Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Ipo siasa iliyopotea njia ndani ya nchi yetu. Ipo mikakati mfu yakiwekezaji isiyo na tija kwa Taifa letu. Wapo watu wanaamini kila Jambo lazima tuwe na viongozi wanaoongozwa na mfumo wa kisiasa. Wapo watu wanaishi vizuri kwa mwonekano wa nje lakini si kwa mwonekano wa ndani. Chama kinatafuta kushika kila Kona yenye wananchi, ajira zinatoka kwa wale wanaoweza kuweka maslahi ya chama mbele siyo wanaotakiwa kusogeza fani au shirika mbele.
Wapo watu wanataka kutuaminisha kwamba Manara aliamka asubuhi tu nakujikuta yupo Yanga, naomba niwaambie leo hii wafadhili wa Yanga SI Mashabiki wa Yanga na waumini wa mpira bali niwafanyabiashara ambao kwao uwekezaji wowote hata usio na tija ila wenye multiplayer effects kwao basi wataukumbatia. GSM ni akina Nani? Na manara ni Nani? Tunataka furaha ya leo bila kuwaza furaha ya kesho.....hakuna uwekezaji serious utatokana na GSM na hakuna hamasa serious na yakudumu itakayotokana na Manara. Isipokuwa ipo faida ya mnyororo wa biashara za watu flani na malengo ya kisiasa vitapitia upenyo huu kuvuka na kwenda mbele.
Yupo Fred Vunja Bei ambaye akaunti zake za mitandao ya kijamii zinaonyesha hadi kufikia mwaka Jana alikuwa anauza nguo za kiume zisizovuka 19000@ trauzer au t-shirts na zote hizi alikua anaagiza nakuuza kama wanavyouza machinga wengine. Leo sawa tunamwita mjasiriamali na kijana aliyepata mafanikio Tanzania, we are wrong Hawa siyo wafanyabiashara bali niwanasiasa waliotegesha mirija yakupata feva nakupewa kazi kwa kuzingatia regime iliyopo. The guy can not compet kwenye tenda, na hii ipo wazi. Leo mfumo ukibadilika hakuna uhakika kwamba Vunja Bei shops zitakuwepo, na hata kwa mfumo uliopo hakuna uhakika kwamba Vunja Bei wanazo bidhaa zakuvuka mpaka zinazozalishwa kwa jina na umiliki wao. Simba na Yqnga walipaswa kuwekeza ndani na nje na ili kufanikisha ilo wangeondoa kupeana tenda kisiasa wakapeana tenda kulingana na ushindani wa biashara.
Manara na Vunja Bei ni watu wanaokwamisha ushindani wa fikra kwa sababu awafanyi mambo kwa nguvu zao wenyewe Bali wanabebwa na mfumo...kwenye business mtu yeyote au kampuni yoyote inayoishi kwa kutegemea mfumo uliopo wa siasa itakufa mara mfumo utakapokufa au baadhi ya watu kubadilika.
Timu za Ulaya zipo beyond mfumo wa kisiasa ndo maana any regime haiwezi kuziathiri. Sisi tumefanya Yanga na Simba kuwa matawi ya vyma vya siasa. Tushangilie leo bila kujiwekea malengo yakushangilia kesho. Tuuze utu na uwezo wetu kwa watu wasiothamini maumivu yetu pale wanaposhiba.
Nimtazamo binafsi na siyo lazima iwe kweli Wala isiwe kweli.