Haka katabia ka kuvaa malapa na socks kanazidi kukua mtaani, nini shida?

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
Wanabodi!

Mjini mjini tu unaweza kuiga jambo hata hujui asili yake ikiwa umeona wengi wanafanya.

Kuna tabia inazidi kukua tena kwa kasi sana ya wababa, wamama, wadada na hata sisi vijana wa kiume kuvaa open shoes, malapa au hata yeboyebo na socks na kuanza kula misele mitaani bila aibu.

Weekends kwenye bars na maeneo ya mikusanyiko sio ishu kumkuta sister du na kapensi kalaini na malapa na socks.

Nani huwa analeta fashion za namna hii za kudhalilisha watu!

USSR

20201217_094326.jpg
 
Ndio mwanzo wa mtindo mpya unavyoanzaga.

Linaonekana jambo la ajabu na la kushangaza wakati wa kuanza kwake. Siku zinavyoenda watu wanazoea na kuonekana jambo la kawaida, na wale waliokuwa wanashangaa wanajikuta bila kulazimishwa wanashiriki.
 
Mleta mada nadhani anaongelea dar as salaam kwenye joto mikoani huwezi kuthubutu kuvaa hivyo au pensi baridi itaua mtu

Kwenye joto fangasi ukivaa viatu mfululizo utapata
 
Kuvaa soksi ni shida! unajua maana ya shida?
Wewe usivae ila anayetaka kuvaa avae,hakuna sheria ya kumkataza mtu kuvaa soksi na malapa.
 
Kweli hakuna jipya chini ya jua. Zamani shule prep tulivaa hivi zababu ya mbu.
 
Back
Top Bottom