'
1626928921-picsay.jpg
 
Hili saga linachanganya naona mapema Sana kusema kitu. Nakumbuka Shafii Dauda aliwahi kumwambia Haji kipindi kile wana kaugomvi.
 
Kuna wakati inabidi tuwe wakweli
Pamoja na mengi mazuri ambayo Manara ameifanyia Simba nafikiri umefika wakati wa kumuacha aende.. Manara ana mapungufu mengi ya kiweledi tena mapungufu ambayo hata mtoto form 1 anaweza kuyazuia.

Manara anapenda kukimbilia mitandaoni ili apate huruma ya mashabiki. Manara anahisi Simba inamuhitaji yeye kuliko yeye anavyoihitaji Simba

Nadhani ni wakati wa kumuacha manara aende iwapo tuna waadhibu kina Mkude pia tusiwaache kina Manara
 
Kati ya Manara na Barbra nani boss? nmesikia Manara anatishia kumfukuza kazi boss wake
Manara chizi kweli. Toka Ile press kabla ya mechi ya tarehe 25 mi nikaona ana connection na upande wa pili na anatumia sana coded language. Ukimsikilizaga kama anaiongelea Simba lakini hua anawapaga ujumbe mahsusi tena kwa msisitizo utopolo, wapo wanaomuelewa na huwa wanafanyia kazi hasa. Kwa Simba ifike sehemu wafanye nae makubaliano ya pande mbili waachane kiustaarabu tu
 
Barbara anaupiga mwingi sana

Manara toka huwezi kushinda vita ya kifamilia kwa akili yako unafikiri Barbara ni rahisi kutoka ukabaki wewe tuliwaambia kwamba hiyo timu ni ya kifamilia zaidi kuliko unavyofikiria kwanza hujiulizi huyo CEO aliingiaje hapo
 
Asalamareku mtanzania Karibu tena kwenye show za vpl kwenye mtanange mgumu ni dabi kubwa uwenda Africa mashiriki na kati waweza iita simba derby Wana lunyasi kati ya Haji sande manara vs Barbara Gonzalez uwezekano wa mvua kunyesha ni asilimia 40 timu zimekwisha kuingia uwanja huku mwamunzi wa kati ni bodi ya simba na mwamunzi wa kulia assistant refaree mshabiki na wanachama wa simba mwamunzi wa kushoto ni moooo energy zikiwa zimebaki sekunde kadhaa mtanange kuanza na refa anampa idhini kuanza Haji naaam kipyanga kimeshasikika na show imeanza Haji Haji na mpira Haji anasakama lango la Barbara, haji anaachia shuti nje kidogo ya kumi na 8 unakwenda nje kidogo ya lango wakati huo huo mwamzi wa pembeni MO akinyoosha kibendera kumaanisha ni offside lkn inaonekana sande alikuwa akifanya dribbling kutokea langoni kwake wacha tuone marudio ya picha kama tutanufaika nayo kutoka kwa lupanda HD mtumbad kwako John samweli, ilikuwa semi voly ambapo manara alikunjuka shuti kali na kwenda nje kidogo ya mringoti mitatu

Aggregate inasoma sifuri bin sifuri Usiyotarajia yanaweza kutokea dabi haina mwenyewe anachua Sasa Barbara barabara na mpira oooh sande kalabwa bonge la tobo mpka mwamzi wa kati anachekelea Barbara anakunjuka shuti kali ninagonga mtambaa wa panya na kurudi ndani anainasa tena barabara anacheza pasi fupi fupi nje ya kumi na nane lengo ni kumvuta adui asogee nje ya lango barabara anapigia kibao kataa kwenda kwa winga yake manara anakimbia kwa speed kwenda kudhibit na kuchukua mpira mwamunzi wa pembeni kibendera kipoo juu huku Barbara akiwa chini anagaagaa kwa maumivu wacha tuone picha za marudio, ohoo mwamunzi wa pembeni MO kaenda yombo na kumpa faida Barbara ikiwa si haki yake ohoo hahaha Barbara analia kwa uchungu pale chini lengo ni kumhadaa mwamzi wa kati manara anaonywa kwa mdomo akiambiwa Mara ya pili Sitakusamehe huku manara akijiuliza kwa kosa gani nilofanya na mpira ni dakika ya 43

Refaree anamaliza mpira bila ya nyongeza yeyote Sande anatoka huku akifoka kwa kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi naam timu zinakwenda kupumzika kujianda na dkika 45 zingine za kipindi cha pili mimi baki kwenye runinga yako na Mimi ni Baraka Hudson mpenja sauti ya radi mtafasiri wa dakika hizi 90 nikiwa na John samweli
 
Back
Top Bottom