Leo nimesikia audio ikitembea mitandaoni inayodaiwa kuwa imerekodiwa na Manara akimtuhumu kwa mambo mengi Barbara.Inaonekana hawa watu wana mgogoro wa mda mrefu na hawawezi kufanya kazi tena pamoja.Wewe kama mwanasoka unadhani nini kifanyike?Au ni madhara ya Mo kujimilikisha timu kifamilia?🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Kwenye audio hyo Manara kaenda mbali zaidi na kumtishia Barabara sijui Barnaba sorry Barbana,duuh Barbara kwamba ataiacha timu kama alivyoikuta.Sasa hapo sijui nani anaondoka nani anabaki.

Povu ruksa nina nguo chafu hapa.


Najaribu kuapload audio husika hapa inazingua
Manara hafai kuwa msemaji wa Simba kwanza hajuwi mpira na hana akili. Yule ilibidi awe mwuimbaji bongo fleva tu au taarab maana hata singeli na muziki wa dansi hauwezi.
 
Una hoja kubwa sana... timu ambazo zinashindana na simba caf hazina nafasi wala roles za watu kama manara katika staffs wao... ukitizama documentary ya enyimba wakati wanabadilika mwaka 2000 walitoa tenda kwa PWC proffessional consultancy firm na hao pwc kuna vyeo vingi sana walivifuta pale enyimba ili timu iwe ya kisasa. Na vikaleta mgogoro kwa wanaotolewa kazini.. ila miaka miwili mbele wakaenda twaa ubingwa wa caf champions league..

Kuna wakati ili usonge mbele unahitaji ubadili viatu vizito na uvae raba ili utembee haraka
Manara hawezi kuendana na Simba ya sasa,sijawahi kumkubali ,kwenye uhamasishaji sawa lakini ana uswahili mwingi,Bidada amesimama kama CEO kwenye nafasi yake na kaachiwa asimamie mambo mengi kiasi kwamba hata mambo ya media yachujwe ndo Manara aongee ,Sasa manara hataki hivo anataka kila kitu awe wa kwanza .

Kwanza hata kama we ni Mo ingekuwa ngumu kumvulia Manara na matangazo yake ,amekuwa balozi wa karibia washindani wote Mo kibiashara. ASAS yeye ,GSM yeye ,Azam media yeye. Boss anakulipa halafu we una promote bidhaa za washindani wake ? Manara anawasifu GSM ila anawakejeli Yanga ,yeye hajui hata huo umaarufu amepata kupitia Simba hamna ambaye angemfahamu,atapiga kelele week nzima atasahaulika Simba itaendelea
 
Simba bingwa FA kilichowakuta yanga nusu fainali ya FA ndicho kitakachowakuta fainali, simba na yanga mechi zao zinachezwa sana nje ya uwanja

Hii mechi wanayanga wanamatumaini makubwa sana ya kupata ushindi, wamewafunga simba Mapinduzi na kwenye ligi pia, asikuambie mtu wanachokifanyaga simba caf champions leage ndicho walichokifanya kuelekea mechi hii ni kufuru. Kwa faida tu fuatilieni huyo mwamuzi wa hiyo mechi, nasema ivi hawatoki kivyovyote vile.
 
Hizi huu sio mpango wa CCM kututoa kwenye reli? Au sio mpango wa Simba kutaka kuichanganya Yanga kisaikologia?

Nitarudi Tena nione Kama ni ugomvi kweli
 
Nilipenda san hamasa zake. Lakini tatizo la watanzania mafanikio kidogo anajiona ana uwezo sawa au kuliko taasisi. Haji amekuwa kama limbukeni wa umaarufu. Nadhani muda wa kutafuta changamoto sehemu zingine ni sasa.

Ni kama anataka awe untouchable hivi, yeye nani asiguswe au kuhojiwa? Kama mwajiriwa na binaadam huwezi kuwa sawa muda wote. Kuna muda utatoka nje ya mstari mwajiri lazima afanye wajibu wake.

Akiguswa anapeleka taarabu insta,anakuwa kama mwanamke mwenye kiranga, kifinyo kidogo tu mtaa mzima anajua. Mdomo mwingi huponza kichwa. Akibaki bila Simba akili itamrudia
 
Kikweli sijui undani wa sakata hii ila Haji amechoka, apumzike aje mtu mwingine mwenye uwezo zaidi. Ile press ya kabla ya game na Yanga ni ujinga mtupu alikuwa anaongea.

Unajiuliza hiki ndio ametumwa na klabu? au anajiropokea tu yeye. Simba wamemchoka Haji kitambo sana ila walikuwa wanamlia timing tu.
 
Back
Top Bottom