Hajui baba wa mtoto ni nani! Je, ni kweli?

Jerry santonga

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
642
549
Habari za muda huu wajumbe? Je ni kweli mwanamke anashindwa kujua baba wa mtoto? Ashtukie mimba ina miezi mitano?? Kweli au kuna upigaji wa wazi wazi... Je inawezekana kabisa usimjue baba wa mtoto kati ya mtu mbili ulizotembea nazo? Wa kwanza kakataa wa pili hana taarifa.

Hawa watoto wetu wa kike ni mazingaombwe, mpwa wangu mmoja wameshamtundika mimba na hajui nani ni nani kwani alikuwa anamiliki wajuba wawili na wote walikuwa wanasakata naye jeje rhumba daah inasikitisha
 
Ni ushenzi kutia mimba binti wa mtu halafu usiwajibike kutunza, hata kama binti alimiliki njemba nyingi anajua aliempa mimba
Sayansi gani mnaitumia kuthibitisha hayo?

Kwa taarifa tu ni kwamba, kama mwanamke ni malaya na anawapanga wanaume kulala naye kwa zamu, jambo hilo hakika ni gumu sana kulitambua, labda abahatishe kwa aliyechagua kumtaja.

Hapa sitaingia kindani sana, lakini kumbuka mbegu za kiume zina uwezo wa kuishi kwenye via vya uzazi vya mwanamke zaidi ya saa24.
Je kama ndani ya huo muda huo, mwanamke akawa kapevusha mayai na akatembea na wote atajuaje!

Tena unaambiwa mwanamke anaweza kupata hata mapacha(siyo identical twins) kwa wanaume wawili tofauti.

Mwenye uhakika na mwanaume aliyempa mimba ni yule anayejiheshimu na hatangi tangi na wanaume hovyo hovyo.
 
Back
Top Bottom