Haji Manara acha Kufanya Wana Simba SC wote ni 'hopeless' kama ulivyo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,874
Hakuna Mtu wa Simba SC hasa hao Viongozi uliowataja wakiongozwa na Salim "Try Again' Wala Nahodha wa Simba SC John Boko aliyekushauri kuwa usifanye ile Press Conference yako uliyoiahidi bali dhamira inakusuta na roho yako ya Kinafiki inakutesa.

Kama hawa uliowataja hapa unawaheshimu na kuheshimiana nao sana tu kwanini ulipokuwa unatishia Kufanya Press Conference yako Jana (Jumatatu) au Leo (Jumanne) hukuwafikiria na usiitoe ile Ahadi yako ambayo tena uliitoa kwa Dharau, Nyodo na Kiburi kingi?

Haji Manara acha 'Kuzuga' Watu na kutufanya wana Simba SC wote (GENTAMYCINE nikiwemo) ni Wapuuzi (Hopeless) kama ulivyo Wewe ambaye bahati nzuri wengine tunakujua A to Z na hata kwa baadhi ya Dada zako wa Kwenu pale Buguruni na Ilala baadhi yetu ni 'Mashemeji' zako ila hujui tu na tunakuchora (tunakuangalia) Kimtindo.

Ukweli ni kwamba umesitisha kufanya hiyo Press Conference yako Jana na Leo (Wiki hii) kama ulivyopanga na kuahidi kwakuwa umepima kuwa hata ukisema hutosikilizwa na mwana Simba SC yoyote sana sana utaendelea tu Kupuuzwa na Kudharaulika kama siyo hata Kuchukiwa.

Najua uliahidi vile kwa 'Majigambo' kufanya Press Conference ukiwa una uhakika wa 100% kuwa kwa 'Usaliti' wako dhidi ya Simba SC na 'Siri' ulizowapa Yanga SC (kama ambavyo umekuwa ukiwapa ndiyo maana Mechi zetu na Yanga SC katika Ligi Kuu huwa ni ngumu) basi juzi katika ASFC Final Simba SC angefungwa na Yanga SC ila Matokeo yake Simba SC si tu imeshinda kwa Kumfunga Yanga SC bali pia imeutwaa Ubingwa wa TFF ASFC kwa Mara ya Pili mfululizo.

Tunajua Simba SC ingefungwa na Yanga SC (kama ulivyokuwa umekusudia ) Basi hiyo Press Conference yako ungeitumia katika Kujitetea kwa kila namna, kusema Unaonewa, Kumshambulia zaidi CEO Barbara na ungejisifu kwa kila namna na najua Wana Simba SC wengi pia wangekuamini na Kuuchukia Uongozi ila bahati mbaya Kwako na nzuri Kwetu ni kwamba Simba SC imeshinda Juzi.

Na ulivyo Mnafiki tena uliyekatika Mshipa wa Aibu baada ya Kuona Simba SC imeshinda Juzi huko katika Social Media Platforms zako Kutwa unajifanya Kuisifia Klabu, Wachezaji na Mashabiki huku hapo hapo ukijisahaulisha kwa Makusudi kuwa Jana na Leo uliahidi Kutema Nyongo (Kuisema vibaya) Klabu ya Simba SC kiasi cha kutaka 'Kuichafua' kabisa.

Sasa tumeshajua kuwa kumbe Mzee Mpili na Watu wa Yanga SC walipokuwa wakijigamba (wakijinasibu) kuwa wana Watu na Simba SC 'hachomoki' kwa Yanga SC iwe isiwe walikuwa wakimaanisha kuwa ndani ya Klabu ya Simba Wana 'Kirusi' chao 'tukuka' ambacho ni Wewe Haji Manara.

Najua tokea Juzi Haji Manara unahangaika Kumpigia Simu na hata Kutaka Kuonana na Tajiri 'Mwekezaji' Mohammed Dewji ila hapokei Simu zako na sasa unamsumbua 'Mwandamizi' Mmoja (namba Tatu) katika Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili akuombee Msamaha kwa Tajiri Mo Dewji na urudi katika Nafasi yako ambaye kwa hali ilivyo sasa ni 'automatically' kuwa Wewe ni Msemaji tena wa Simba SC isipokuwa Bodi inasubiri Kukutana, Kukujadili Kisha itoke na Official Statement kuwa you're no longer our Club Spokesperson hivyo uende huko Yanga SC au GSM 'wanaokutumia' ukawe Msemaji na Chawa wao pia.

