Haji aondoke tu maana anaitumia Simba kwenye personal gain zake haswa hayo matangazo ya akina GSM. Yaani mchana msikitini usiku kanisani is it possible?!
20210722_053226.jpg

siku nilipoona ameandika haya madudu nikajua huyu ni wa kuondosha haraka. Eti Simba & Bugati, huku ni kujiona mko level na Simba. Tatizo wabongo hatuna washauri tuna mashabiki
 
Leo nimesikia audio ikitembea mitandaoni inayodaiwa kuwa imerekodiwa na Manara akimtuhumu kwa mambo mengi Barbara.Inaonekana hawa watu wana mgogoro wa mda mrefu na hawawezi kufanya kazi tena pamoja.Wewe kama mwanasoka unadhani nini kifanyike?...
Mi Simba damu, ila huyo Manara hafai kabisa,mswahili Sana kumbe
 
Utopolo kwa mlivyoshikwa vibaya na Manara hili kwenu jema..Hatoki mtu hapo,Manara ataendelea kuwakeraa.
 
Manara hawezi kuendana na Simba ya sasa,sijawahi kumkubali ,kwenye uhamasishaji sawa lakini ana uswahili mwingi,Bidada amesimama kama CEO kwenye nafasi yake na kaachiwa asimamie mambo mengi kiasi kwamba hata mambo ya media yachujwe ndo Manara aongee ,Sasa manara hataki hivo anataka kila kitu awe wa kwanza...
Manara kichwani hamna kitu,aondoke tu
 
Huwezi kutengeneza Mind game inayogawa mashabiki wako mwenyewe. Yanga walipokuwa wanasema hatuchezi July 3 walikuwa na sapoti ya mashabiki. Sasa Leo unaletaje mind game kuwagawa watu wako?
Mashabiki hatujagawanyika hata kidogo ngoja baada ya 25/7/2021 pale lake Tanganyika ndo utajua Simba ni kampuni na sio Mali ya mtu binafsi kwa Sasa Simba inaendeshwa Kama real Madrid au Bayern Munich
 
Manara mwenyewe akili kubwa, ashajua kinachoenda kutokea kwahiyo anachofanya sasa ni kutafuta public sympathy
Manara kumbe akiri zero, confict za ofcn kazileta ktk mitandao, bado anamtishia boss wake, duuuuh

Weredi na uswahili havikai pa1

Muda wa manara kupisha kiti umewadia
 
Manara uswahili unamdanganya.. manara hana uwezo wa kumtoa simba babra wala mo.. ila babra na mo wana uwezo wa kumtoa simba manara..

Mwenye pesa sio mwenzako.. hao kina chama na konde boy unawaona sababu ya kina babra na mo hapo.. hizo robo fainali za klabu bingwa unaziona sabab ya kina babra na mo.

Je manara ana uwezo wa kulipa mshahara hata wa zimbwe tu?
Weledi na uswahili havikai pamoja
 
Nilipenda san hamasa zake. Lakini tatizo la watanzania mafanikio kidogo anajiona ana uwezo sawa au kuliko taasisi. Haji amekuwa kama limbukeni wa umaarufu. Nadhani muda wa kutafuta changamoto sehemu zingine ni sasa...
Na kashaipa sababu bodi kumfukuza kazi, conflicts za ofisini anazipeleka Instagram.

Weledi na uswahili havikai pamoja

Na tuone Haji bila Simba kama hao kina Asas, GSM, Bakhresa kama watamthamini
 
Back
Top Bottom