lakini dawa ni moja kufanyia kazi chanzo cha matatizo na sio matokeo.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Ikiwa Waalim ni waogo wanafuzniai watakuwaje?, wewe saa ngapi ulikuwa kwenye foleni ya kushindwa kuingia ofisini? saa ngapi ulikuwa unamsikiliza Waziri Mkuu saa ngapi unaingia JF kufanya uchochezi?

  Njia za kudai haki si maandamano, hii biashara ya machinga Mbeya, kama haijadhibitiwa na kuondolewa mabarabarani inakuwa ni kero kwa wenye maduka, kwani hawa wa machinga hupanga vitu vyao nje ya maduka ya watu, nnauhakika kuna tatizo na ufunbumzi wake ni kutengewa sehemu kamili za kufanyia biashara na nnauhakika hili walifanyiwa huko Mbeya.

  Kuhusu wanafunzi kugoma, hili nalo limekuwa ni kawaida yao, na Serikali imejitia kitanzi kwa wema wake, pale ilipoamuwa kuwa kila mwanafunzi atakopeshwa, sasa wakigoma unashindwa hata kuwafukuza, utatowa wapi bajeti ya kuwapa wengine ukiwafukuza hao uliokwisha walipa? hapo sasa.

  Mimi naona ingerudishwa vilevile, bajeti ya mwanafunzi itoke "serikalini" na wawe wanalipwa kwa mahudhurio yao na si kupewa kitita "in advance" ili watapogoma ndio watokomee na wapatiwe hiyo fursa wanafunzi wengine wasiodekadeka.
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Naamini hakikuwa kichwa kimoja kilichokurupuka na kuanzisha HELSB.. Halafu adhabu ya kaburi aijuaye maiti. Usimshangae huyo lecturer kuongea namna. Na ukitaka kuujua uhondo wa ngoma uingie ucheze! Mi naona hizo huzielewi Faizafoxy. We unaelewa ile moja ya mwamba ngoma ngozi huvutia kwakee.....
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Wewe tunakufaamu msimamo wako,unatetea watawala.
   
 5. l

  lyimoc Senior Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alie shiba hamjui mwenye njaa wewe ni gamba shika adabu yako watu wanatafuta riziki unasema wanasababisha msongamano we we ni mtu gani usiewajali wenzako
   
 6. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  ff una tatizo kwenye ubongo wako na kama haujaganda basi una wadudu wanaokufanya ufikirie kwa masabburi au magamba wana kukameroon ndo mana unatetea ushuzi
   
 7. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  ff una tatizo kwenye ubongo wako na kama haujaganda basi una wadudu wanaokufanya ufikirie kwa masaburi au magamba wana kukameroon ndo mana unatetea ushuzi
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280

  Wewe mama ebu acha udaku....eneo la Makunguru ulipoanzia mzozo hakuna maduku pale ni soko la jioni ndipo wamachinga wanapanga vitu chini kusubiria watu wanaotoka maofisini. Eneo lenyewe hulijui kazi kukaa kupiga domo tu. aibu ndenda kakae mbeya utaelewa wanachopigania hawa kaka zetu wamachinga
   
 9. e

  emrema JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FF waweza kuzuia matone ya mvua sio mvua yenyewe.
   
 10. B

  Buto JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wewe ff mbona unakuwa kama ubongo wako umeganda?
   
Loading...