Watu wa Simba SC (tena nikiwemo mno Mimi GENTAMYCINE) tulikupenda sana Haji Manara na hata 'Kukutetea' kwa kila hali ila kitendo chako cha 'Kutusaliti' Simba SC na kutumika na Yanga SC kupitia Nguvu ya Baba yako Mzazi, Mkeo, Mstaafu wa Nchi Mmoja na Marafiki zako wa Utotoni akina Gharib Said Mohammed (GSM) na Injinia Hersi Said kumetufanya 'tukuchukie' ghafla na labda tukiambiwa tupendekeze Adhabu inayokufaa tutaomba utembee kwa Miguu Mikoa yote nchi nzima ukawaombe Msamaha wana Simba SC na ukihurumiwa na kutakiwa kurejea ndani ya Simba SC yetu basi Cheo pekee ambacho ningeomba upewe ni cha kuwa Mkuu wa Kuangalia Usafi wa Mazingira na Vyoo vya Wachezaji wakiwa Kambini kama vimejaa au bado.

Na una bahati mno umesitisha (tena kwa Kusalimu Amri) kufanya hiyo Press Conference yako uliyoiahidi kwani GENTAMYCINE nilikuwa nasubiri uimalize kisha niuombe Uongozi wa Simba SC uniachie Mimi peke yangu nimalizane na Wewe kwa 'Kukuumbua' na mengi uliyoyafanya ndani ya Simba SC ambayo ungeshangaa nimeyajuaje na nakuambia ungejuta Kuzaliwa Kudadadeki.

Tena nakuomba kuwa Mpole sana sawa?
 
Kapima kina cha maji kaona kina kirefu kaamua kula kona kijanja kwa gia eti eti watu wameshauri asifanye hiyo
"press conference".

Kaondoka Senzo akiwa mtendaji mkuu na mafaili yenye siri zote za Simba lakini kachemsha mwaka wa pili sasa amefanikiwa tu kupata kikombe cha mapinduzi basi itakuwa yeye Haji bana.

Yeye aondoke tu kiustarabu huwezi jua labda miaka ijayo anaweza kurudi kufanya kazi Simba.
 
Tuliza Povu ndugu yangu!

Either wewe ni Yanga (aka Utopolo) au Mpambe wa wanaomchukia Manara Simba, au mwandishi mmojawapo anayeona Haji anazidi kuwa maarufu, au una chuki binafsi.

Haji ana kasoro moja tu kuhamaki. Lakini uongo au tamaa ya kununuliwa sio asili yake. Halafu Haji ni maarufu sana (umpende umchukie) huo ndio ukweli. Makamba na Boko kuongea na Manara hakuna Jipya!
 
Mimi nilikuwa namsubiria tu alete wazimu wake nimmalize na ile ishu yake na Mzee Tozi,na ndiyo angeenda kuitafuta sumu mwenyewe anywe. Asione tumemkalia kimya tuna vimeo vyake kibao.
Mkuu em iandikie uzi huu 'issue' ili kila mwana jf aielewe vizuriiii.
 
Hakuna Mtu wa Simba SC hasa hao Viongozi uliowataja wakiongozwa na Salim "Try Again' Wala Nahodha wa Simba SC John Boko aliyekushauri kuwa usifanye ile Press Conference yako uliyoiahidi bali dhamira inakusuta na roho yako ya Kinafiki inakutesa...
Kwa mara ya kwanza naunga mkono hoja yako.
 
Hakuna Mtu wa Simba SC hasa hao Viongozi uliowataja wakiongozwa na Salim "Try Again' Wala Nahodha wa Simba SC John Boko aliyekushauri kuwa usifanye ile Press Conference yako uliyoiahidi bali dhamira inakusuta na roho yako ya Kinafiki inakutesa...
Ha ha ha ha ha 🤣🤣

MTUTSI BANYAMULENGE katika ubora wako.....

Nimecheka sana....

Haji anajifanya KABOBEA sana katika propaganda na mbinu za kuzamia mbizi....nawe ukamuibukia Upande wa pili.....🤣🤣

#DaimaMbeleNyumaMwiko
 
Tuliza Povu ndugu yangu!

Either wewe ni Yanga (aka Utopolo) au Mpambe wa wanaomchukia Manara Simba, au mwandishi mmojawapo anayeona Haji anazidi kuwa maarufu, au una chuki binafsi...
Haji nje ya simba hana tofauti na harmorapa tu, subiri uone muda utakavyoamua, haji kabla hajaja simba alikuwa anajulikana na baadhi ya watu tu kwa kutapeli magari na kumuweka mama yake bond huko polisi
 
Back
Top Bottom