Haji Vs Barbara: Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu atoa tamko

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,170
103,636
Habari za wakati huu!

Ninawaomba sana wanachama, wapenzi na washabiki wa Simba tuwe watulivu na makini kuelekea fainali ya FA CUP

Uongozi wa Simba upo makini na ulishatoa maelekezo ya kutatua mgogoro uliojitokeza. Simba ni timu inayojipambanua kuendeshwa kiweledi hivyo tusimame katika misingi hiyo.

Wote wanaolumbana ni waajiriwa na muajiri yupo

Baada ya mashindano tathmini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika.

Kwa sasa mmoja wetu azingatie nidhamu, hekma na misingi ya ajira au nafasi yake katika club.

Nawaomba tuwe watulivu na tuendelee na mikakati ya michezo ijayo

Simba Nguvu Moja

Murtaza Mangungu

My Take
Bodi ichukue hatua stahiki lakini Haji Manara aonyeshwe mlango wa kutokea. Hana nidhamu ya kazi Simba Sc sio kilabu cha pombe
 
Hapa Mangungu kafunika kombe ili Mwanaharamu asepe. Sidhani kama statement hii ndo wanayohtaji wanasimba baada ya udhalilishaji wa brand uliojitokeza Jana. Mechi ya ASFC haiwezi kuwa kinga kwa watovu wa nidhamu.

Iwe ni Manara, Barbra au hata Kaduguda hatua sitahiki zinapaswa kuchukuliwa bila kubembeleza au kuonea mtu. Tatizo hili litakuwa kubwa sana undapo timu itakosa matokeo Kigoma.
 
Kaduguda anahusikaje hapa?
 
ivi wakuu mbna team zetu zinaviongozi wa kulimbikiza kutafuna mkwanja tu ivi nini maana ya CEO halafu apo apo kuna mwenyekiti wa simba ivi vyeo viwili naona kama vinafanana majukum yao ni yapi yanayowatofautisha je mwenyeliti anaweza kumsimamisha kazi mtendaji mkuu na je bodi ya wakurugenzi inaweza kumsimamisha kazi mwenyekiti
 
Mangungu naye bana eti wanaorumbana!! Hapo hakuna marumbano Bali Manara kamshambulia bosi wake kwa maneno.
Inakueje mi nimepigwa Bila kujibu halafu mtu atoe statement eti tumepigana?!
 
Halafu mmiliki anadeal vipi na staff conflicts resolution wakati kuna management?
Hapa uswahili ushaingia teyari. Hii ilibidi imalizwe na CEO wao wapate report tu,
 
Kama ni kweli Haji S Manara analipwa laki saba kwa mwezi na hana mkataba wa kazi pale simba na vile anafanya kazi kubwa, ni halali yake awe balozi wa GSM na Bidhaa za Azam Bkhresa pamoja na Asasi ili kipato chake kiendane na umaarufu alionao, kama wanataka Manara asifungamane ma GSM basi apewe mshahara unao endana na status. I stand to be corrected
 
Haswaa, leo hii ukizungumzia mtu anayeweza kutumia dakika mbili tu kuwaaminisha watu waujaze uwanja wa mkapa ni Manara,

Huyu Manara anaweza kua na mabaya yake ila ni mtu muhimu sana pale Simba.
 
Kama ni kweli Haji S Manara analipwa laki saba kwa mwezi na hana mkataba wa kazi pale simba na vile anafanya kazi kubwa, ni halali yake awe balozi wa GSM na Bidhaa za Azam Bkhresa pamoja na Asasi ili kipato chake kiendane na umaarufu alionao, kama wanataka Manara asifungamane ma GSM basi apewe mshahara unao endana na status. I stand to be corrected
Sikiliza clip ya hanspope, ina majibu yako
 
Sikiliza clip ya hanspope, ina majibu yako
Mkuu Haji S Manara pesa anayoingiza kwa dili zake za ubalozi ni kubwa kuliko hiyo ya milioni 4 ambayo atajifunga kwa Mo dewji. It's clear nature ya wahindi payment zao huwa ni ndogo kuliko zaki inayofanywa
 
Kama ni kweli Haji S Manara analipwa laki saba kwa mwezi na hana mkataba wa kazi pale simba na vile anafanya kazi kubwa, ni halali yake awe balozi wa GSM na Bidhaa za Azam Bkhresa pamoja na Asasi ili kipato chake kiendane na umaarufu alionao, kama wanataka Manara asifungamane ma GSM basi apewe mshahara unao endana na status. I stand to be corrected
Unapaswa kusikiliza na upande wa pili ,mm kabla sijasikia upande wa pili nilijua tu Kuna namna haji kulipwa hiyo pesa km posho tu ,kumbe nilikuwa sahihi maana manara aligoma kusain mkataba wa kulipwa 4m alijua fika atajifunga zaid kutangaza bidhaa zingine out of Simba.

Manara ni mtoto wa mjin haswa anajua anachokipata nje ya hiyo laki Saba lakin pia anajua umuhimu wa yeye kuendelea kuwa Simba hata kwa kulipwa hicho kiasi kidogo.

Kwa lugha nyepes ni kwamba hata asilipwe hata Mia moja lakin aendelee kusalia Simba ili apige pesa nje ya Simba huku hiyo power ya ushawish kwa makampun mengine itokane na Simba wenyew.

Ogopa kitu kinaitwa brand ndugu.
 
Back
Top Bottom