Haji Manara ni mzima kweli?

Si nasikia wameleta dawa ya sindano?
Maana vidonge Kila siku vinatesa!
Hujui kesho yako, acha utoto wa kudhihaki afya za watu

Na umri wako na kujinasibu kusoma Bado una tumia afya ya mtu kutaka kumshusha thamani acha utoto
 
Tatizo haji, post ya kwanza analalamika kuwa yanga alionewa kwa kunyimwa goli halali, kweli ni goli halali, mechi ya simba vs gwambina onyango alifunga goli halali pia kama hilo likakataliwa pia

Post ya pili analalamika simba walipewa penat ambayo sio halali kwani kagere alichezewa foul nje ya box, abasahau kuwa yanga walipewa penati kama hiyo hiyo onyangoa alipomchezea foul tuisila nje ya box
Kwa hiyo, tabia hiyo ni ya Simba na Yanga kulazimisha ushindi pasipokuwa na ushindi

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 

KUNA TOFAUTI KATI YA KUSAHAU NA KUJISAHAULISHA MASHABIKI WA SIMBA PUNGUZENI UMBUMBUMBU​

Wengi wetu tunajisahaulisha(ni kitendo cha kujisababishia kupoteza kumbukumbu kwa makusudi)

Twende sote
emoji3596.png

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya round ya pili kati ya Yanga vs Azam msimu uliopita na Azam kushinda 1-0(Prince Dube)
Jiulize ndani ya mechi ile Yanga walinyimwa penati ngapi?
Usibishe kabla ya kuitazama tena hii mechi
Lakini haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya Namungo vs Yanga kule Lindi msimu uliopita na Yanga kukataliwa goli lake kipindi cha pili(Yacouba Sogne)
Lakini haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya Yanga vs Geita Gold na kukataa magoli mawili ya Yanga(Mayele na Yusuf Athumani) Haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi za timu ambayo ikiwa haijapata goli mpaka dakika ya 89/90 basi zitaongezwa dakika 5 za kwenye kibao lakini zitakazochezwa ni zaidi ya zile zilizooneshwa kwenye kile kibao na ile timu itapata goli
Lakini haiwi mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi dhidi ya Kmc vs simba na mchezaji wa simba Erasto Nyoni akarudisha mpira golini kwa Manula kisha Salum Kabunda akawa anauwahi ule mpira ili kufunga lakini akaambiwa yupo offside lakini vilevile kwenye mechi hii hii simba walipata penati mbili(moja tu ndiyo ilikuwa ni halali) lakini hata ile ya halali mwanzo mpigaji alikosa na akaambiwa arudie tena Lakini vilevile haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya Kmc vs simba na mpira kumgonga kiunoni mchezaji wa kmc kisha likawekwa tuta katika dakika ya 80+ Lakini vilevile haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya simba vs Dodoma jiji na hawakutoa kadi yoyote ile baada ya kuonekana Kennedy Juma akiurusha mguu juu ya mchezaji wa Dodoma jiji Lakini vilevile haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi ya simba vs Namungo na hawakutoa kadi yoyote ile dhidi ya John Bocco akimchezea rafu mchezaji wa Namungo, Morrison kumpiga kipepsi mchezaji wa Namungo.

Huku Manula naye akimfuata mchezaji wa Namungo na kumsukuma baada ya kutoka na kuukosa mpira katika eneo lake
Lakini vilevile haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa waliochezesha mechi za timu fulani ambayo wao ndiyo wanaoona wanastahiki kupata mipira ya penati kuliko timu nyingine yoyote ile kwenye ligi yetu Lakini vilevile haikuwa mjadala

Waamuzi wetu ndio hawahawa wanaosababisha timu fulani ikipata sare/suluhu basi wahisi kuwa kuna hujuma na GSM wamewapa pesa timu wanazocheza nazo wao bila kuwaheshimu timu pinzani.

Yaani hii timu yenyewe inaona ndiyo ina haki ya kushinda tu kuliko timu nyingine yoyote ile Hili nalo pia halikuwa mjadala na hata wale wacha-MBUZI eti nao walidai kuwa hii timu inakamiwa

Waamuzi wetu ndio hawahawa wanaochezesha mechi za Yanga na kupata sare wakati mwingine ni za makusudi, mechi dhidi ya Namungo msimu uliopita pale Lindi, mechi dhidi ya Mbeya City msimu uliopita pale Mbeya, Biashara vs Yanga kule Mara goli la Yanga linakataliwa na Yanga kuishia kupoteza ile mechi Lakini vilevile si mjadala.

Na wala huwezi kusikia mashabiki wa Yanga wakisema kuwa hizi sare au suluhu ni kwa sababu Mo Dewji ametumia pesa kwa timu pinzani ili ziikamie Yanga

Matukio yaleyale ya kudhulumiwa wakifanyiwa Yanga huonekana kama ni kawaida vile lakini yakitokea kwa timu nyingine huonekana ni dhambi kubwa TUACHE KUJISAHAULISHA

CC: Solomon mdau jf
 
Sasa wewe zuzu unatakaje. Kachezeshe wewe.

Wee Zuzu makosa ya Jana hayawezi kujustfy makosa ya leo.

Mhuni tu km wahuni wenzio wale waliojaa kwa penati box.

Refa 1- 1 Namungo
 
Analalamikia kuhusu upewaji wa Pernati tu. Vipi kuhusu Feisal kuwa offside kabla ya Penart haijapigwa?

Nimemuuliza Feisal alifata nini pale, alichonijibu nimeishia kucheka tu.
 
Badala m deal na TFF na marefa wao, nyie mnapambana na Manara. Wakupigiwa kelele na hatua zichukuliwe kwa marefa wa aina hiyo iwe ameibeba Yanga au ameibeba Simba ni TFF dhidi ya marefa. Naweza kuishauri TFF kama refa atafanya makosa ya wazi kiasi hicho kwenye michezo mitatu atakayochezesha kwa kipindi chote cha msimu ashushwe daraja waje vijana wengine
 
Back
Top Bottom